Msanii Simon Mwapagata
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII wa filamu Tanzania, Simon Mwapagata, amewataka wasanii
wenzake kuupa ushirikiano viongozi wa vyama wanaohusika na mambo
sanaa ya maigizo, ili waendeleze harakati za kupigania maendeleo
yao.
Mwapagata aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam, akizungumzia
maendeleo ya wasanii katika patashika ya serikali na wasanii katika
mvutano wa sheria za filamu.
Akizungumza mapema wiki hii, Mwapagata, alisema kwamba viongozi wao,
wakiwamo wale wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), wanafanya
kazi nzuri kwa kuhakikisha kuwa sheria za filamu zinaleta tija kwa
wasanii.
Alisema kwa sababu hiyo wasanii wote na wadau wenye mapenzi mema na
wasanii wanahitaji kuwapa ushirikiano, maana viongozi wao wanafanya
kazi kwa ajili ya maisha ya wasanii wote.
"Tuwape ushirikiano viongozi wetu kwa kuhakikisha kuwa harakati za
kuboresha maisha ya wasanii zinafanikiwa kwa vitendo, ukizingatia
kwamba sheria zilizoundwa ni mbaya na hazina tija.
"Hatuhitaji sheria zinazoweza kuwakandamiza wasanii na waandaaji wa
filamu, huku wasambazaji wakiachiwa watese kwa kutunyonya, huku
ufedhuli huo ukisaidiwa na baadhi ya watendaji wa COSOTA na Bodi ya
Filamu," alisema.
Kwa kuweza kutafuta njia ya kupambana na sheria hizo, wasanii wa
filamu Tanzania walifanya kikao cha pamoja mwishoni mwa wiki katika
Ukumbi wa Vijana, Kinondoni.

No comments:
Post a Comment