Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini
Kenya, John Michael Haule, wakati Balozi huyo alipofika Osifini kwa Makamu
Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kumuaga leo Mei 27 2015. Picha na OMR
Wednesday, May 27, 2015
Rais Kikwete alipozindua mkutano wa mabalozi wa nje na Tanzania
Mhe. Rais Kikwete akizungumza huku Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakimsikiliza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano wa Nne wa Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi. Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam ukiwa umebeba Kaulimbiu isemayo "Diplomasia ya Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa 2025".Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani).
Tuesday, May 26, 2015
Bayport: Wa mikoani nao wanaweza kukopa viwanja vya Kibaha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha ya Bayaport Financial Services
inayojihusisha na mambo ya mikopo,imesema hata Watanzania wanaoishi mikoani
wanaweza kutumia fursa ya kukopeshwa viwanja katika mradi wa Vikuruti, uliopo
Kibaha, mkoani Pwani. Unaweza kuptata fomu hapa.
Afisa Mipango wa Wilaya ya Kibaha, Obed Katonge, akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya mikopo ya viwanja, uliyofanyika mwishoni mwa wiki, katika hoteli ya Serena.
Bonyeza hapa kupata fomu ya mkopo wa viwanja kutoka Bayport Financial Services
http://www.kopabayport.co.tz/RESERVATION%20FORM.pdf
Kauli hiyo imetolewa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa
taasisi hiyo, Ngula Cheyo, ikiwa ni siku chache baada ya kuzindua huduma ya
mikopo ya viwanja katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, huku
akisisitiza kwamba si lazima mkopaji wa viwanja hivyyo atoke Dar es Salaam au
Kibaha.
Kicheko cha furaha. Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, kulia akifurahia jambo na Meneja Masoko na Mawasiliaano wa Bayport Financial Services, jijini Dar es Salaam.
Cheyo alisema kwamba huduma hiyo ni ya Watanzania wote, ndio
maana wamesambaza fomu za kuomba mkopo wa viwanja katika matawi yao mbalimbali,
bila kusahau wale wanaoweza kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz.
“Nafasi ni chache, maana maombi yetu yanafanyika kwa siku (20),
kuanzia ile Mei 22 hadi Juni 10, huku fomu za maombi zikipatikana katika matawi
yao yote ya Bayport Financial Services, bila kusahau kupitia bank of Africa (BOA),
ambapo malilipo ya awali yakianzia Sh 150,000 na yatakuwa yakilipwa kwa akaunti
yao ya Bayport iliyopo BOA.
Saturday, May 23, 2015
Mwelekeo wa utalii mkoani Kilimanjaro
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu anunua madawati 270
Baadhi
ya madawati 270 yaliyonunuliwa na Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa Shule
za Sekondari zilizopo Jimboni kwake ambapo madawati 100 yalikwisha
chukuliwa kupelekea jumla ya madawati 300 yenye jumla ya Sh. Mil 60 Picha zote na Khamis Mussa.
Bayport Financial Services yaanzisha huduma ya kokopesha viwanja kwa watumishi wa umma na wajasiriamali
Mkurugenzi wa Bayport Financial Services, John Mbaga, pichani, akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya viwanja katika mradi wa Vikuruti, Kibaha, mkoani Pwani. Uzinduzi huo ulifanyika Ijumaa ya Mei 22, katika Hoteli ya Serena na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo viongozi wa serikali. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.
Meneja Biashara wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya viwanja Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Katika huduma hiyo, watumishi wa umma, wajasiriamali na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa wanaweza kujipatia viwanja hivyo kwa matumizi yao wapendayo, hususan ujenzi wa nyumba.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaama
KATIKA hali
isiyokuwa ya kawaida, taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services,
inayojihusisha na mikopo, imeanzisha huduma mpya ya kukopesha viwanja watumishi
wa umma, wafanyakazi wa kampuni za kawaida na wajasiriamali wa aina zote.
Kuanzishwa
kwa huduma hiyo mpya kumetokana na taasisi hiyo kupania kuboresha maisha ya
Watanzania, likiwamo kundi la wajasiriamali ambalo limeendelea kusahauliwa na
kampuni nyingi kupewa mikopo.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, akizungumza katika uzinduzi huo, jijini Dar es Salaam.Meneja Biashara wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya viwanja Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Katika huduma hiyo, watumishi wa umma, wajasiriamali na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa wanaweza kujipatia viwanja hivyo kwa matumizi yao wapendayo, hususan ujenzi wa nyumba.
Akizungumza jana katika uzinduzi uliofanyika katika Hoteli ya Serena, Mkurugenzi Mtendaji wa
Bayport Financial Services, John Mbaga, alisema kuwa ni kusudio lao kutoa fursa ya watumishi
wa umma, wafanyakazi wa kampuni na wajasiriamali kupata nafasi ya kutimiza
ndoto za kumiliki ardhi nchini Tanzania.
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Kibaha, Obed Katonga, kulia akijadiliana jambo na Meneja Uzalishaji wa Bayport Financial Services, Mashaka Mgeta kulia kwake na Mkuu wa Kanda ya Pwani, David Ndiega.
