https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, February 25, 2013

Serikali yaingilia kati Uchaguzi TFF, yapinga Katiba yake



Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara.

SERIKALI Serikali kwa kupitia Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo,  Dk.Fennella Mukangara,  imeingilia kati na kubadilisha mchakato wote wa uchaguzi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF),  kwa madai ya kuwa Katiba iliyotumika si halali.

Habari zilizotufikia Handeni Kwetu leo, jijini Dar es Salaam zinasema kuwa Mukangara aliitaka TFF kufanya mchakato wao upya kwa kuelekea kwenye uchaguzi huo kwa kuhakikisha kuwa wanatumia Katiba ya mwaka 2006 na sio mpya iliyozua utata kwa wadau wa michezo hususan mpira wa miguu.

Waziri huyo alisema kwa kutumia Ibara ya 10 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumuondoa msajili wa vyama na vilabu michezo. Sakata hilo lilikuja siku chache baada ya Kamati ya Uchaguzi na ile ya Rufaa ya TFF kuwaengua katika mbio za uchaguzi huo, Jamal Malinzi na Michael Wambura hivyo kuzua zogo kubwa.

Wiki iliyopita, Serikali kwa kupitia Waziri huyo wa Michezo, ilifanya kikao cha pamoja na viongozi wa Baraza la Michezo, akiwa na nia ya kupewa ushauri na kuangalia jinsi mchakato huo ulivyokwenda hadi kuzua mzozo huo.

Hata hivyo, TFF wao, kwa kupitia Rais wake, Leodgar Tenga, ilitangaza kusimamisha uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Februari 24 mwaka huu, kwa madai kuwa utafanyika baada ya kikao cha wajumbe wa FIFA wanaotarajiwa kufika mapema mwezi ujao.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...