Yameandikwa na Rashid Hassan Kilo, kutoka kijiji cha Misima, wilayani Handeni, mkoani Tanga katika mtandao wa facebook.
HAYA ni malalamiko ya watu wa kijiji cha Misima, wilayani Handeni mkoani
Tanga, yameandikwa na Rashid Hassan Kilo, nikaona niyapachike hapa
kutoka kwenye wall yake...... Sijaongeza wala kupunguza...
Habari za asubuhi "Wana wa Handeni"
Kwangu kumekucha salama hofu na mashaka ni kwenu. Hoja yangu leo ni juu
ya matangazo yaliyozagaa kila kona ndani ya mipaka ya kijiji cha Misima
yanayohusu kuchangia ujenzi wa maabala ya shule ya sekondari Misima
katika mchanganuo ufuatao:
1. Nguvu kazi 10,000@
2. Ng'ombe 3000@
3. Mbuzi/kondoo 1000@
Labda niishie hapo kwanza kwakuwa mlolongo ni mrefu sana kwani ni zaidi
ya vipau mbele 26 na viwango tofauti vya kulipia. Mwisho ni jina
Mtendaji wa kijiji
S. KIDUNDA
VEO-MISIMA.
Japo tunajuwa haya
ni maendeleo lakini kwanini tusingeitishwa mkutano na kupata ufafanuzi
juu ya ghalama za ujenzi wa maabala hiyo, gawanya kwa idadi ya watu,
mifugo, maduka, migahawa na vyanzo vyote vya vijiji 5 vya kata ya
Misima?
Katika ibara ya 18(d) ya Katiba tuanayotumia sasa ya
1977 "Kila mtu anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio
mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu
masuala muhimu kwa jamii."
Leo hili lakujenga maabala ni tukio
muhimu sana kwetu na kwa vizazi vyetu ila jinsi ya uongozi wa kiimla wa
Misima unavyotufanyia umeyatokomeza na unazidi kuyatokomeza kabisa
maendeleo ya Misima.
Leo hii ni miaka mingi imepita bila
kusomewa mapato na matumizi, lakini pia ni zaidi ya mwaka 1.6 tangu
18/10/2012 hatujafanya mkutano kwa viongozi kutuogopa kwa maovu yao, leo
hatupo tayari kuchangia bila kupata mchanganuo unaoeleweka lakini pia
hatupo tayari kutoa pesa kwa kwa viongozi wasio waaminifu.
Lakini la mwisho kiwango kilichowekwa ni kikubwa bora ingekuwa kila kaya
10000, lakini nguvu kazi? Kwa kipindi hiki ambacho wachangiaji wenyewe
wanategemea chakula cha msaada toka serikalini? Ningeomba viongozi
wangefanya mkutano kwanza na wanakijiji ili kujadiliana kwanza kuliko
kutuogopa, mtatuogopa hadi lini?
Friday, January 31, 2014
Julio aitwa Mwadui FC Shinyanga
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA msaidizi wa zamani wa Simba,
Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ameitwa katika kuinoa timu ya Mwadui FC inayoshiriki
ligi daraja la kwanza, huku akisubiriwa kwa hamu kuona timu hiyo inapata tiketi
ya kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Kocha wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo Julio ambaye yupo kwenye mipango ya kufundisha timu ya Mwadui FC.
Habari zilizotufikia katika chumba chetu cha habari zinasema kuwa tayari Julio ameshawasili katika timu hiyo kwa ajili ya kuanza taratibu za kuinoa timu hiyo.
Julio alikuwa kocha msaidizi wa
Simba, hata hivyo alienguliwa akiwa sambamba na kocha wake mkuu, King Abdallah
Kibadeni, jambo linalomuumiza kichwa hadi leo.
Akizungumza kwa njia ya
simu, Julio alisema kuwa ni mapema mno kuelezea maisha yake ya soka, ikiwa ni
miezi michache tangu alipoenguliwa Simba kwa mizengwe.