“Huduma yetu
katika mradi wa Vikuruti, Kibaha, mkoani Pwani, fomu zake zinapatikana katika
matawi yote ya Tanzania Bara, ambapo kwenye matawi yetu yote fomu hizo zitakuwapo, huku fomu hizo za kukopeshwa viwanja zikipatikana kwa wiki mbili, kuanzia Mei 22 hadi Juni 10 mwaka huu.
Wednesday, May 20, 2015
MGODI UNAOTEMBEA: Joto la wataka urais CCM, linadhihirisha nguvu ya chama tawala
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
INAHITAJI akili ya kiuwendawazimu kuaminishwa na kuamini kuwa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepoteza mvuto. Kwamba vinavyokubalika ni Chadema,
CUF, NCCR Mageuzi, NLD, TLP na vinginevyo, ambavyo kwa udhaifu wao, wameona
waungane baada ya kukosa dawa ya kukiangusha chama tawala.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ni mmoja wa makada wa CCM, wanaotajwa kuwa na ndoto za kuwania Urais, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, nchini Tanzania.
Si kweli, maana vipo viashiria vingi vinavyoonyesha kuwa
chama hicho kikongwe Tanzania, kipo imara na kinaungwa mkono na watu wengi,
wakiwamo watoto, wazee, vijana na wake kwa waume. Bado wapo watu wanaoamini kuwa mtu mtu anayepitishwa kugombea
katika nafasi yoyote ndani ya CCM, basi huyo ndiye mshindi. Na yapo maeneo
mengi ambayo watu wake hawajui chochote kuhusu vyama vya upinzani, isipokuwa
CCM.
Kuelekea katika Uchaguzi Mkuu, kumekuwa na kauli za hapa na
pale zinazoshiria kuwa baadhi ya Watanzania wenzetu, hususan wanaotoka katika
Chama Tawala wamedhamiria kuchukua fomu za kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu
utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Ingawa wapo wengine wenye nia hiyo ya kutaka urais, ila ndani
ya CCM hali hiyo imezidi. Ndani ya CCM kuna joto na mchuano mkali. Takribani
miaka mitatu sasa tumeshuhudia mivutano ya kila aina.
Wataka urais huo wamekuwa na vikao na safari za kutunisha
makundi yao, bila kusahau kasi ya kuongeza ushawishi kwa vijana wao
wanaoshindana katika mitandao ya kijamii kwa kujiita majina ya kila aina,
kuashiria wapo kwenye msafara huo. Haya yote yanadhihirisha nguvu ya chama tawala. Kila mtu
anaangalia nani ana mvuto zaidi ya mwenzake ndani ya CCM. Kila jina linalotajwa
zaidi mtaani, basi linatokana CCM.
Wapo wanaomtaja Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe, kwamba anayo haiba na uwezo wa juu ya kurithi kiti
cha urais, kitakachoachwa na Rais, Profesa Jakaya Mrisho Kikwete, baadaye mwaka
huu. Wanaoamini Membe anafaa wanafanya kila wawezalo ili jamii
iwaelewe, bila kusahau wanaojiita wapo kwenye safari ya matumaini, nao
wakichagiza Edward Lowassa, Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzulu na Mbunge wa
Monduli arithi mikoba ya JK.
Monday, May 18, 2015
Treni ya Deluxe ya kwenda mkoani Kigoma kuondoka leo saa 2 usiku
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL ) unasikitika kuwataarifu abiria wa treni ya Deluxe ya kwenda Kigoma jana Mei 17, 2015 saa 2 usiku kuwa safari hiyo imeahirishwa hadi leo Jumatatu saa 2 usiku. Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kuahirishwa zinatokana na ajali mbili mfululizo za treni za mizigo.
Ajali ya kwanza ilitokea asubuhi saa 1:30 maeneo ya Stesheni ya Ngeta mkoa wa Pwani na ya pili saa 5 asubuhi maeneo ya Stesheni za Kinguruwila na Morogoro!
Ajali hizo zimehusisha kuanguka kwa mabehewa manne ( Ngeta ) na kuacha njia behewa moja (Kinguruwila )! Treni zote mbili zilikuwa zikielekea bara! Tayari wahandisi na mafundi wa TRL wako katika maeneo ya tukio kwa ajili ya kazi ya kuyaondosha mabehewa yaliopata ajali na pia kukarabati njia ili ifunguliwe haraka na kurejesha mawasiliano ya njia ya reli katika hali ya kawaida.
Kutokana na uzito wa kazi hiyo ya ukarabati njia ndio sababu kuu iliyopelekea safari ya Deluxe iahirishwe hadi kesho usiku! Wakati huo huo taarifa imeongeza kusema kuwa ajali hiyo imeathiri urejeshaji wa vichwa viwili vya treni ya Jiji ambavyo havotoweza kufika Dar kwa wakati na hivyo kesho huduma ya treni ya Jiji haitokuwepo.
Vichwa hivyo vya treni vilikuwa katika ukarabati wa kawaida katika karakana kuu ya TRL Morogoro! Atakayesoma taarifa hii amuarifu nwenzake!
Uongozi wa TRL unasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza!
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Mhandisi Elias Mshana
Dar es Salaam,
Mei 17, 2015
Mhandisi Elias Mshana
Dar es Salaam,
Mei 17, 2015
SIWEZI KUVUMILIA: Timu tatu, Mkoa wa Tanga utakuwa na cha kujivunia?
