https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, February 19, 2013

Makabu amdunda Gorgiladze Afrika Kusini



Ilunga Makabu kulia, akiwa na mpinzani wake, Gogito Gorgiladze.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MAPAMBANO mawili yenye mguso wa aina yake Bara la Afrika, yamefanyika katika majiji mawili ya Johennsburg, Afrika ya Kusini na Tunis, Tunisia, kwa kushirikisha miamba miwili, kati ya Ilunga Makabu, mwenye asili ya nchini Kongo na Gogito Gorgiladze wa Georgia, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Ilunga Makabu

Katika pambano hilo la raundi nne, lilikuwa la kugombea Ubingwa wa Dunia wa vijana walio chini ya miaka 25 katika uzito wa Cruiserweight, ambapo Makabu aliibuka na ushindi katika patashika hiyo.

Taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari na Rais wa Shirikisho la Ngumi Afrika na Ghuba ya Uajemi, ambaye pia alikuwa mmoja wa waamuzi katika pambano hilo, Onesmo Ngowi, ilisema kuwa mambo yalianza kujionyesha katika raundi ya kwanza tu wakati bondia Makabu alipokuwa anarusha ngumi ya mkono wa kushoto ambayo ilikuwa inafanya madhara yasiyojificha kwa Gogito.

Katika raundi ya pili na ya tatu Gogito alikuwa anarudi nyuma na kuongea kana kwamba anamwambia Illunga asimwadhiri mbele ya watu lakini Mkongo man Makabu alisonga mbele akirusha makonde mazito bila huruma.

Ilipoanza raundi ya nne (4) Ilunga alirusha makonde sita ya kasi ambayo yalimfanya referee wa mpambano huo Wally Snowball wa Afrika ya Kusini kuingialia kati na kusimamisha mpambano huo!

Golden Gloves ya Rodney Berman ndiyo iliyoandaa mpambano huo na Illunga amepangwa kuteta taji lake mwezi ujao nchini Monaco katika tamasha la “The Last Man Standing” litakalofanyika katika jiji la Monte Carlo.

Katika pambano la nchini Tunisia, bondia kutoka nchini Belgium, Ayoub Nefzi, alimtwanga mpinzani wake mwenye asili ya nchini Ghana, Ishmael Tetteh, katika raundi ya 7, ambapo walipigana katika jiji la Tunis na kuvutia hisia za wengi.

Mpambano huo ulikuwa wa kugombea Ubingwa wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya kati (IBF AMEPG) katika uzito wa Jr. Middle na uliandaliwa na Halmashauri ya jiji la Tunis katika juhudi zake za kukuza ‘Utalii wa Michezo’.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...