Ramadhani Shauri akipima uzito
Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BONDIA
wa ngumi za kulipwa na Bingwa wa IBF Intercontinental, Ramadhani Shauri,
anatarajiwa kupanda ulingoni Jumapili ya kesho kwa ajili ya kuzipiga na Said
Njechele wa Iringa, katika pambano la kirafiki la raundi nane katika Ukumbi wa
D.I.D Hall, uliopo Mabibo Mwisho, jijini Dar es Salaam.
Ramadhani Shauri kulia akipimana ubavu na Said Njechele
Mratibu
wa pambano hilo Charles Christopher,
amesema kuwa maaandalizi ya pambano hilo yamekamilika na mabondia wote
wapo katika hali nzuri ya ushindani, sanjari na kupima uzito.
Ambapo
pia kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi na mabondia watakaosindikiza
pia wamepima chini ya usimamizi wa katibu mkuu wa TPBO bw Ibrahim kamwe na
docta john wapo sawa kwa kupambana.
Mabondia
watakaocheza utangulizi ni Hamis Mohamed na Haruna Mnyalukolo, Pendeza Shomari
akipizipiga na Martin Richard, wakati Mbaruku Nassoro akipanda ulingoni dhidi
ya Karimu Respect, huku Doto Mustafa naye akipigana na Shomari Miurundi, bila
kusahau Issa Omari, akipigana na Juma Kashinde.
Katibu
Mkuu wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Kamwe, amethibisha kuwa kanuni na
taratibu za ngumi za kulipwa zimefuatwa na mabondia wapo katika hali nzuri ya
kupigana kwenye pambano hilo.
No comments:
Post a Comment