Na Mwandishi Wetu, Kilindi
MKUU wa Wilaya ya Kilindi,
pichani, Selemani Liwowa, ametangaza njaa katika wilaya yake na kutaja kata
zilizoathiriwa zaidi kuwa ni pamoja na Saunyi, Kwediboma, Mkindi, Jaira na
Kisangasa.
Akizungumza na Handeni Kwetu leo
asubuhi wilayani hapa, Liwowa alisema tayari wameshaomba chakula kutoka kwenye
mfuko wa hifadhi wa chakula (NFRA), wakiomba kupewa tani 70,000.
Mkuu huyo wa wilaya alisema
kilichosababisha njaa katika eneo wilaya yao ni kutokana na watu kuuza chakula
chao mapema, huku wakishindwa kujiwekea akiba katika kaya zao.
Alisema jambo hilo ni baya, huku
wakitarajia chakula hicho kitakachapolekwa kuuzwa kwa bei isiyozidi 750 hadi
900, wakati bei iliyopo sasa ni 1200 hadi 1300 na kuwafanya watu waishi kwa
tabu.
“Tumeshafanya utaratibu wa
kuwasiliana na wenzetu wakiwamo NRFA ili watuletee chakula cha bei rahisi kwa
ajili ya watu walioathiriwa na njaa hii katika wilaya yangu ya Kilindi.
“Naamini chakula kitakapofika
wananchi wetu watakipata kwa bei rahisi, maana masharti ni kwamba watu
wachangie kidogo kwa bei yaa 750 au 900,” alisema Liwowa, Mkuu wa wilaya
Kilindi.
Mbali na Kilindi, wilaya ya
Handeni nayo imekumbwa na baa la njaa, baada ya Mkuu wake wa wilaya, Muhingo
Rweyemamu naye kuomba msaada kwa ajili ya kuwanusuru baadhi ya wananchi wake
wilayani humo, ambazo zote kwa pamoja zinaunda Mkoa wa Tanga, unaongozwa na
Chiku Gallawa.
No comments:
Post a Comment