https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, February 23, 2013

Yanga yaichana chana Azam FC wataalamu wa lamba lamba

Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao alilofunga Haruna Niyonzima....
                               Mshambuliaji wa Yanga Hamis Kiiza na beki wa Azam, Hamis Mcha
 Mshambuliaji wa Yanga Hamis Kiiza akiwa na mpira huku beki wa Azam, Hamis Mcha akimzuia wakati wa mchezo wa ligi kuu uliochezwa uwanja wa Taifa

Haruna Niyonzima akishangilia bao kwa staili ya aina yake
 
Na Rachel Pallangyo, Dar es Salaam

TIMU ya Yanga leo imeibuka na pointi tatu kwenye mchezo wao dhidi ya Azam FC uliochezwa uwanja wa Taifa.
Yanga ambao walionekana kushambulia sana mwanzoni lakini baada ya dakika 20 walionekana kusimama kana kwamba wanatazama mechi na Azam kuwashambulia lakini umakini wa washambuliaji uliwakosesha mabao ya wazi.

Baada ya kosakosa hizo dakika ya 32 mshambuliaji wa Yanga Hatuna Niyonzima aliwainua mashabiki wa Yanga kwenye viti baada ya kuunganisha pasi ya Jerryson Tegete na kuandika bao la kwanza na la pekee kwa mchezo huo.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...