Na Mwandishi Wetu, Kenya
BAO pekee la mshambuliaji Gaudence Mwaikimba wa Azam FC,
limeipa ushindi timu hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya SOFAPAKA
uliochezwa jana Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, Kenya.
Azam FC imecheza mchezo wake wa pili wa kirafiki, juzi jioni
walifungwa 2-1 na AFC Leopard katika mechi iliyochezwa uwanja huo.
Katika mchezo huo, kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu
zote kutoka suluhu, wachezaji wa Azam FC Himid Mao alipiga mpira wa adhabu
uliogonga mwamba na kurudi ndani katika dakika ya 14, dk 22 Seif Abdalah akiwa
na lango la SOFAPAKA alipiga mpira uliotoka nje.
Azam FC waliendelea kufanya amshambulizi katika lango la
SOFAPAKA, dk 27 na 45 Michael Bolou alipiga shuti likatoka nje na dakika ya 37
Humprey Mieno alishindwa kufunga na badala yake shuti likaokolewa na kipa wa
SOFAPAKA, Duncan Ochieng
SOFAPAKA dk 24 Kago Dawson alikosa nafasi ya wazi kwa kupiga
shuti lililodakwa vyema na kipa chipukizi wa Azam FC, Aishi Salum ambaye
aliweza kulinda lango hilo katika vipindi vyote.Kipindi cha pili Azam FC walifanya mabadiliko walitoka Samih Haji Nuhu, Michael Bolou, Khamis Mcha na David Mwantika nafasi zao zikachukuliwa Luckson Kakolaki, Abdulhalim Humud, Gaudence Mwaikimba na Malika Ndeule,mabadiliko hayo yaliimarisha kikosi hicho na kufanya mashambulizi mengi.
Kipa Aishi Salum alitumia vema nafasi aliyoipata katika
mchezo huo kwa kuzuia mashuti ya wachezaji wa SOFAPAKA na kusimama vema katika
nafasi hiyo, kutokana na umri wake mdogo amecheza katika kiwango cha juu kama
anavyokuwa golikipa namba moja Mwadini Ally ambaye jana alipumzishwa na
kuwapisha vijana Aishi na Jackson Wandwi.
Azam FC walipata goli katika dakika ya 58 kupitia kwa mkwaju
wa penati iliyopigwa na Mwaikimba baada ya beki wa SOFAPAKA Kisuya Colins
kunawa mpira katika eneo la hatari.
Goli hilo lilidumu hadi kumalizika kwa mchezo huo na
kuifanya Azam FC kushinda 1-0 katika mchezo huo ulioshuhudiwa na Raisi wa
SOFAPAKA, Elly Kalekwa na Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrissa.
Azam FC kesho itapumzika na kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa
City ambao watacheza siku ya Jumanne dhidi ya KCB na kumalizia safari hiyo ya
mechi za kirafiki ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya ligi kuu na Mashindano ya
Kombe la Shirikisho Afrika.
Azam FC, Aishi Salum, Himid Mao/Omary Mtaki, Samih Haji
Nuhu/Luckson Kakolaki, Jockins Atudo, David Mwantika/Malika Ndeule 45’, Michael
Bolou/Abdulhalim Humud 45’, Humphrey Mieno/Ibrahim Mwaipopo 66’, Salum
Abibakar, Brian Umony Jabir Aziz 81’, Seif Abdalah/Uhuru seleman 68’, Khamis
Mcha/ Gaudence Mwaikimba.
SOFAPAKA Duncan
Ochieng/Okeko David, Shivash Collins, Kisuya Collins, Situma James, Felly
Mulumba, Abdalah Nyanzi, Hilary Echesa, Koko Manopi, Kagogo Patrick/George
Owino, Kago Dawson na John Baraza/Tarumbwa Cabadian.
No comments:
Post a Comment