Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WASANII wane wa muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo
Fleva, Chid Benz, Amini, Synag na Tunda Man, wamepangwa kufanya shoo ya wiki nne
za zawadi inayoandaliwa na Extra Bongo, itakayofanyika Ijumaa, katika Ukumbi wa
Ikweta Grill, Temeke.
Kufanyika kwa onyesho hilo ni maalum kwa ajili ya kutoa
burudani kwa wapenzi wa muziki nchini, huku ikitoa zawadi mbalimbali, ikiwamo
150,000 na elfu 50,000, katika shoo iliyofanyika Meeda wiki iliyopita.
Akizungumza na Handeni Kwetu, Mkurugenzi wa bendi hiyo, Ally Choki, alisema kuwaita wasanii hao wa
kizazi kipya ni kuongeza hamu ya utoaji wa burudani kwa wapenzi wao.
Alisema kila kitu kinaendelea vizuri kwa ajili ya wanamuziki
wa bendi yake na wasanii hao wa Bongo Fleva kufanya mambo katika shoo hiyo.
“Tunafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa burudani ya
wiki nne za zawadi inakuwa ya aina yake na watu wapate raha wanapokuwa
ukumbini.
“Naamini kila kitu kitakuwa sawa, maana waimbaji hao
tumeshafikia muafaka na wamekubali kuja kutoa burudani katika tukio hilo la
Ijumaa,” alisema.
Onyesho hilo la Ijumaa atakosena msanii Linah, ambaye nafasi
yake imejazwa na msanii Chid Benz, ambaye naye amejigamba kufanya makubwa
katika shoo hiyo.
No comments:
Post a Comment