Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni
HANDENI ni wilaya kongwe inayounganisha Mkoa wa
Tanga. Uwepo wa wilaya hii umesababisha kuzaliwa kwa wilaya nyingine ya Kilindi.
Licha ya kugawanywa na serikali bado Handeni inaendelea kuwa wilaya kongwe na
kubwa.
Mkuu wa wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani
Handeni ni kati ya wilaya saba za Mkoa wa Tanga katika Tanzania. Imepakana na
Wilaya ya Kilindi upande wa magharibi, Wilaya ya Korogwe na Mkoa wa Kilimanjaro
upande wa kaskazini, Wilaya ya Pangani upande wa mashariki na Mkoa wa Pwani kwa
kusini.
Kulingana na sensa ya watu na makazi ya
Mwaka 2002 Wilaya ilikuwa na watu 248,633 kwa kiwango cha ukuaji wa asilimia
3.3% katika kaya 52,240 ambayo ni sawa na wastani wa watu 4.66 kwa kaya.
Wastani wa msongamano wa watu ni watu 30 kwa kilometa ya mraba.
Msongamano mkubwa upo kando kando ya
barabara kuu na mijini. Idadi ya watu huongezeka kwa wastani wa asilimia 3.3%
kwa mwaka, kwahiyo idadi ya watu mwaka 2010 ilikadiriwa kuwa 322,375 na mwaka
2013 ilikadiriwa kuwa na watu 355,355.
Juhudi nyingine zinafanyika
kuigawa tena wilaya hii sambamba na kufanikisha kuifanya kuwa mkoa mpya, ukitoa
wilaya za Kilindi, Korogwe na ile Halmashauri ya Kabuku ambapo juhudi na
maarifa zinaelekezwa huko.
Ni vyema sasa mkakati huo ukawa kijiji kwa kijiji, kata kwa kata,
tarafa kwa tarafa na wilaya yote ya Handeni, ili kuleta dira mpya kimaendeleo. Tarafa
hizo ni pamoja na Kwamsisi, Mkumburu, Mzundu, Sindeni,
Mazingara, Magamba na Chanika, wakati kata ni pamoja na Vibaoni,
Kideleko, Chanika, Kwankonje, Kwachaga, Kwaluguru, Kang'ata, Mkata, Mazingara,
Kiva, Kwamatuku, Misima, Sindeni, Kabuku, Kabuku ndani, Komkonga, Ndolwa,
Mgambo, Segera, Kwedizinga, Kwamgwe, Kwamsisi na Kwasunga.
Vijiji vinavyopatikana katika wilaya ya Handeni ni pamoja na Kwabaya, Konje , Konje, Kwamasaka na Vibaoni, Msasa, Kideleko, Bangu, Kwamngumi, Kwakivesa, Mdoe, Malezi, Kwenjugo, Mashariki, Kilimilang'ombe,
Kwenjugo
magharibi, Kwediyamba, Kwedizando, Kwenkambala, Nkumba, Kwamsundi, Kwamsangazi,
Kwankonje, Kwamkunga, Kwachaga, Mkomba, Tuliani, Mpalagwe,
Magamba,
Kibindu, Muungano B, Kwamagome, Msaje, Kwaluwala, Madebe, Nyasa, Gole,
Kang'ata, Kilimamzinga, Manga.
Vingine ni Kwenkwale,
Kwang'ahu, Kitumbi, Mkata Mashariki, Mkata Magharibi, Suwa, Amani, Mazingara, Kweditilibe,
Kwedibangala, Zavuza, Kweingoma,
Komsala, Nkale, Kwamatuku, Mzeri, Misima, Kibaya, Mbagwi, Msomela, Sindeni,
Kweisasu, Kwamkono, Komfungo, Mbuyuni, Bongi, Kabuku Kaskazini, Kabuku Nje,
Kwedibago.
Vijiji vingine
ni pamoja na Msilwa, Kwedikwazu Mashariki, Kwedikwazu Magharibi, Kabuku Ndani, Majani Mapana, Kabuku Mjini,
Chogo, Komkonga, Kwamachalima, Hoza, Mumbwi, Tuliani/Kabuku, Kwamnele, Chanika Kofi, Komkole 'B",
Luiye, Kwamwenda, Komdudu Mzundu, Seza Kofi, Gendagenda, Kwedihwahwala,
Komsanga, Kwabojo, Jitengeni, Mandera,
Masatu, Mailikumi, Segera, Chang'ombe, Michungwani, Taula,
Kwedizinga, Ugweno, Bondo,
Kwamgwe, Kwadoya, Ngojoro, Mkalamo, Pozo, Kwedikabu, Kwamsisi, Kwandugwa, Kwasunga, Kwanyanje na vinginevyo,
No comments:
Post a Comment