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
LIGI ya Tanzania Bara itakayoanza baadaye mwaka huu, itakuwa
na raha za aina yake, baada ya mkoa wa Tanga, kupata timu tatu zitakazoshiriki
Ligi hiyo.
Timu hizo ni Coastal Union, Mgambo Shooting ya wilayani
Handeni na ile African Sports, iliyopanda daraja msimu huu, ikijikatia tiketi
ya kushiriki ligi hiyo kubwa nchini Tanzania.
Kushiriki kwa timu hizo, mkoa wa Tanga utakuwa unashika
nafasi ya pili nyuma ya jiji la Dar es Salaam, ambalo lenyewe lina timu ya
Yanga, Simba na Azam FC. Hata hivyo, mkoa wa Tanga unapaswa kujipanga ili kushiriki
kwa timu hizo tatu kuwe na cha kujivunia. Namaanisha kupata ushindani wa aina
yake. Kusiwe na timu ya kufungwa kila mechi. Itakuwa ni aibu kubwa.
Katika kuangalia mfumo uliopo, ni wazi mkoa wa Tanga utakuwa
umepanda kiasi fulani katika sekta ya mpira wa miguu, jambo linalohitaji
ushirikiano pia kutoka kwa wadau wa michezo, wakazi wa Tanga na Watanzania kwa
ujumla. Kinyume cha hapo siwezi kuvumilia. Hii ni kwa sababu
kusipokuwa na mipango, timu hizo zitaendelea kusua sua. Ni Mungu tu, ila ni
wazi Mgambo ilibaki kidogo ishuke daraja.
Kwa sababu imenusurika, kila mdau wa michezo wa mkoa wa Tanga
ahakikishe anafanya bidii kuliweka soka lao katika kilele cha mafanikio.
Kushiriki kwa Ligi ya Tanzania Bara, ni wazi Mkoa wa Tanga utakuwa na sehemu ya
kujitangaza. Pia unaweza kuwa na nafasi nzuri kibiashara kutokana na
wageni watakaoingia na kutoka kufuata timu zao kutoka katika mikoa mbalimbali,
ikiwamo Dar es Salaam kunapopatikana timu kubwa na kongwe, kama vile Yanga,
Simba na Azam.
Kwa timu kama African Sports na Mgambo Shooting zenyewe
zinapaswa kufanya bidii ili kuhakikisha kwamba zinaonyesha soka la uhakika, ili
zisiwe katika hatari ya kushuka daraja. Mkoa kuwa na timu tatu zinazocheza Ligi
Kuu si jambo dogo. Hata hivyo kunaweza kusiwe na tija kama hakutakuwa na juhudi,
mipango na kujituma kusaka ushindi utakaowaweka juu kisoka na kibiashara pia.
Kinyume cha hapo siwezi kuvumilia, maana hakutakuwa na jipya licha ya kuwa na
timu tatu zinazoshiriki Ligi Kuu katika Mkoa mmoja wa Tanga.
Tuonane wiki ijayo.
+255 7120539
Sunday, May 17, 2015
Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM mjini Dodoma ni balaa
Muonekano wa ndani wa ukumbi mpya wa mikutano uliojengwa na CCM mjini Dodoma ambao uko katika hatua za mwisho kukamilika kabla ya kuanza kutumika.Ukumbi huu upo karibu na jengo la Benki Kuu, njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha Dodoma - UDOM.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Dodoma unaojengwa na CCM.
|
Mbunge wa Kigamboni Mh Ndugulile afanya mkutano wa hadhara Tua Moyo jijini Dar es Salaam
Mwalimu mstaafu wa Sekondari na Mjumbe mwelimishaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa Wzazi Tua Moyo Ali Ahmad kwa jina maarufu mpemba wa Asili, akisoma shairi wakati wa Mkutano wa Hadhara ambapo Mgeni Rasmi ni Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile. Picha zote na Khamis Mussa.
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile akisalimia wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara ulio fanyika Dar es Salam.
Dk. Faustine Ndugulile akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya kigamboni na Katibu Kata wa chama hicho kabla ya kuanza Mkutano huo.
Saturday, May 16, 2015
MKUTANO MKUU:Wanahisa wa CRDB wanavyopigania kuiweka juu benki yao
*Wafanya
Mkutano Mkuu wa 20 AICC Arusha
*Dkt Kimei
aanika mikakati ya kuipaisha CRDB
Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Arusha
NI kama vile uhai na mafanikio ya benki ya CRDB umejulikana
upya, baada ya menejimenti, Bodi ya Wakurugenzi na Wanahisa kukubaliana kwenye
Mkutano wao Mkuu wa 20 wa Wana Hisa uliofanyika Mei 9, mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB benki, Dkt Charles Kimei, akizungumza jambo katika Mkutano wa wanahisa wa benki hiyo jijini Arusha.
Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Simba, kwenye Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano cha AICC, huku ukifurika wana Hisa wengi kutoka
mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Mtangazaji mkongwe nchini Tanzania, Salimu Mbonde, akisikiliza kwa makini mkutano wa hisa wa benki ya CRDB, jijini Arusha.