Pitia historia mpiga tumba wa Twanga Pepeta, MCD aliyezikwa juzi mkoani Kilimanjaro
Marehemu MCD enzi za uhai wake
Historia ya Marehemu Soud Mohammed Timbo (MCD) 1973-2014. Kama
ilivyosomwa na Shemeji yake Bwana Mlanzi siku ya Maziko Jumatano tarehe
29-01-2014.-Marehemu alizaliwa Mwaka 1973 mkoani Kilimanjaro.
-MCD alisoma katika Shule ya Msingi Mawenzi iliyopo Manispaa ya Moshi na alihitimu mwaka 1987. Alianza Masomo ya Sekondari katika Shule ya Shemsanga Korogwe Tanga kuanzia 1988-1992. Baada ya kumaliza masomo ya Sekondari alijiunga na Chuo cha Sanaa Bagamoyo.
-Baada ya kumaliza Chuo cha Sanaa Bagamoyo, alifanya kazi katika Bendi ya Diamond Sound "Wana Dar es salaam Ikibinda Nkoi", African Stars Band "Twanga Pepeta", Mashujaa Musica kwa muda mfupi na baadae alirejea katika Bendi ya African Stars "Twanga Pepeta" mpaka mauti yalipomfika.
Thursday, January 30, 2014
Mzee Yusuph: Tumejipanga kuwapa raha Morogoro
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa kundi la Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuph,
amewataka wadau wa muziki wajipange imara kwa ajili ya kupokea burudani zao
katika onyesho la aina yake litakalofanyika Januari 31 katika Ukumbi wa Tanzanite
Complex, uliopo mjini Morogoro.
Mzee Yusuph, pichani.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mzee Yusuph, alisema kuwa amejipanga yeye na waimbaji wake kujibu maswali
kwanini wao ni vinara katika muziki huo.
Alisema kuwa mkoa Morogoro ni kati ya ile inayopenda muziki
wao, hivyo suala hilo limemfanya aone shauku ya kufanya kazi nzuri jukwaani
kwenye onyesho hilo.
“Nimejipanga imara kama Mkurugenzi kuwapatia burudani kabambe wadau na mashabiki
wetu katika onyesho la mkoani Morogoro ambapo tutafanya vitu vya aina yake.
“Tutaimba nyimbo zetu mpya na zile za zamani ambapo wadau
wetu wana kila sababu ya kuja kupata vitu vya aina yake kutoka kwetu Jahazi,
lenye waimbaji hodari,” alisema.
Jahazi ni miongoni mwa makundi ya muziki wa taarabu yenye
waimbaji wenye uwezo wa juu katika tasnia ya muziki wa taarabu hapa nchini,
huku mashabiki wengi wakiwaunga mkono.
Mkuchika aelezea adha ya utawala bora na changamoto zake Tanzania
Kaptemo mstaafu George Mkuchika, pichani. |
WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais anayeshuhulikia
Utawala Bora, Kapteni mstaafu, George Mkuchika amesema migogoro ya
ardhi, mauaji ya maalbino na vikongwe, wanachi kujichukulia sheria
mikononi, rushwa pamoja na ujangili zinadaiwa kuwa moja ya sababu
zinazochangia kuporomoka kwa Tanzania katika viwango vya utawala bora
duniani.
Mkuchika aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika
kikao cha 30 cha kamati ya ushauri wa mkoa wa Kilimanjaro (RCC) kikao
ambacho ni cha kwanza kwa mwaka 2014 na maalum kwa ajili ya kujadili
vipauumbele vya Bajeti ya Mkoa huo kwa mwaka 2014/2015.
Kaptein Mkuchika alisema kutokana na taarifa zilizotolewa hivi karibuni, Tanzania inashika nafasi ya pili kwa utawala bora nyuma ya Rwanda kwa nchi za ukanda wa Afrika mashariki nyuma ya Rwanda, 17 katika ukanda wa Afrika na 102 kati ya nchi 176 duniani ambapo kwa mujibu wa taarifa hizo Tanzania imeshuka kiwango katika ukanda wa Afrika katika kipindi cha miaka miwili.
