Afisa Mauzo ya Nje wa NMB Martin Nshunju akipata
maelezo ya SmartBoard Kutoka Kwa Mfanyakazi wa Kitengo Cha Kompyuta Cha Chuo
Kikuu Cha Dar Es Salaam (UCC) Smartboard hizo zinauzwa na Kitengo cha Komyuta
Cha Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UCC).
Sunday, June 30, 2013
The Dawoodi Bohra leader arrives in Dar es Salaam Welcomed by Mayor Jerry Silaa
A cross section of dawoodi Bohra members who had
come to receive Ali Qadar Wamolai syedi Mufaddal Bhaisaheb Saifuddin in Dar es
Salaam today 29 June 2013 at the Annadil Burhani grounds.
Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb
Saifuddin and his Worship mayor Jerry Silaa planting a palm tree.
Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb
Saifuddin and his Worship mayor Jerry Silaa watering a palm tree.
Mtibwa yasimamisha kwanza usajili wao kwa ajili ya vigogo wa Simba na Yanga
Na Kambi Mbwana, Dar es
Salaam
KOCHA Mkuu wa timu ya
Mtibwa Sugar, Mecky Mexime, amesema kwa sasa wameacha kwanza suala la usajili
hadi watakapogundua kuwa timu kongwe za Simba na Yanga zimemaliza, ili kuepusha
migogoro inayotokea mara kwa mara kutokana na kuchukua hata wale walioingia
mkataba na timu nyingine.
Mexky Mexime, Kocha wa timu ya Mtibwa Sugar
Sakata la usajili kwa
klabu za Ligi Kuu limeibua msisimko wa aina yake, huku timu za Simba, Yanga na
Coastal Union zikionekana kugongana vichwa kwa ajili ya kuboresha vikosi vyao.
Twanga Pepeta kuizundua albamu yao ya Nyumbani ni Nyumbani leo Leaders Club
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAZEE wa Kisigino, bendi ya
African Stars “Twanga Pepeta” leo Jumapili inazindua albamu yake 10
ijulikanyo kwa jina la ‘Nyumbani ni Nyumbani’, katika Viwanja vya Leaders Club,
Kinondoni, sambamba na kusherehekea miaka 15 tangu kuanzishwa kwake.
Mwanamuziki wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu.
Uzinduzi huo utapambwa na
michezo mbali mbali kuanzia saa 3.00 asubuhi ambapo timu nane za mpira wa miguu
zitawania zawadi mbali mbali katikamichuano ijulikanalo kwa jina la ASET
Bonanza.
Saturday, June 29, 2013
Serikali yasimamisha shughuli za uchimbaji dhahabu, mgodi wa Magambazi
Na Mwandishi Wetu, Handeni
SERIKALI kwa kupitia Mkurugenzi wa Wilaya ya Handeni, Khalfany
Haule, imetangaza kupiga marufuku shughuli zote za uchimbaji au utafiti wa
madini, katika Mgodi wa Dhahabu uliopo wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu
Mgodi huo unaojulikana kama Magambazi, uliopo Magamba,
wilayani Handeni mkoani Tanga, umekuwa ukiibuka kwa matamshi ya kila aina, huku
ukikumbukwa pia kuleta mtifuano miongoni mwa wananchi wilayani humo.
Barack Obama aomba kumuona Mzee Nelson Mandela
Rais wa Marekani, Barack Obama pichani.
Rais
Barack Obama wa Marekani ambaye ameshaingia nchini Afrika Kusini amesema kwamba
yupo tayari kumuona Nelson Mandela ikiwa familia yake itamkubalia.
Taarifa za awali kutoka nchini humo zilisema kwamba Barack Obama hataweza kumuona kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini ambaye amelazwa hospitalini.
Taarifa za Ikulu ya Marekani zilisema kwamba kiongozi huyo suala la kumuona Mandela lipo mikononi mwa wanafamilia ya mzee huyo.
Taarifa za awali kutoka nchini humo zilisema kwamba Barack Obama hataweza kumuona kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini ambaye amelazwa hospitalini.
Taarifa za Ikulu ya Marekani zilisema kwamba kiongozi huyo suala la kumuona Mandela lipo mikononi mwa wanafamilia ya mzee huyo.