Katika mkutano huo ulioanza saa 3 asubuhi, mengi
yalijadiliwa, ikiwamo ripoti ya wakaguzi na mwelekeo wa benki hiyo katika
kufungua matawi, bila kusahau tawi lao lililokuwa nchini Burundi.
Katika mazungumzo yaliyofanyika jijini Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dkt Charles Kimei, anasema kwamba
kufanyika kwa amani na mafanikio mkutano huo, ni kama vile benki yao imezaliwa
upya.
Anasema biashara yoyote inayohusiana na wana hisa, kunahitaji
mipango ya kukubaliana kwa pande zote, jambo linalowafanya menejimenti, bodi na
wanahisa kuona ipo dhamira ya dhati ya kuhakikisha kwamba bendi yao inapiga
hatua.
“Wanahisa ni watu muhimu na ndio maana tumekuwa tukifanya
mkutano wa mwaka kwa ajili ya kupitisha ripoti, kutaja vipaumbele na kuangalia
jambo gani la kufanya katika kuhakikisha kwamba benki yetu inakuwa bora zaidi.
CRDB ni kati ya benki bora nchini ambayo tumefanikiwa pia
kuwa na tawi letu nchini Burundi ambapo hata hivyo kumekuwa na hali ya sintofahamu
katika mambo ya kisiasa,” alisema.
Katika mkutano huo, baadhi ya wanahisa walitoa ushauri wao
juu ya mwenendo bora wa benki yao, ikiwamo taratibu za ufunguaji wa matawi
katika mikoa mbalimbali.
Awali, mkutano huo ulikuwa na dondoo kama vile kufungua
mkutano, Kuchagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu, Kuridhia
ajenda ya mkutano, kuthibitisha kumbukumbu za Mkutano Mkuu uliopita, kujadili
yatokanayo na kumbukumbu za Mkutano Mkuu wa 19, kujadili na kupokea taarifa ya
Bodi ya Wakurugenzi na taarifa hesabu zilizokaguliwa za mwaka 2014.
Friday, May 15, 2015
Serikali yasema elimu bora ni ile inayomuelekeza mtu kujitegemea
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ya kukutana na wadau wa elimu walioshiriki mkutano wa kutathmini sekta ya Eimu nchini kwa mwaka 2014 uliofanyika katika kumbi za mikutano Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).(Picha zote na Zainul Mzige.
Na Modewjiblog team
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini amesema elimu ya sasa inaelekezwa zaidi katika kumwezesha mtu kujitegemea.
Kauli hiyo ameitoa katika mahojiano maalum kuhusu maendeleo na changamoto kwenye sekta ya elimu nchini katika wiki ya maadhimisho ya elimu inayofikia tamati leo mjini Dodoma.
Alisema katika mahojiano hayo kwamba mfumo sasa unawaondoa watu kwenye ajira ya serikali na kutokana na hilo uimarishaji wa elimu ndio kitu cha msingi kabisa.
Alisema katika maadhimisho ya elimu watu wanajifunza usimamizi kama msingi mkubwa wa maendeleo ya elimu nchini.
James Mbatia aalikwa mahafari ya kidato cha sita Maua Seminary
Tuesday, May 12, 2015
Waandishi wa habari waaswa kuandika habari sahihi kwenye gesi na mafuta
Mwenyekiti wa Mpango wa Uhamasishaji wa Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI), Jaji Mstaafu, Mark Bomani akifungua warsha ya siku moja kwa wadau na wandishi wa habari za biashara, mkutano uliofanyika Ledger Plaza Bahari Beach Hotel jijini Dar es Salaam, Mei 7, mwaka huu.
Na Andrew Chale
Mwenyekiti wa Mpango wa Uhamasishaji Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi Asilia na Mafuta (TEITI) Jaji Mark Boman amewataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi zenye lengo la kuielimisha jamii hasa pindi wanaporipoti habari za sekta ya madini hapa nchini.
Akizungumza wakati wa semina ya waandishi wa habari za biashara na uchumi ya siku moja iliyofanyika hivi karibuni Ledger Plaza Bahari Beach Hotel, jijini Dar es Salaam, Jaji Bomani alisema taarifa sahihi hasa za masuala ya uchumi zinahitajika kwani zikitolewa tofauti zinaweza kusababisha mkanganyiko kwa wananchi.
Alisema taasisi hiyo ilianzishwa kuwa lengo la kufuatilia sekta ya madini kwani hapo awali ilionekana kutowanufaisha wananchi.“Awali kuliwa na mkanganyiko wa kwamba sekta ya madini haiwanufaishi wazawa hivyo Serikali ilichukua hatua na kuunda kamati ya kushughulikia tatizo hilo kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta hiyo ya madini,”alisema.
Rais Kikwete amteua Kamishna mpya wa Polisi, Diwani Athumani Msuya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi
(CP) Diwani Athumani Msuya, kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya
Jinai (Director of Criminal Investigation).
Kabla ya uteuzi huu CP Msuya alikuwa Kaimu Kamishna wa kamisheni ya Intelijensia ya Jinai. CP Msuya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Robert S. Manumba ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.
Kabla ya uteuzi huu CP Msuya alikuwa Kaimu Kamishna wa kamisheni ya Intelijensia ya Jinai. CP Msuya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Robert S. Manumba ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.
