Mkuu wa Wilaya Kilindi, Selemani Liwowa
Na Rahimu Kambi, Kilindi
Mganga Mkuu wa Zahanati ya Kata ya Saunyi, Tarafa ya Mgela,
wilayani Kilindi mkoani Tanga, Rashid Mhande, anasakwa na porisi baada ya
kufumwa akiiba dawa zenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni tano.
Tukio hilo lilitokea juzi, baada ya Mhande kufumwa akiiba
dawa kwa kutumia toroli la Zahanati hiyo, kabla ya kuzihamishia kwenye pikipiki
yake kwa ajili ya kuzipeleka anakojua yeye.
Akizungumza jana usiku, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, mkoani
Tanga, Selemani Liwowa, alisema kwamba hadi sasa mganga huyo hajulikani alipo,
huku akiagiza asakwe popote alipo ili afikishwe kwenye vyombo vya dola.
Alisema hospitali hiyo imekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa
wananchi wakisema mara kadhaa wanaambiwa hakuna dawa, jambo linalowapa wasiwasi
mkubwa.
“Tunashukuru kubainika kwa mganga huyo aliyekuwa anaiba dawa
katika zahanati ya Saunyi, jambo ambalo hakika limetusikitisha mno kwa
watumishi kama hawa.
“Baada ya kubainika, baadhi ya wananchi walianza kumpiga,
hivyo kufanikiwa kukimbia, ambapo alipofika polisi alisingizia amepigwa na
wafugaji, hivyo kupewa matibabu Makao Makuu ya wilaya, hata hivyo alipoona
atagundulika janja yake kutoka kwa wananchi na serikali, aliamua kutoroka
kusipojulikana," alisema Liwowa.
Kwa mujibu wa Liwowa, ameagiza porisi wamsake mhalifu huyo
ili sheria zichukuwe mkondo wake kwa watumishi wanaohujumu Taifa na kuiletea
aibu serikali kwa vitendo vyao visivyokuwa vya kiungwana.
No comments:
Post a Comment