Ni ujinga wasanii kutumia vifo kuuza sura
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KUNA msemo unaosema kuwa siku zote uungwana ni vitendo. Kama msemo huu ni uongo, basi pia upo karibu na ukweli. Katika jamii yetu, wapo baadhi ya wasanii ambao wana tabia ya kupenda kuuza sura msibani, yaani kujionyesha.
Msanii Aunt Ezekiel. Note, matumizi ya picha hizi katika makala haya sio kwamba hawa ndio walengwa, ila zimetumika kama kufikisha kilio hiki kwa wasanii wote Tanzania.
Ukitaka kuwajua hawa, wala huwezi kupata tabu, maana siku zote huhudhuria kwenye misiba ya watu wanaojulikana. Kama si wao kufariki, basi ndugu zao.
Rose Ndauka
Wakifika hapo, hawana kingine wanachofanya zaidi ya kupita katika makundi ya watu ili waonekane na kunyooshewa vidole. Mbaya zaidi, hata aina ya mavazi wanayovaa pia ni tatizo.
Wema Sepetu
Jambo hili limekuwa likiwakera watu wengi kupita kiasi. Na baadhi yao hufikia kuanza kuwadharau wasanii hao wanaona hakuna mahala pengine kwa kuuza sura zaidi ya msibani.
MAMBO FULANI MUHIMU:Ukijirahisi, inaweza kuwa balaa kwako
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
NI
Jumamosi nyingine msomaji wangu tunakutana tena katika safu hii, kwa ajili ya
kujadili mambo mbalimbali yanayohusu uhusiano na maisha yetu ya kila siku.
Hatua ya muonekano wa picha hii inakuja kama kila mmoja ameamua kwa ridhaa yake pamoja na kujiridhisha kuwa hapo ndipo mahali sahihi.
Hiyo ni
kwa sababu jambo hili linawagusa watu wengi katika jamii, hivyo kwa kulijadili
tunaweza kupeana hili na lile kwa ajili ya kuishi maisha ya furaha.
Wapo
wanaojichanganya na kuishi kwa presha katika mitaa yao, hasa pale wanaposhindwa
kuwa makini katika uamuzi unaohusu mambo ya mapenzi.
Kwenye mapenzi ya kweli, kila kitu kinasema.
Msomaji
wangu mpendwa, katika jamii wapo baadhi ya kina dada wanaojirahisi wanapowaona
wanaume ambao ni machaguo yao halisi.
Friday, June 28, 2013
Simba wafanya mazoezi babu kubwa, angalia picha za GYM
Baadhi ya wachezaji wa Simba wakifanya mazoezi ya GYM wakisimamiwa kwa karibu na kocha wao Mkuu, King Abdallah Kibadeni hayupo pichani na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo Julio.
Kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo Julio wa pili kutoka kulia akisimamia mazoezi ya GYM ya wachezaji wake yanayoendelea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiweka sawa.
Kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo Julio wa pili kutoka kulia akisimamia mazoezi ya GYM.
Mapacha Watatu walishambulia jukwaa la Zoughua Garden kwa kasi ya ajabu
Mkurugenzi wa Mapacha Watatu, Jose Mara kulia akishambulia
jukwaa kwa ushirikiano wa karibuni na Mkurugenzi mwenzie wa bendi hiyo, Khalid
Chokoraa wa kwanza kushoto, huku katikati kukiwa na mcheza shoo wao katika
Ukumbi wa Zoughua Garden Kinondoni Morocco, jijini Dar es Salaam juzi.
Wazabuni wakutana jijini Dar es Salaam leo kujadili changamoto zao
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAZABUNI leo wamekutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
kujadiliana mambo mbalimbali katika kazi zao.
Engineer James Dotto kutoka Kampuni ya SimbaNet (T)
Ltd, akizungumza jambo katika kikao cha pamoja cha Wazabuni kilichofanyika leo
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia changamoto wanazokutana nazo.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkurugenzi Ununuzi na Ushauri wa Government Procurement Services Agence (GPSA) Yoswam Nyongera, huku kikiandaliwa na mratibu wake Francis Mugasa.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkurugenzi Ununuzi na Ushauri wa Government Procurement Services Agence (GPSA) Yoswam Nyongera, huku kikiandaliwa na mratibu wake Francis Mugasa.
