Katibu mkuu wa chama cha
CCM, Abdurahman Kinanan akifungua pazia kuzindua tawi jipya la chama hicho ndani
ya kata ya Bunyambo,Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma mapema leo
jioni.
Ndugu kinana akishiriki
ujenzi wa ofisi ya tawi jipya la chama cha CCM kata
ya Bunyambo,Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma mapema leo
jioni.
Kinana akisomewa
taarifa kutoka kwa wanachama wa chama cha CCM,mapema leo
jioni.
Ndugu Kinana akizungumza na
wanachama wa chama hicho sambamba na wananchi wa kata hiyo ya Bunyambo,Ndugu
Kinana aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni mbili kukamilisha ujenzi wa
tawi hilo jipa la chama hicho.
Ndugu Kinana akizungumza na
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kumwambu,Wilaya ya Kibondo,Ndugu Kinana
alikwenda shuleni hapo kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo na pia
kushiriki ujenzi wake,pia aliahidi kutoa Solar Pannel kwa ajili ya kuzalisha
umeme ofisi za walimu,Kompyuta moja,seti ya jezi mbili sambamba na mipira miwili
kwa ajili ya shule hiyo.
Ndugu Kinana akishiriki
ujenzi wa shule ya sekondari ya Kuwambu akiwa sambamba na baadhi wa viongozi wa
Wilaya na mkoa kutoka chama cha CCM.
Wazee wa chama wa
shina,Matawi,kata,Madiwani Wilaya,Wazee pamoja na Jumuiya kwa ujumla
wakishangilia jambo kwenye mkutano wao wa ndani uliofanyika kwenye ukumbi wa
Vijana,wilayani Kibondo.
Ndugu Kinana akizungumza na
Wazee wa chama wa shina,Matawi,kata,Madiwani Wilaya pamoja na Wazee,lengo ikiwa
ni kuwasilisha taarifa ya kazi za chama na serikali,Ndugu Kinana ameahidi kutoa
kiasi cha shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia shunguli mbalimbali za
Vijana sambamba na hilo Kinana ameahidi kutoa kiasi cha shilingi Milioni tatu
kwa ajili ya kuwasaidia Walemavu.Mkutano huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa
Vijana,wilayani Kibondo,Mkoani Kigoma.
Ndugu Kinana akisalimiana
na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibondo,Emmanuel Gwegenyeza,pichani kati ni Mkuu
wa Wilaya ya Kibondo,Venance Mwamoto pamoja na Kada wa chama hicho,Matoni
Nyobeye,mara baada ya kuwasili kijiji cha Kilemba,wilayani Kibondo mapema leo
jioni.
No comments:
Post a Comment