Rais Kikwete pia amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino
Mlowola kuongoza Idara ya Intelijensia ya Jinai, kujaza nafasi
inayoachwa na Kamishna Msuya.
Kabla ya Uteuzi huu, DCP Mlowola alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.
Uteuzi huu umeanza tarehe 3 Mei, 2015.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Mei, 2015
Kabla ya Uteuzi huu, DCP Mlowola alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.
Uteuzi huu umeanza tarehe 3 Mei, 2015.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Mei, 2015
Sunday, May 10, 2015
Uhondo wa Lady Jay Dee
Finally Lady Jaydee's Give Me Love music video is out. The video was shot and directed by Nicky Campos on location in Johannesburg, South Africa. The Song was produced by Uhuru and features Mazet & DJ Maphorisa.This is the follow up single after the mega hit 'Forever ft Dabo' which has earned Jide multiple nominations in the upcoming Kili Music Awards, including 'Best Collaboration' and 'Best Female'. Other nods are from the prior releases 'Nasimama' and 'Historia' which both are competing for the 'Best Zouk Song' category.
For more info please follow Lady Jaydee:
Twitter: @jidejaydee
Instagram: @jidejaydee
Facebook: @ladyjaydee
Enjoy the video below
Ratiba ya vikao vya ndani vya CCM yatolewa, kuanza Mei 18
Chama Cha Mapinduzi kupitia Katibu wake wa Uenezi Ndugu Nape Nnauye
kimetangaza ratiba za Vikao vya juu vya Chama hicho kuanzia tarehe 18
mpaka 23 Mjini Dodoma.
Tarehe 18 mpaka 19 Mei Kikao Cha Sekretarieti ya CCM chini ya Katibu Mkuu Ndugu Kinana
Tarehe 20 Mei kutakuwa na Kikao cha Kamati Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti Ndg Jakaya Kikwete.
Tarehe 18 mpaka 19 Mei Kikao Cha Sekretarieti ya CCM chini ya Katibu Mkuu Ndugu Kinana
Tarehe 20 Mei kutakuwa na Kikao cha Kamati Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti Ndg Jakaya Kikwete.
Tarehe 21 mpaka 22 kutakuwa na Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Ndg Jakaya Kikwete.
Vikao hivyo ambavyo vitafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Makao Makuu
Dodoma maarufu kama "whitehouse" vinategemea kujadili ajenda zifuatazo.
1. Kuwasilisha na kujadili ripoti ya hali ya siasa nchini.
2. Ratiba ya mchakato wa uteuzi wa wagombea wa nafasi za udiwani, uwakilishi, ubunge, urais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
3. Kupitia Rasimu ya Kwanza ya maboresho ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015/2020.
4. Mapendekezo ya uboreshaji wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM.
5. Namna ya Ushiriki na Mkakati wa Ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu.
Vikao hivyo ambavyo vitafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Makao Makuu
Dodoma maarufu kama "whitehouse" vinategemea kujadili ajenda zifuatazo.
1. Kuwasilisha na kujadili ripoti ya hali ya siasa nchini.
2. Ratiba ya mchakato wa uteuzi wa wagombea wa nafasi za udiwani, uwakilishi, ubunge, urais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
3. Kupitia Rasimu ya Kwanza ya maboresho ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015/2020.
4. Mapendekezo ya uboreshaji wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM.
5. Namna ya Ushiriki na Mkakati wa Ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu.
Saturday, May 09, 2015
UTT watembelea China kuangalia uwezekezaji na maanufaa yake
Bodi ya UTT-PID ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. E Mlaki pamoja na Menejimenti wakiwa na wenyeji wao katika jiji la Chengdu ambapo walifanya ziara katika maeneo tofauti ya uwekezaji na manufaa wanayopata wananchi wa jiji hilo. Ziara hiyo ya siku Tano katika Miji tofauti inatarajia kukamilika Tarehe kumi kabla ya kurejea nyumbani.
Na Mwandishi Maalum
Bodi ya Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyo chini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID), pamoja na Menejimenti yake ipo nchini China katika ziara maalum ya Mafunzo na kujenga uzoefu ya siku tano ikiwa na lengo la kuimmalisha utendaji kaziw wa taasisi hiyo.
Katika ziara hiyo, Bodi ya UTT-PID, ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. E Mlaki pamoja na Menejimenti wapo katika miji mbalimbali na kutembelea maeneo tofauti ya uwekezaji ilikushuhudia manufaa wanayopata wananchi wa maeneo hayo.
Kazi za UTT-PID ni pamoja na Utoaji huduma za ushahuri katika maeneo ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.
World Lung Foundation yazindua mradi wa elimu kwa mtandao kusaidia uokoaji wa akina mama na watoto
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif
Rashid (wapili kulia), akiwa na baadhi ya watendaji wa Shirika la World
Lung Foundation (WLF) la hapa nchini wakishudia uzinduzi wa mradi wa
elimu kwa mtandao unaosaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao
unaendeshwa na kusimamiwa na shirika hilo katika vituo vya Afya 13.