Mkurugenzi Ununuzi na Ushauri wa Government Procurement
Services Agence (GPSA) Yoswam Nyongera, akizungumza jambo katika kikao cha
Wazabuni kilichofanyika leo. Kulia kwake ni Mratibu wa kikao hicho, Francis
Mugasa.
Wachezaji wawili wapata nafasi ya kujiunga na Kituo cha kuendeleza vipaji cha Qatar
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Wachezaji wawili kutoka
Tanzania wamechaguliwa miongoni mwa 50 waliofanyiwa majaribio nchini Uganda kwa
ajili ya kuingia katika kituo cha kuendeleza vipaji (centre of excellence)
kilichoko Doha nchini Qatar kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football
Dream.
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura
Taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa Abdulrasul Tahir Bitebo
(15) ambaye ni mshambuliaji kutoka Kituo cha Uwanja wa Karume, na Martin Omela
Tangazi (14) ambaye ni beki kutoka Kituo cha Ukonga ndiyo waliochaguliwa kutoka
Tanzania kuingia katika kituo ambapo watakaa kwa mwezi mmoja kabla ya kusaini
mkataba rasmi wa kuendelezwa.
Cheka: Nipo tayari kwa vita
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA mwenye masumbwi mazito hapa nchini, Francis Cheka,
amesema yupo katika kiwango cha juu, huku akiwa na uchu wa kupambana na
mabondia wakubwa zaidi duniani.
Bondia Francis Cheka
Cheka huenda akacheza na bondia kutoka Marekani mwishoni mwa
mwezi wa nane katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, likiwa ni kuwania Ubingwa wa
Dunia.
Akizungumzia hilo, Cheka alisema kiwango chake
sio cha kupigana kwenye mapambano madogo, hivyo atajisikia raha kama atavaana
na wenye uwezo mkubwa, wakiwamo mabondia kutoka nchini Marekani na kwingineko.
Thursday, June 27, 2013
Kuachwa kwa Juma Kaseja Simba, wadau wacharuka, Edo Kumwembe, Fredrick Mwakalebela wanena wakiungwa mkono na utitiri wa wadau wao mitandaoni
SAKATA la Juma Kaseja kuachwa timu
yake ya Simba, limezidi kuwachanganya wadau wa mpira wa miguu ndani na nje ya
nchi, wengi wakionekana kupinga uamuzi huo.
Haya
ndio maoni ya Edo Kumwembe, mchambuzi na msemaji wa timu ya Coastal Union ya jijini Tanga kwa Wagosi wa Kaya, ambapo pia maoni yake yakafuatiwa na utitiri wa wachangiaji katika mtandao wa facebook.
"Maisha yako kasi na yanachekesha....kiongozi mmoja wa Simba aliwahi kuniambia kuhusu Maximo kumuacha kaseja wakati ule akasema 'mpumbavu tu yule kocha anaiona timu yake'.....jana nimemuuliza kiongozi yule yule kuhusu Simba kumuacha Kaseja kajibu 'Mpumbavu tu yule kipa anaiona timu yake'.........hahahahaha"+.
"Maisha yako kasi na yanachekesha....kiongozi mmoja wa Simba aliwahi kuniambia kuhusu Maximo kumuacha kaseja wakati ule akasema 'mpumbavu tu yule kocha anaiona timu yake'.....jana nimemuuliza kiongozi yule yule kuhusu Simba kumuacha Kaseja kajibu 'Mpumbavu tu yule kipa anaiona timu yake'.........hahahahaha"+.
Maoni ya Fredrick Mwakalebela, Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Fredrick Mwakalebela.
"Mimisikubaliani kama ni kweli kitendo walichomfanyai kaseja simba sio cha kiustaarabu, hata kama wanamuache sio kivile, anatakiwa apewe taarifa mapema, aagwe kwa heshima kutokana na mchango wake simba, cha kushangaza hajawahi kukaa benchi ghafla kiwango kishuke, captain Nationalteam????????????????.K
Angella
Michael Msangi ni mwandishi mwandamizi wa TBC 1 naye akasema kwa ufupi, "aibu sana"
2 hours ago · Like
Grace
Hoka kushoto mhariri wa Michezo wa Gazeti la Bingwa naye akasema, "sio hivyo edo kuna mmoja wa
kiongozi kasema eti kasema ana hela kuliko baadhi ya viongozi"
16 minutes ago · Like.
