https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, January 13, 2013

Ngwasuma hapatoshi leo New Msasani Club

Wanenguaji wa Wazee wa Ngwasuma wakiwa jukwaani

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya FM Academia, Maarufu kama Wazee wa Ngwasuma, leo inatarajia kufanya shoo ya nguvu katika Ukumbi wake wa New
Msasani Club, Msasani, jijini Dar es Salaam.

Shoo hiyo ni ya kumalizia wiki, huku wakiitumia kama sehemu ya kuwaburudisha zaidi mashabiki wao wanaoingia kwa wingi katika
ukumbi huo kuwaona wakali hao.

Akizungumza na Handeni Kwetu, leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa bendi hiyo, Kelvin Mkinga, alisema mashabiki wao watajionea burudani za aina yake.

Alisema wanamuziki wao wamejipanga imara kwa ajili ya kutoa vionjo ili kuwapatia burudani za aina yake mashabiki wao
wanaoendelea kuwaunga mkono.

“Naomba mashabiki wetu waje kwa wingi kujionea jinsi wazee wa Ngwasuma wanavyofanya mambo makubwa katika tasnia ya muziki wa
dansi hapa nchini.

“Naamini mambo yatakuwa mazuri, maana wanamuziki wetu wamejipanga imara kuhakikisha kuwa wapenzi wao wanaburudika zaidi.
Ngwasuma ipo chini ya Rais wa Vijana, Nyosh El Sadaat, akiwa na wanamuziki wengine mahiri wanaoiweka juu bendi hiyo ya FM
Academia,” alisema.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...