Yusuph Shabani (Yusuphed Mhandeni)
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
CHAMA
chochote chenye dira na mfumo mzuri, lazima kianzie na chini kabisa, hasa kwa
viongozi wa matawi, ambao ndio wanaosababisha uwepo wa viongozi wa juu, akiwamo
Mwenyekiti wa Taifa.
Yusuph Shabani Mhandeni
Kwa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), mfumo huo ni kawaida, jambo ambalo mara kadhaa limekuwa na
tija kwao, hasa kwa kuona viongozi wao na wote wanapigania ushindi wao.
Kwasababu
hiyo, tumeshuhudia joto kali kutoka kwenye chaguzi za ndani za CCM
zilizofanyika mwaka jana, ambapo viongozi mbalimbali walishaguliwa.
Ni
viongozi mahiri na wenye kutegemewa kuleta tumaini jipya kwa wanachama wao,
katika kipindi cha kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, bila kusahau
ule wa mwaka 2015, ukishirikisha vyama vya siasa kutafutwa Rais, wabunge na
madiwani.
Miongoni
mwa viongozi waliochaguliwa katika chaguzi za ndani za CCM mwaka jana, ni
Yusuph Shaban Mhandeni. Mwanachama huyu ameshinda kiti cha Katibu wa Uchumi na
Fedha wa Kata ya Makumbusho.
Katika
mazungumzo na Handeni Kwetu yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Yusuph
Shaban Mhandeni, anayejulikana zaidi kwa jina la (Yusuphed Mhandeni), anasema
kuchaguliwa katika nafasi hiyo ni sehemu ya kuhakikisha kuwa anakisaidia chama
chao ili kiendelee kushika dola kwa kusimamia vyema miradi yako.
Anasema
hali hiyo inasababishwa na imani kubwa kwa Watanzania juu ya CCM, hivyo ni budi
viongozi wote kuanzia ngazi ya matawi hadi Taifa kufanya kazi bila kuchoka kwa
ajili ya kuwaletea maendeleo Watanzania wenye kukithamini chama chao.
Mwanachama
huyo anasema kwamba CCM imekuwa ikitesa katika Taifa hili kutokana na mipango
yao imara, hasa kwa kuhakikisha kuwa inakuwa na viongozi makini sehemu zote.
Anasema
hali hiyo imesababisha chaguzi za CCM Tanzania nzima kugusa hisia za watu
wengi, jambo ambalo linaleta upinzani wa aina yake kwa wanachama wote wenye
hamu ya kuteuliwa na kupewa nafasi mbalimbali za uongozi za chama chao.
“Nashukuru
kwa kupata nafasi ya Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Makumbusho,
nikimuangusha mpinzani wangu wa karibu, Mary Mtawali, aliyekuwa anatetea nafasi
yake, hivyo ninachofanya ni kuhakikisha kuwa tunasimamia miradi ya chama chetu
pamoja na kutangaza ilani kwa watu wote.
“Kushika
nafasi hii sijabahatisha, maana nina uwezo huo na wanachama wenzangu wana imani
na mimi, hivyo jukumu langu kubwa ni kuhakikisha watu wanakipenda zaidi chama
chetu ili kuwapa nafasi viongozi wafanye kazi kwa ajili ya Watanzania wote,”
alisema.
Mbali na
kuwa Katibu wa Uchumi na Fedha, pia mwanachama huyo ni Kamanda wa Vijana Tawi
la Mwanyamala, nafasi ambazo zote kwa pamoja anazifanya kwa uaminifu akiwa na
lengo moja la kuwaunganisha wanachama wote na Watanzania kwa ujumla.
Yusuphed
anasema umuhimu wake ndani ya chama utatokana na kusimamia vyema utendaji kazi
wao, hasa kwa jumuiya tatu ambazo ni Jumuita ya Wazazi, Jumuiya ya Wanawake na
ile ya Vijana, UVCCM ambayo imekuwa na pilika pilika za hapa pale.
Mwana CCM
huyo anasema jumuiya ndio nguzo imara za chama, hivyo kwa kufanya hivyo, mambo
yao yataendelea kuwa mazuri na kupewa ridhaa na Watanzania kuongoza Tanzania.
Kitu
kingine kinachowapa kiburi na kuamini kuwa Watanzania wanakipenda chama chao ni
kutokana na viongozi wa chama na serikali kufanya kazi bila kuchoka, huku
wakitetea ilani na sera za CCM katika Uchaguzi wa mwaka 2010.
Anasema
chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni mwenyekiti wao Taifa,
amesimamia vyema watendaji na mawaziri ili wafanikishe maisha bora kwa
Watanzania, ingawa baadhi yao wanabeza kuwa nchi haina maendeleo.
“Sisi CCM
na Watanzania wote tunashangaa mtu anapopita katika barabara nzuri kutoka Dar
es Salaam hadi Mwanza, lakini akifika huko kwenye mkutano wake anakibeza chama
chetu.