Kaptein Mkuchika alisema kutokana na taarifa zilizotolewa hivi karibuni, Tanzania inashika nafasi ya pili kwa utawala bora nyuma ya Rwanda kwa nchi za ukanda wa Afrika mashariki nyuma ya Rwanda, 17 katika ukanda wa Afrika na 102 kati ya nchi 176 duniani ambapo kwa mujibu wa taarifa hizo Tanzania imeshuka kiwango katika ukanda wa Afrika katika kipindi cha miaka miwili.
CCM yaelezea mafanikio yake ikiwa ni kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya miakaa 37 ya kuzaliwa kwake
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mkutano wa CCM Mkoa wa Mbeya.
Wakati CCM inatimiza miaka 37 tangia kuanzishwa kwake februari 5 mwaka
1977,Chama hicho kinajivunia sana mafanikio makubwa kiliyopata hasa
katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwa Watanzania ,kutunza na
kuilinda Amani ya nchi hii na kujenga misingi imara ya uchumi wa
nchi,akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano CCM
Mkoa wa Mbeya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye alisema sherehe za miaka 37 zimeanza nchi nzima na
zilizinduliwa rasmi tarehe 26 na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar)
Dk.Ali Mohamed Shein Unguja Zanzibar.
Kilele cha sherehe hizi kitakua tarehe 2 februari ,Nape alisema “kwa
nini tarehe mbili na sio tano ni kwa sababu tarehe tano ni siku ya kazi
hivyo tumeona tufanye tarehe mbili ili tuwaruhusu watu wengi zaidi
waweze kushiriki”.
Wadau kibao wamzika MCD mkoani Kilimanjaro
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
HATIMAYE mwili wa mwanamuziki wa zamani wa bendi ya The
African Stars, Twanga Pepeta, Soud Mohamed ‘MCD’ ulizikwa jana katika makaburi
ya Njolo, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
Wananchi na wadau wa muziki wakimzika Mpiga tumba wa zamani wa Twanga Pepeta, marehemu MCD.
Marehemu MCD alifariki juzi mjini Moshi baada ya kuugua kwa
muda mrefu, huku akiacha pengo la majonzi makubwa katika tasnia ya muziki wa
dansi nchini.
Akizungumza mara baada ya maziko ya MDC, Meneja wa bendi ya
Twanga Pepeta, Hassan Rehani, aliwashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha
mazishi ya mpiga tumba wao huyo nguli nchini.
“Wadau mbalimbali waliweza kujitokeza kwa wingi katika vikao
vya kujadili msiba wa MCD na hatimaye kufika nyumbani kwa marehemu Moshi, mkoani Kilimanjaro.
“Twanga Pepeta imepata pigo zito kwa kuondokewa na MCD,
ambapo pia tunaamini kuwa uwezo wake utaenziwa na wadau wote wa muziki wa
dansi,” alisema.
MCD aliwahi kufanya kazi na bendi mbalimbali, ikiwamo
Mashujaa Musica, ambapo pia walishirikiana na wadau walioguswa na msiba huo
mzito.
Tuesday, January 28, 2014
Wadau wa ngumi wasifia mkutano wao
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KATIBU wa Ngumi za Kulipwa hapa nchini, Ibrahim Kamwe, amesema
kwamba mkutano wao utakaofanyika Februari Mosi mwaka Vijana Hall Kinondoni,
utakuwa na faida kubwa ya kujadili sekta hiyo ya masumbwi.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kamwe alisema kwamba mkutano
huo umepewa Baraka zote na Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa (TPBO),
Yasin Abdallah.
Alisema kuwa anaamini wadau wote wa masumbwi, wakiwamo mapromota
watajumuika pamoja kutafuta namna bora ya kuendeleza mchezo wa masumbwi hapa
nchini.
“Huu ni mkutano wa kwanza unaofanyika nchini huku ukiwa na manufaa
makubwa kwa sisi wadau wa masumbwi hapa nchini, hivyo naomba tujiandaye vizuri
kwa maendeleo yetu.
