https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, February 21, 2013

Diamond anatisha: Aendelea kuwafaidi mabinti wa watu jamani



Diamond akiwa na demu wake mpya.. Uhusiano wao huu umeanza kwa mbwembwe nyingi, ingawa jamaa anazuga kama kawaida yake.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul, Diamond, ameshangaza watu kwa kitendo chake cha kuendekeza kuvua nguo watoto wa watu, ikiwa ni tabia inayozidi kuota mizizi kwa mkali huyo.
 
Diamond na Jokate Mwigelo enzi za uhusiano wao

Hadi sasa, Diamond ametoka kimapenzi na wasichana kibao, akiwamo Wema Sepetu, Jokate Mwigelo na sasa yupo na Vj Penny, uhusiano ulioanza kwa mbwembwe lukuki.
Wema Sepetu, akiongea kwa jazba.

Jana usiku alipokuwa akizungumza katika kipindi cha mapenzi kinachorushwa na Clouds FM, kinachoongozwa na mtangazaji wake, Diva, Diamond alionekana kujikanyaga zaidi kwa kushindwa kuzuia hisia zake kwa akina dada.

Diva alimuuliza Diamond idadi aliyowavua nguo mabinti, swali ambalo lilionyesha kuwakera watu wengi waliokuwa wakifuatilia. Kwa kipindi cha miaka miwili sasa, stori zote za msanii huyo zimekuwa zikihusiana na wanawake kama ilivyokuwa kwenye nyimbo zake nyingi kuwa za mapeni.

Hata hivyo, anapobanwa, mkali huyo hudanganya kuwa ni rafiki tu ingawa baada ya muda mchache hutoa ukweli wote. Wakati anaanza kuwa na Wema Sepetu, Diamond alikanusha kila wakati, hata hivyo baadaye alikuwa wazi.

Na alipoachana naye na kuanza uhusiano na binti Mwigelo, alikuwa akifanya siri hadi pale alipokuwa wazi, ingawa uhusiano wake haukudumu sana. Kwa kiasi kikubwa, Diamond amekuwa akiibua maswali mengi kutoka kwa wadau wake wakitaka kujua kuwa kama ataendelea kuwavua nguo akina dada hadi wakati gani?

Uhusiano wake mpya na VJ Penny, utachukua muda gani kwa msanii huyo anayetamba na nyimbo mbalimbali, vile Mbagala, Kesho, Kamwambie, Nataka Kulewa na nyinginezo zinazofanya vyema katika vituo vya redio na televisheni.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...