“Hizi ni
siasa chafu, hivyo ifikie wakati hawa wenzetu nao mara moja moja watangaze
mazuri yaliyofanywa na chama chetu, maana ni mengi na wao wenyewe wanajua
hayo,” alisema.
Yusuphed
anasema katika kipindi cha uongozi cha Kikwete, aliyeanzia mwaka 2005, mambo
mengi yametatuliwa, hasa katika barabara za kuunganisha mikoa, wilaya, bila
kusahau Hospitali, vituo vya afya, zahanati na shule nyingi kujengwa katika
kila Kata.
Kinachofanywa
sasa katika shule hizo ni kuhakikisha kuwa zinakuwa na walimu wa kutosha, huku
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ikitangaza kupeleka zaidi walimu vijijini
kwa kuhakikisha kuwa hawatoi nafasi zaidi sehemu za mijini.
Mwana CCM
huyo anasema kwamba kwa kulijua hilo, wanaamini chama chao kitaendelea kupendwa
na kupewa heshima kubwa zaidi, huku wale wanaosema kinapoteza mvuto ni
wanasiasa wasiokuwa na jipya na wanaohaha kutafuta mabaya yachama chao.
Kwa Taifa
kama Tanzania, changamoto zote zinazoonekana zinafanyiwa kazi kwa wakati, hivyo
watu wasichanganywe na maneno ya wanasiasa.
Anasema
ili maneno yake yawe na nguvu na kuaminiwa na Watanzania, wamejipanga imara
kuhakikisha wanarudisha kiti cha Diwani wa Makumbusho, ambaye mwaka 20110
ilikwenda kwa Chama cha Wananchi wa (CUF), ambaye umuhimu wake bado hauonekani
hasa anaposhindwa kufanya kazi kama alivyojipambanua kwa wapiga kura wake.
Kwa kuona
kushindwa kiutendaji kwa Diwani huyo, ofisi yao yao bado inaendelea kutatua
zile kero za kijamii bila kuangalia nani anahusika katika eneo lao.
Vitu kama
vile ukarabati wa kituo kidogo cha Polisi cha Mwananyamala Mwinjuma, huku mfuko
wake binafsi ukisaidia kwa kiasi kikubwa sare za watu wa ulinzi shirikishi
mitaa ya Mchangani na Kisiwani, bila kusahau ukarabati wa eneo la kulaza magari
linalomilikiwa na chama chao, huku akiwa mwepesi kusaidiana na vijana mbalimbali
katika eneo lao, hasa katika sekta ya michezo na burudani.
Yusuphed
anasema baada ya kuonyesha umakini zaidi katika ufanyaji wake wa kazi pamoja na
kushiriki kusaidiana na Watanzania kukuza ustawi wa Taifa, aliteuliwa kuwa
Mjumbe wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Pugu kwenye Kamati ya Mipango na Fedha,
Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Msingi, shule ya Mchangani, ambapo kwa
kushirikiana na wenzake wamekuwa na mafanikio makubwa.
“Mwaka
jana shule yetu iliweza kufaulisha wanafunzi 182 kati ya wanafunzi 210, wakati
katika matokeo ya mwaka huu, shule hii imeweza kutoa wanafunzi 104 kati ya 175.
“Haya ni
mafanikio yaliyokuja kwa haraka kwa kushirikiana na wenzangu, hivyo naamini
hata serikali kuu, bado watu tunatakiwa tumuamini Kikwete kuwa anaweza
kutuletea maendeleo zaidi kwa kushirikiana na mawaziri wake na watendaji
wengine,” alisema Yusuphed.
Kuhusu
mpasuko wa Chama chao katika mbio za urais za mwaka 2015, mwanachama huyo
anasema kuwa kwakuwa wakati bado, ni vyema wanachama wote wakawa kitu kimoja
kuhakikisha kuwa Taifa linapata maendeleo ili yawe alama ya uchaguzi ujao.
Yusuphed
aliyezaliwa mwaka 1967, Magomeni mtaa wa Mlandizi, anayeishi Mwananyamala
Kisiwani, alimaliza kwa kuwataka Watanzania wote kuwa na imani na chama chao
kwakuwa ndio pekee chenye dira na mvuto wa kuliongoza Taifa lao.
“Hakuna
chama chenye uwezo wa kuliongoza Taifa letu zaidi ya CCM, hivyo wapinzani
wanavyokuja kutulaghai ili wapewe madaraka, wanasahau kuwa vyama vyao havina
mfumo mzuri na wengineo wamejazana watu kutoka eneo moja nab ado wanataka
tuwape uongozi.
“Watanzania
tusikubali kudanganywa na wapinzani, maana bado wanahitaji kufundishwa siasa
zenye tija sanjari na kuelimishwa CCM inavyoongoza kwa amani, utulivu na
kudumisha udugu, huku wapinzani wao sera zao zikiwa ni vurugu na kuwagawa
Watanzania kwa dini na ukanda,” alisema Yusuphed.
No comments:
Post a Comment