TAASISI ya World Lung Foundation (WLF) Tanzania
imezindua mradi wa elimu kwa njia ya mtandao katika hatua mpya ya
kusaidia kuboresha ubora wa huduma za wajawazito pamoja na akina mama na
watoto wao. Mradi huu wa Mawasiliano umefadhiliwa na Shirika la
Maendeleo la Sweden (Swedish International Development Cooperation,
(Sida)) na Shirika la Merck For Mothers. Mradi huu upo katika vituo vya
afya 13 vinavyo fadhiliwa na WLF katika mikoa ya Kigoma, Pwani na
Morogoro.
Mfumo
huu wa WLF Tanzania wa elimu kupitia mtandao (e-learning) umeundwa ili
kuboresha ujuzi wa wafanyakazi wa vituo vya afya na kuongeza wao uwezo
wa kufanya maamuzi sahihi katika kliniki zitoazo huduma za afya. Mfumo
huuutawasaidia kufanya maamuzi ya kitaalam kuhusu usimamizi wa dalili
hatarishi za ujauzito, huduma wakati wa kujifungua na baada ya
kujifungua kwa ajili ya akina mama na watoto wao.Mafunzo haya
yatawawezesha watoa huduma ya afya kuwasiliana na kupata taarifa muhimu
za kuongeza ujuzi, kusoma Makala za jarida za kitaalam, kuona filamu
zinazoelimisha, picha na masomo ya kujifunzia. Wafanyakazi wa afya pia
wanaweza kutumia jumuishi ya vikao vya mitandao na kubadilishana ujuzi
na taarifa kuhusu changamoto na mafanikio yao pamoja na wenzao na
wataalam waandamizi katika vituo vya afya 13.
Mamilioni ya Kopa Bayport yazidi kupata wenyewe
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Ngula Cheyo, katikati akizungumza jambo wakati wa droo ya pili ya Kopa Bayport kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, ambapo jumla ya washindi watatu kila mwezi wanapatikana na kila mmoja kujishindia jumla ya Sh Milioni moja. Kulia ni Afisa wa Huduma kwa Wateja wa taasisi hiyo, Gladys John, huku kushoto akiwa ni bwana Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania. Picha zote na Mpiga Picha wetu.
Akizungumza katika droo hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema shindano lao limepokewa vizuri na wateja wao, waliopata urahisi wa upatikanaji wa huduma za mikopo kutoka kwenye taasisi hiyo.
Tunatafuta washindi wa kujinyakulia Sh Milioni moja kila mmoja kwa washindi watatu kutoka Bayport Financial Services. Ndivyo wanavyoonekana kusema katika droo hiyo ambapo washindi kutoka Njombe, Dar es Salaam na Bukoba wamechanua.
Alisema awali wateja walilazimika kusafiri kuelekea kwenye tawi lao, lakini kuanzishwa kwa tovuti hiyo, kumetoa urahisi wa ukopaji kwa kiasi kikubwa mno, huku kila mmoja akiwa na uwezo wa kushinda endapo ataamua kutumia huduma hiyo.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHINDANO la Kopa Bayport kwa njia ya mtandao linaloendeshwa na taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, limezidi kuchanja mbuga, baada ya wateja watatu wa mwezi Mei kuibuka na Sh Milioni moja kwa kila mmoja, huku mikoa ya Bukoba, Njombe na Dar es Salaam ikichanua katika droo iliyochezeshwa jana, jijini Dar es Salaam.
Wateja hao walioshinda katika shindano hilo ni Tryphone Mashamba mkoani (Njombe), Kisa Mboya (Dar es Salaam) na Oscar Gadawu (Bukoba) ambao wote kwa pamoja wameibuka na Sh Milioni moja baada ya kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, ikiwa ni huduma nzuri kutoka kwenye taasisi hiyo ya Bayport Financial Services.
Afisa wa Huduma kwa Wateja wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Gladys John katikati akichagua koponi ya mmoja wa washindi wa shindano la Kopa Bayport linaloendelea ambapo washindi watatu wamepatikana na kila mmoja kupata bahati ya kujinyakulia Sh Milioni moja kila mmoja baada ya kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz. Kulia ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, wakati kushoto ni Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.SHINDANO la Kopa Bayport kwa njia ya mtandao linaloendeshwa na taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, limezidi kuchanja mbuga, baada ya wateja watatu wa mwezi Mei kuibuka na Sh Milioni moja kwa kila mmoja, huku mikoa ya Bukoba, Njombe na Dar es Salaam ikichanua katika droo iliyochezeshwa jana, jijini Dar es Salaam.
Wateja hao walioshinda katika shindano hilo ni Tryphone Mashamba mkoani (Njombe), Kisa Mboya (Dar es Salaam) na Oscar Gadawu (Bukoba) ambao wote kwa pamoja wameibuka na Sh Milioni moja baada ya kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, ikiwa ni huduma nzuri kutoka kwenye taasisi hiyo ya Bayport Financial Services.
Akizungumza katika droo hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema shindano lao limepokewa vizuri na wateja wao, waliopata urahisi wa upatikanaji wa huduma za mikopo kutoka kwenye taasisi hiyo.
Tunatafuta washindi wa kujinyakulia Sh Milioni moja kila mmoja kwa washindi watatu kutoka Bayport Financial Services. Ndivyo wanavyoonekana kusema katika droo hiyo ambapo washindi kutoka Njombe, Dar es Salaam na Bukoba wamechanua.