"Mkutano utaanza mapema asubuhi, huku nikiamini kuwa kila kitu
kitakwenda kama kilivyopangwa, ukizingatia kuwa mbali na mapromota, pia
mabondia na makocha wa ngumi ni miongoni mwa wanaotarajiwa khudhuria,” alisema
Kamwe.
Mchezo wa masumbwi unatajwa kati ya ile iliyopunguza makali yake,
licha ya wadau mbalimbali katika tasnia hiyo kuendelea kuupigania ili ubaki
katika mafanikio yake kama zamani.
Jumuiya ya Wazazi CCM Wilayani Kongwa yajipanga
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
JUMUIYA ya
Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani Kongwa mkoani Dodoma, Januari 29
itaandaa mechi ya kirafiki itakayokutanisha timu za Kata ya Segeri kwa ajili ya
kusherehekea miaka 37 ya CCM tangu kuzaliwa kwake inayoadhimishwa Februari tano
kila mwaka.
Akizungumza
jana kwa njia ya simu kutoka mkoani Dodoma, Katibu wa Jumuiya hiyo, Hussein
Mwaikambo, alisema kuwa lengo la mchezo huo ni kuwakusanya wadau wa michezo na
kutafuta fursa ya kusherehekea kwa pamoja kuzaliwa kwa CCM.
Alisema kuwa
lengo lao ni kutumia fursa hiyo kufurahia kuzaliwa kwa chama chao, wakiamini
kuwa vijana watapata nafasi ya kubadilishana mawazo na kujiweka sawa kiafya.
“Katika
kuelekea miaka 37 ya CCM ambapo kwa mwaka huu sherehe hizi zitafanyika mkoani
Mbeya tumejipanga kwa sisi wilaya ya Kongwa kujipanga kwa vitu vingi ikiwapo
mechi ya kirafiki ambayo wakati huu maandalizi yake yanaendelea.
Hili
litakuwa tukio muhimu ambalo litatangazwa litakapokamilika, hasa kwa timu
zitakazochaguliwa ambazo zitacheza baada ya vitu vyote kufanyika asubuhi hadi
jioni,” alisema.
Kwa mujibu
wa Mwaikambo, taratibu zote za sherehe hizo zitaendelea kuratibiwa ili
kuhakikisha kuwa tukio hilo la burudani na michezo linafanyika kwa mafanikio
makubwa.
Cheza Kidansi wakutana kuujadili muziki wa dansi
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WADAU wa
muziki wa dansi wanaotokea katika mkusanyiko unaojulikana kama Cheza Kidansi,
juzi walifanya kikao cha kwanza na kuadhimia mpango wao kuwawezesha wanamuziki
wa muziki huo na kuwakwamua kiuchumi.
Wadau wakijadiliana jambo katika kikao hicho cha Cheza Kidansi.
Kikao hicho
kilifanyika katika Ukumbi wa Garden Breeze, ambapo kilihudhuriwa pia na mlezi
wao Yusuph Mhandeni, maarufu kama Yusuphed Mhandeni, ambaye ni Mchumi wa Kata
ya Makumbusho katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza
katika kikao hicho, Yusuphed alisema kuwa mengi yaliyojadiliwa katika kikao
hicho ni kuona muziki wa dansi unarudi katika chati yake ili wanamuziki
wajimudu kiuchumi.
Alisema
wanamuziki wengi wa dansi hawana maisha mazuri kuliko wenzao wa Bongo Fleva,
hivyo hilo ni kati ya changamoto zinazoendelea kuwakumba.
