Mkuu wa Mkoa Tanga, Chiku Gallawa
Na Rahimu Kambi, Kilindi
MKUU wa Mkoa Tanga, Chiku
Gallawa, amewataka Watanzania na wananchi wa wilayani Kilindi kuhakikisha kuwa
wanatunza mazingira ili wapate maisha bora, hasa kwa kupitia kilimo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa
Mkuu wa Mkoa aliyasema hayo
alipokuwa anazungumza na wananchi wa Lumutio, katika ziara yake ya siku nne
inayomalizika leo wilayani hapa, kabla ya kuelekea jijini Tanga kuendelea na
kazi zake nyingine za ujenzi wa Taifa.
Akizungumza zaidi, Chiku
Gallawa alisema kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakifanya shughuli za ukataji wa
mkaa bila kufuata sheria wala maagizo ya serikali yanayokataza kazi hizo.
Alisema watu hao wamesababisha
hatari kubwa ya ukame na kuleta jangwa na ukosefu wa mvua katika baadhi ya
maeneo kutokana na matatizo ya watu wachache, jambo ambalo haliwezi kufumbiwa macho.
“Hii haiwezi kuchekewa wala
kufumbiwa macho na serikali, hivyo ni jambo la msingi kwa kila mwananchi wa
wilayani Kilindi na Tanzania kwa ujumla kuhakikisha kuwa inatunza mazingira.
“Tukitunza mazingira, kuhifadhi
misitu na miti yetu inayovamiwa kwa kasi na watu kwa ajili ya ukataji wa mkaa,
hakutakuwa na jangwa wala badiliko lolote, hivyo kuwa tunu kwetu,” alisema.
Ziara ya Mkuu huyo wa Mkoa Tanga,
ilisimamiwa kwa umakini na mwenyeji wake, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilindi,
Selemani Liwowa na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwamo jingo la
wazazi la zahanati wilayani humo.
No comments:
Post a Comment