Alisema awali wateja walilazimika kusafiri kuelekea kwenye tawi lao, lakini kuanzishwa kwa tovuti hiyo, kumetoa urahisi wa ukopaji kwa kiasi kikubwa mno, huku kila mmoja akiwa na uwezo wa kushinda endapo ataamua kutumia huduma hiyo.
Thursday, May 07, 2015
Francis Cheka kukwaana na Mthailand jijini Dar es Salaam Mei 30
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BONDIA Fransic Cheka atapanda ulingoni kwa mara ya kwanza kabisaa baada ya kutoka jera ambapo atacheza na Kiatchai Singwancha kutoka Thailand mpambano uho wa raundi kumi utafanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es salaam,
Akizungumza matayalisho ya mpambano huo, promota Kaike Siraju alisema kuwa amejipanga vizuri kwani kila kitu kinaenda vizuri kwa ivi sasa ambapo mabondia wa utangulizi wote wanatarajia kusainishwa wiki hii mpambano uho utakaosimamiwa na chama cha ngumi za kulipipwa nchini P.ST chini ya rais wake Emanuel Mlundwawamesema kuwa wao wako tayali kwa mpambano uho na bondia wa Thailand ataingia nchini siku tatu kabla ya mpambano uho ambao uatavuta isia za wapenzi wengi wa mchezo wa ndondi nchini siku hiyo Vicent Mbilinyi 'Sugu' atavaana na Keis Amal
BONDIA Fransic Cheka atapanda ulingoni kwa mara ya kwanza kabisaa baada ya kutoka jera ambapo atacheza na Kiatchai Singwancha kutoka Thailand mpambano uho wa raundi kumi utafanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es salaam,
Akizungumza matayalisho ya mpambano huo, promota Kaike Siraju alisema kuwa amejipanga vizuri kwani kila kitu kinaenda vizuri kwa ivi sasa ambapo mabondia wa utangulizi wote wanatarajia kusainishwa wiki hii mpambano uho utakaosimamiwa na chama cha ngumi za kulipipwa nchini P.ST chini ya rais wake Emanuel Mlundwawamesema kuwa wao wako tayali kwa mpambano uho na bondia wa Thailand ataingia nchini siku tatu kabla ya mpambano uho ambao uatavuta isia za wapenzi wengi wa mchezo wa ndondi nchini siku hiyo Vicent Mbilinyi 'Sugu' atavaana na Keis Amal
Katika
mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo
wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali
kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez, Mike Tyson, Mohamed Ali, Ferex Trinidad, Miguel Cotto na wengine wengi pia
kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila
'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa
kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha
Aliyekuwa Mkurugenzi MUWSA, Cyprian Luhemeja aaga kwa ajili ya kuanza kazi rasmi DAWASC
Aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshu (MUWSA) mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na wafanyakazi wa mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa kauli ya kuwaaga baada ya kuteuliwa kushika nafasi ya Mtendaji mkuu DAWASCO. |
Kauli ya Mhandisi Luhemeja ya kuwaaga
wafanyakazi hao ilionekana kama mwiba na kuzua simanzi kuu kwa
watumishi hao waliofanya kazi na mkurugenzi huyo kwa kipindi cha mwaka
mmoja na miezi 10. |
Wednesday, May 06, 2015
Yanga kukabidhiwa ubingwa wake leo jijini Dar es Salaam
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
LIGI Kuu
ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea leo kwa mchezo mmoja
utakaopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,
wenyeji timu ya Azam FC watawakaribisha Mabingwa wapya wa ligi hiyo
msimu huu timu ya Young Africans.
Mechi
hiyo no. 141 itachezeshwa na mwamuzi wa kati Jacob Adongo kutoka Mara,
akisaidiwa na washika vibendera Frednand Chacha (Mwanza), Hellen Mduma
(Dsm), huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Hussein Kalindo (Dsm) na Kamisaa
wa mchezo huo ni Damian Mabena kutoka Tanga.
Katika
mchezo huo timu ya Young Africans itakabidhiwa Kombe lake la Ubingwa wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2014/2015, na mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr
Fennela Mkangara.
Mchezo
huo wa kesho unatarajiwa kuanza majira ya saa 11 kamili jioni, kwa saa
za Afrika Mashariki na kati ili kutoa fursa kwa wadau, wapenzi na
mashabiki wa mpira wa miguu nchini kujitokeza kushudia mchezo huo pamoja
na shamrashamra za kukabidhiwa kikombe.
Young
Africans watakabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu
na mgeni rasmi, huku wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi
ya Vodacom wakimkabidhi zawadi mchezaji bora wa mwezi Aprili Mrisho
Ngasa na fedha taslimu sh. millioni moja.
Friday, May 01, 2015
Kambi Mbwana amparua Dkt Kigoda kuhusu kitabu chake
Na Mwandishi Wetu, Handeni
MWANDISHI wa kitabu cha Dira na Tumaini Jipya Handeni, Kambi Mbwana, amemjia juu mbunge wa Handeni, mkoani Tanga na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda, kwa madai kuwa anajaribu kumziba mdomo ili wananchi waendelee kuwa vipofu wasiweze kuwawajibisha wananasiasa mizigo wasiokuwa na faida kwa wilaya hiyo kongwe yenye rasilimali lukuki.
