https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, February 23, 2013

Ally Choki aanza mbwembwe na Extra Bongo yake


Ally Choki, Mkurugenzi wa Extra Bongo

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki, amesema kwamba sasa wamekuwa imara zaidi tofauti na walivyoanza kwa kwa kufanya juhudi kuwapa raha mashabiki wao.

Akizungumza na Handeni Kwetu, Choki alisema kuwa hata bonanza lao wanalopiga Garden Breeze, Magomeni kila Jumapili, limepata mashabiki wengi kila wiki.

Alisema hali hiyo inawapa imani kuwa maendeleo yao ni mazuri tofauti na walivyoanza, wanamuziki wengi wakitokea katika bendi za watu, akiwamo yeye aliyekuwa Twanga Pepeta.

“Sasa naweza kusema kuwa bendi yetu imeshakuwa imara zaidi na ndio maana mashabiki wengi wanaingia kwa wingi kwenye shoo zetu kila siku ya Mungu.

“Naamini kinachofuata sasa ni mafanikio katika ramani ya muziki wa dansi kutokana na juhudi zetu, mvuto na mipango ya kufanya shoo za aina yake kwa ajili ya kuwapatia burudani kamili wadau wetu,” alisema.

Extra Bongo imepangwa kusindikiza uzinduzi wa bendi ya Victoria Sound, ikiwa chini ya Mwinjuma Muumini, unaotarajiwa kufanyika Machi Mosi mwaka huu katika Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...