Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Said Mswaga, amesema kuwa kupatikana
kwa nyati mweupe wa ajabu na pekee duniani katika hifadhi ya Ngorongoro,
imekuwa ni chachu na kichocheo cha pekee kwake katika mpango mkakati wake wa
kuitangaza Hifadhi ya Ngorongoro kitaifa na kimataifa, ambapo kwa kuanzia
ameamua kuanza kampeni hiyo kupitia mashindano ya dunia anayokwenda kushiriki
ya Miss Tourism World 2013, ambayo mwaka huu yanafanyikia nchini Equatorial
Guinea Octoba 12, 2013.
Kupatikana kwa Nyati huyo wa ajabu Mweupe, ambaye hapatikani sehemu
nyingine yoyote Duniani, wakati huu ambao anakwenda katika mashindano hayo ya
Dunia, imekuwa ni fulsa ya pekee kwa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
na kwake , kuithibitishia dunia kuwa Ngorongoro Cater ni Ajabu la Asili la
Dunia Barani Afrika.
Ambapo sasa Ngorongoro Crater pamoja na maajabu ya
bonde lenyewe la kreta ya Ngorongoro, pia kuna maajabu ya Nyati Mweupe, Unyayo
wa Binadamu wa kale zaidi Duniani, Mchanga wa ajabu unao hama kila mwaka kwa
umbo la Nusu mwezi, Mlima wenye Volkano Hai wa Oldonyo Lengai, lakini pia
ushirikiano wa kuishi bila kudhuriana wa binadamu na Wanyama katika hifadhi
hiyo na upatikanaji wa jamii karibu zote za Wanyama wakubwa (BIG FIVE) na adimu
duniani wakiwemo Faru Weusi, Duma, Mbwa Mwitu, Kaka kuona n.k.