Kocha wa Yanga, Ernest Brandts
Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MABINGWA
wa zamani wa Tanzania Bara, Yanga SC, Jumamosi inatarajia kujitupa uwanjani
kumenyana na Black Leopard inayoshikilia nafasi ya 12 katika Ligi Kuu ya Afrika
Kusini, mchezo uliopangwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Katika
mchezo huo, viingilio vimepangwa kuwa shilingi 5,000, viti rangi ya Chungwa Sh
10,000, VIP C Sh 15,000, VIP B Sh 20,000 wakatia VIP A Sh 30,000.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam, Kocha mkuu wa Yanga Ernest Brandts, alisema mechi za
majaribio kwa Yanga itazisaidia timu kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa
Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
“Katika
msimu wa mzunguko wa kwanza, sikuwa na timu ila baada ya kukabidhiwa timu,
niliomba uongozi tufanye maandalizi ya kutosha sambamba na kupata mechi nyingi
za majaribio ili kuweza kuweka timu fiti kwa ajili ya mzunguko ujao, hivyo
mechi tulizozipata zitatusaidia katika kuongeza ubora wa timu,” alisema
Brandts.
No comments:
Post a Comment