Haya ndio maoni ya Zena
Chande, mwandishi mwandamizi wa michezo wa Gazeti la Habari Leo.
We unadhani Fedha ndio ingekuwa faraja kwa Kaseja? Masoud Sanani, walipaswa kumuonyesha heshima tu, tena sio kumfanyia sherehe, wangemwita tu na kumueleza kwamba hatuongezi mkataba na wewe, hiyo ingetosha, lakini hii ya kuzungumza kwenye vyombo vya habari wakati mwenyewe yupo haitoshi,bosi wangu,
We unadhani Fedha ndio ingekuwa faraja kwa Kaseja? Masoud Sanani, walipaswa kumuonyesha heshima tu, tena sio kumfanyia sherehe, wangemwita tu na kumueleza kwamba hatuongezi mkataba na wewe, hiyo ingetosha, lakini hii ya kuzungumza kwenye vyombo vya habari wakati mwenyewe yupo haitoshi,bosi wangu,
2 hours ago · Like · 1.
Katikaa mitandao ya kijamii
kama vile twitter, facebook na mingineyo kumekuwa kukiendelea mijadala ya wadau
wa soka na kuonyesha kuwa uwezo wa Kaseja unaheshimika nchini kote. Pitia maoni yote.
Mgogoro waibuka wa kugombea shule ya Sekondari Ndembela, wilayani Rungwe
Na Esther Macha,
Mbeya
SAKATA la Mgogoro
uongozi shule ya sekondari ya Ndembela ambayo inamilikiwa na Kanisa la Wasabato
na wananchi wanaoizunguka shule hiyo uliodumu kwa muda mrefu umechukua sura
mpya baada ya uongozi wa serikali wilayani Rungwe kupora vifaa vya shule na kutia
kufuri majengo ya shule hiyo huku wakiwataka wamilikiwa kukabidhi
majengo hayo kwa wananchi.
Coastal union kutua Arusha Julai 4 tayari kwa mashindano ya Rolling Stone
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
TIMU ya
vijana ya Coastal Union inatarajia kuelekea jijini Arusha, Julai nne mwaka huu
tayari kuanza kwa michuano ya Kombe la Rolling Stone, iliyopangwa kuanza
kutimua vumbi Julai sita.
Kikosi cha vijana wa Coastal Union kikijifua uwanjani.
Coastal
wanakwenda Arusha huku wakiwa na kumbukumbu ya kushika nafasi ya pili katika
mashindano yaliyofanyika mwaka jana nchini Burundi na kuitangaza vyema
Tanzania.
Kamati ya Utendaji ya Simba kukutana leo jioni Dar es Salaam
Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
KAMATI ya Utendaji ya
klabu ya Simba, leo jioni inatarajia kukutana kwa ajili ya kufanya kikao cha
kujadili mambo mbalimbali yanayohusu timu yao, ukiwapo mchakato wa usajili.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage.
Simba inakutana huku
benchi la ufundi likihaha juu ya mlinda mlango wake, Juma Kaseja, ambaye
ameripotiwa kuwa huenda akawa nje ya timu hiyo kwa msimu mwingine wa ligi, japo
kocha wa Simba Mkuu, King Abdallah Kibadeni, ameonyesha nia ya kipa huyo abaki
kukipiga kwa msimu ujao.
Mohamed Matumla, mtoto wa Snake Boy kuzipiga na Khamis Mohamed, Julai sita, DDC Keko
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BONDIA Mohamed Matumla pichani anatarajia kupanda ulingoni Julai
6 mwaka huu katika Ukumbi wa DDC Keko, kwa ajili ya kupambana na Hamis Mohamed
kutoka Gym ya Mzazi.
Akizungumza na mwandishi wetu mwandaaji wa mpambano huo
Shabani Adios 'Mwaya mwaya' amesema mpambano huo utasindikizwa na mabondia
mbalimbali wanaotamba katika masumbwi.
