Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), limebandika majina ya wagombea wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi za Shirikisho lao kwa ajili ya kuwapa fursa wadau wa michezo wawaone na kuweka pingamizi wanapoona wanafaa kwa kuafuata masharti ya kanuni za uchaguzi.
Michael Wambura, mgombea Makamu wa Rais TFF
Majina hayo yamebandikwa kwa kufuata kanuni za uchaguzi za TFF kwa mujibu wa ibara ya 11 (1), (2) na (3), ikiwa ni njia ya kuwafanya wanamichezo wengine kutoa fursa kwa wale wote wenye pingamizi kwa watu wasiopenda wagombee katika Uchaguzi huo wa TFF.
Athumani Nyamlani, kulia, mgombea urais TFF
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa katika vyombo vya sambamba na Handeni Kwetu Blog, ilisema pingamizi lolote litakalomuhusu mgombea yoyote, lazima liwe kwa maandishi.
Mbali na
maandishi hayo, lieleze kwa uwazi sababu za pingamizi, liambatanishwe na
ushahidi wa pingamizi, liwe na jina kamili la mtoa pingamizi, anwani ya kudumu
na saini ya mwanamichezo huyo.
Wagombea
waliobandikwa majina yao kwa ajili ya kuwekewa pingamizi ni pamoja na nafasi ya
urais kwa Athumani Jumanne Nyamlani, Jamal Emily Malinzi na Omary Mussa
Nkwarulo, huku nafasi ya Makamu wa Rais wakitajwa Michael Richard Wambura, Ramadhan
Omar Nassib, Wallace Karia.
Wajumbe
waliopitishwa ni Abdallah Hussein Mussa, Kalilo Samson, Salum Hamis Umande
Chama, Jumbe Oddessa Magati, Mugisha Galibona, Samuel Nyala, Vedastus F.K
Lufano, Epaphra Swai, Mbasha Matutu, Charles Mugondo, Elley Simon Mbise, Omary
Walii Ali.
Wengine
ni Ahmed Idd Mgoyi, Yusuf Hamis Kitumbo, Ayubu Nyaulingo, Blassy Mghube Kiondo,
Nazarius A.M Kilungeja, Seleman Bandiho Kameya, David Samson Lugenge, Eliud
Peter Mvella, John Exavery M. Kiteve, Lusekelo E. Mwanjala, James Patrick
Mhagama, Stanley W. D Lugenge, Athuman Kingome Kambi, Francis Kumba Ndulane, Zafarani Mzee Damoder na Hussein
Zuberi Mwamba.
No comments:
Post a Comment