Mwandishi wa habari aula uenyekiti UVCCM mkoani Kilimanjaro
Arnold Swai (wa kwanza kushoto)wakati wa upigaji kura, zoezi lilofanyika juzi, wilayani Hai kuziba pengo la nafasi ya Mwenyekiti |
Mjumbe wa Halmshauri kuu CCM wilaya ya Hai, Fuya Kimbita, akizungumza katika zoezi la kupiga kura lililoshuhudia Mwandishi wa Habari Leo, Arnold Swai akiibuka kidedea. |
Arnold Swai akihutubia baada ya kutangazwa Mwenyekiti Mpya kwa kushinda uchaguzi uliofanyika juzi. Swai alipata kura 151 kati ya kura 222 zilizopigwa |
Sunday, January 26, 2014
Madabida mgeni rasmi Diwani Cup
Na Kambi Mbwana, Dares Salaam
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es
Salaam, Ramadhan Madabida leo atakuwa mgeni rasmi katika mashindano ya Diwani
Cup yatakayofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mbagala Kuu, iliyopo
katika Kata ya Mbagala Kuu.
Timu za Kuzazi na Sansiro kutoka kata hiyo zitapambana
kuwania zawadi ya kombe, ng'ombe na jezi seti ambazo ni zawadi za mshindi wa
kwnza.
Madabida ndiye atakayekabidhi zawadi ya mshindi wa kwanza na
ile ya pili ambaye ataondoka na jezi seti moja huku msindi wa tatu atapewa jezi
seti moja.
Akizungumza jana, Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu,
Benson Malawandu, ambaye ndiye mwandaaji wa mashindano hayo alisema fainali
hiyo inatarajiwa kuwa ya aina yake kutokana na kukutanisha timu zenye upinzani
wa jadi.
Alisema kilichopelekea kumwalika Madabida katika mashindano
ni kutokana na kiongozi kuwa ni mpenda michezo ambaye amekuwa akitoa
kuhakikisha anasaidia vijana.
Malawandu akizungumzia mashindano hayo kwa ujumla alisema kwa
kiasi kikubwa malengo yametimia.
Alisema wakati anayaanzisha alikuwa na malengo ya kukutanisha
vijana pamoja, kutoa fursa kwa vijana kutumia michezo kwa ajili ya kujenga
mshikamano na kuepukana na kukaa kwenye magenge.
"Malengo ya mashindano haya kwa asilimia kubwa
yamefanikiwa sana, na ndio maana hata zawadi za washindi zilianza kutoka katika
hatua za makundi kila timu iliiyoongoza ilipata jezi seti moja na mpira na zile
za pili zilipata mipira," alisema.
"Pia kila timu iliyoshiriki nilitoa mpira mmoja kwa
ajili yao kujiandaa, na katika hatua ya robo fainali kila timu pia ilipata
zawadi ili kuongeza morali ya mashindano, aliongeza.
Pia alisema lengo lingine lilikuwa ni kukamilisha ilani ya
chama chao ambacho kinaichukulia michezo kama ni ajira tosha kwa vijana ambayo
inaweza kuwakomboa kiuchumi.
Wakati huo huo Malawandu alisema mashindano hao kuanzia sasa
yatakuwa ni endelevu na ana mpango wa kuyafanya kila mwaka huku pia kwa sasa
akijipanga na kamati yake kwa ajili ya kuanzisha na wanawake.
Wadau wa Cheza Kidansi wakutana kuujadili muziki wa dansi
JANA kulikuwa na kikao cha wadau wa muziki wa dansi hapa
nchini kilichoendeshwa na kundi la Cheza Kidansi, linaloendeshwa chini ya mlezi
wao Yusuph Mhandeni, maarufu kama Yusuphed Mhandeni, ambaye pia ni Mchumi wa
Kata ya Makumbusho wa Chama Cha Mapinduzi CCM.
Wadau wa Cheza Kidansi wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kikao cha kujadili maendeleo ya muziki wa dansi nchini. Wa pili kutoka kushoto ni Yusuphed Mhandeni, ambaye ndio mlezi wa kundi hilo.
Katika kikao hicho, mengi yalijadiliwa yanayohusu maendeleo
ya muziki wa dansi hapa nchini kwa ajili ya kuuwezesha muziki huo kufikia
malengo.
Subscribe to:
Posts (Atom)