Wednesday, June 26, 2013
Kiwanja cha wazi chaleta utata Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga
Na Mwandishi Wetu, Handeni
HALMASHAURI ya Wilaya ya Handeni imekumbwa na kashfa nzito kufuatia kugawa kiwanja cha wazi kilichopo maeneo ya mtaa wa Zizini kwa mfanyabiashara Said Khalfan bila kuzingatia sheria na kanuni za ugawaji wa ardhi.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Handeni imekumbwa na kashfa nzito kufuatia kugawa kiwanja cha wazi kilichopo maeneo ya mtaa wa Zizini kwa mfanyabiashara Said Khalfan bila kuzingatia sheria na kanuni za ugawaji wa ardhi.
Eneo la wazi lililopo mtaa wa Zizini Handeni
Tanga ambalo limejengwa nyumba ndogo ya biashara kama inavyoonekana kwa mbele
lipo katikati ya hifadhi ya barabara na msongo mkubwa wa umeme. Picha na
Mwandishi wetu.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa wilayani
Handeni, umebaini kuwa kiwanja hicho kipo kwenye ndani ya hifadhi ya barabara
pamoja na msongo mkubwa wa umeme.
Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Mtaa huo
Musa Rajabu Kasidi au ‘Jaba’ alisema kiwanja hicho cha wazi kilikuwa ni kati ya
viwanja sita ambavyo halmashauri ya wilaya hiyo ilibainisha kuwa ni viwanja vya
wazi kwa kuwa tayari vilikuwa kwenye hifadhi ya barabara lakini alishangaa
kuona mfanyabishara huyo akiendeleza ujenzi.
Ziara ya Barack Obama: Tanzania wajivunia kwa fursa za kibiashara
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kwa kupitia Waziri wake wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernad Membe, amesema ujio wa Rais wa Marekani, Barrack Obama,
utatoa fursa pana za kibiashara kwa Watanzania na kukuza uchumi wao.
Rais wa Marekani, Barack Obama, pichani, akiwa kwenye mipango ya kuitembelea nchini Tanzania mwishoni mwa wiki hii katika ziara ya kikazi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Bernard Membe.
Obama anatarajiwa kuwasili
mwishoni mwa wiki hii, huku jiji la Dar es Salaam kwa sasa linatikisika
kutokana na kuboreshwa kwa ajili ya ujio huo wa Rais wa Marekani.
Mmoja ashikiliwa kwa kudaiwa kutaka kuua kwa njia ya imani za ushirikina, Kibaha mkoani Pwani
Mama huyu anayeitwa Magreth Simon
Nkwera, akiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa akidaiwa kutaka kuua kwa njia ya imani za ushirikina, Kibaha Maili Moja,
mkoani Pwani.
Mama huyo akiwa katika gari la polisi.
Baada ya kunaswa na polisi Kibaha mkoani Pwani.
Mume wa anayedaiwa kutaka kuua, Douglas Shirima, aliiambia Handeni Kwetu Blog kuwa kwa sasa hajielewi baada ya kuona mambo mazito kwenye barua yenye majina ya watu ambao mama huyo alitaka wauliwe.
"Naona hatari tupu, maana barua hiyo niliyoonyeshwa ni nzito mno, hivyo sijui nini kinaendelea," alisema kwa ufupi. Taarifa kamili zinaendelea kufuatiliwa...
Mama huyo akiwa katika gari la polisi.
Baada ya kunaswa na polisi Kibaha mkoani Pwani.
Mume wa anayedaiwa kutaka kuua, Douglas Shirima, aliiambia Handeni Kwetu Blog kuwa kwa sasa hajielewi baada ya kuona mambo mazito kwenye barua yenye majina ya watu ambao mama huyo alitaka wauliwe.
"Naona hatari tupu, maana barua hiyo niliyoonyeshwa ni nzito mno, hivyo sijui nini kinaendelea," alisema kwa ufupi. Taarifa kamili zinaendelea kufuatiliwa...
Rais Kikwete kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri leo mjini Dodoma
Rais
Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda baada ya kuwasili
kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma leo kwa ajili ya kuongoza kikao cha kamati Kuu
ya CCM na Baraza la Mawaziri. Picha na Ofisi ya waziri Mkuu.
Rais Jakaya Kikwete
akiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda baada ya kuwasili kwenye uwanja
wa ndege wa Dodoma leo kwa ajili ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM na Baraza
la Mawaziri . Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Subscribe to:
Posts (Atom)