Mbwana aliyasema hayo jana mjini hapa, ikiwa ni siku chache baada ya Dkt Kigoda kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika Handeni Mjini katikati ya wiki iliyopita kuwataka wananchi wapuuze kitabu hicho, jambo lililoibua mvutano kwa wasomaji wa kitabu hicho na wanaoamini maneno ya Kigoda, ambaye ni mbunge wa jimbo la Handeni kwa miaka 20 sasa.
Akizungumzia hatua hiyo, Mbwana alisema kitabu chake hakijaandikwa kwa lengo la kumuonea wala kudhalilisha upande mmoja, ingawa alikiri kuwa mtu asiyekuwa na malengo ya kuwakomboa wananchi wake, kamwe hawezi kupata nafasi ya kukisifia kitabu hicho pekee kinachotoa dira na tumaini jipya kwa wananchi wa wilaya hiyo kongwe nchini Tanzania.
“Kwanza namshangaa Dkt Kigoda kwa sababu amedhihirisha upeo wake wa kufikiria umekuwa mdogo ndio maana anajaribu kuingilia kitabu hiki kinachoelimisha jamii sit u watambue changamoto zao, bali pia wajue namna bora ya kujikwamua kiuchumi.
Hii inakera na kuhuzunisha maana kama watu kama akina Kigoda wanaoaminiwa ni wasomi wazuri katika nchi hii wanashindwa kushirikiana na jamii yao ili kuwakwamua wananchi wao, ni kuonyesha kuwa uwezo wao kiakili na malengo ya kuwatumikia wananchi wao yamefikia ukingoni,” alisema Mbwana.
Akielezea kitabu hicho, Mbwana alisema Dira na Tumaini Jipya Handeni kimegusia mambo ya migogoro ya ardhi, shida ya maji, ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya na mengineyo yanayoendelea kuwaumiza wananchi wa Handeni na Watanzania kwa ujumla, huku wakikipokea kitabu hicho kama mkombozi wao kutokana na aina ya kilichoandikwa ndani ya kitabu katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.
Kwa mujibu wa Mbwana, kitabu hicho kinapatikana sehemu mbalimbali za mkoa wa Tanga, kama vile Handeni, Korogwe, Tanga Mjini na baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam, huku kikionekana kupokewa kwa shangwe na wananchi waliopenda hoja na suluhisho zake zilivyoongelewa kwa kina ndani ya kitabu hicho cha aina yake.
MWANDISHI wa kitabu cha Dira na Tumaini Jipya Handeni, Kambi Mbwana, amemjia juu mbunge wa Handeni, mkoani Tanga na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda, kwa madai kuwa anajaribu kumziba mdomo ili wananchi waendelee kuwa vipofu wasiweze kuwawajibisha wananasiasa mizigo wasiokuwa na faida kwa wilaya hiyo kongwe yenye rasilimali lukuki.
Mbwana aliyasema hayo jana mjini hapa, ikiwa ni siku chache baada ya Dkt Kigoda kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika Handeni Mjini katikati ya wiki iliyopita kuwataka wananchi wapuuze kitabu hicho, jambo lililoibua mvutano kwa wasomaji wa kitabu hicho na wanaoamini maneno ya Kigoda, ambaye ni mbunge wa jimbo la Handeni kwa miaka 20 sasa.
Akizungumzia hatua hiyo, Mbwana alisema kitabu chake hakijaandikwa kwa lengo la kumuonea wala kudhalilisha upande mmoja, ingawa alikiri kuwa mtu asiyekuwa na malengo ya kuwakomboa wananchi wake, kamwe hawezi kupata nafasi ya kukisifia kitabu hicho pekee kinachotoa dira na tumaini jipya kwa wananchi wa wilaya hiyo kongwe nchini Tanzania.
“Kwanza namshangaa Dkt Kigoda kwa sababu amedhihirisha upeo wake wa kufikiria umekuwa mdogo ndio maana anajaribu kuingilia kitabu hiki kinachoelimisha jamii sit u watambue changamoto zao, bali pia wajue namna bora ya kujikwamua kiuchumi.
Hii inakera na kuhuzunisha maana kama watu kama akina Kigoda wanaoaminiwa ni wasomi wazuri katika nchi hii wanashindwa kushirikiana na jamii yao ili kuwakwamua wananchi wao, ni kuonyesha kuwa uwezo wao kiakili na malengo ya kuwatumikia wananchi wao yamefikia ukingoni,” alisema Mbwana.
Akielezea kitabu hicho, Mbwana alisema Dira na Tumaini Jipya Handeni kimegusia mambo ya migogoro ya ardhi, shida ya maji, ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya na mengineyo yanayoendelea kuwaumiza wananchi wa Handeni na Watanzania kwa ujumla, huku wakikipokea kitabu hicho kama mkombozi wao kutokana na aina ya kilichoandikwa ndani ya kitabu katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.
Kwa mujibu wa Mbwana, kitabu hicho kinapatikana sehemu mbalimbali za mkoa wa Tanga, kama vile Handeni, Korogwe, Tanga Mjini na baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam, huku kikionekana kupokewa kwa shangwe na wananchi waliopenda hoja na suluhisho zake zilivyoongelewa kwa kina ndani ya kitabu hicho cha aina yake.
Subscribe to:
Posts (Atom)