Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Soka nchini
(TFF), limesema Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho hilo imepanga kukutana kwa
mara kwanza kesho Jumatano, ili kupitia majina yote na pingamizi zilizowekwa
kwa wagombea wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi za TFF.
Wagombea ambao wamewekewa
pingamizi ni pamoja na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji, anayewania nafasi ya
Bodi ya Ligi, Michael Wambura, anayetaka nafasi ya Makamu wa Rais, Athuman
Nyamlani anayewania Urais, Jamal Malinzi Urais, sambamba na Mugisha Garibona,
Vedastus Lufano wanaowania nafasi ya Ujumbe, huku wakiwekewa pingamizi na Paul
Mhangwa.
Katika taarifa yake iliyotumwa kwenye
vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Angetile Osiah, alisema
Kamati ya Uchaguzi itapitia pingamizi zote zilizowekwa kwa wagombea hao.
Osiah alisema katika kikao
hicho cha kujadili pingamizi kitakachoanza saa nne asubuhi, waombaji wote wa
nafasi za uongozi na wale walioweka pingamizi wanatakiwa kufika katika tukio
hilo.
“Wale walioweka pingamizi kwa
wagombea na wanaowania nafasi za uongozi za TFF wote watashiriki kikao hicho
cha kujadili pingamizi,” ilisema taarifa hiyo.
Uchaguzi wa TFF umepangwa
kufanyika Februari 24 jijini Dar es Salaam, huku wadau mahiri wa michezo
wakipigana vikumbo kuzitaka nafasi mbalimbali za Shirikisho hilo nchini.
Nafasi zote zimekuwa na
ushindani wa aina yake, huku majina ya wadau kama vile Malinzi, Nyamlani kwa
nafasi ya urais, bila kusahau Manji na Wambura wakipigania ubosi wa TFF katika
Uchaguzi wa mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment