Dogo Rama katika pozi
Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWANAMUZIKI
wa bendi ya The African Stars, Dogo Rama, jioni ya jana aliumbuka makao makuu
ya bendi yao, baada ya kushindwa kuiona printer iliyokuwa juu ya meza.
Meneja wa Twanga Pepeta, Hassan Rehani
Hatua hiyo, alisababisha kicheko kutoka kwa meneja wake,
Hassan Rehani, aliyeanza kumshangaa Dogo Rama.
Hata
hivyo, kitendo cha kuchekwa katika ofisi hiyo, kilimuumiza na kuanza kuhoji
sababu ya kicheko cha bosi wake, ambaye pia hakuwa peke yake ofisini kwake.
Dogo Rama
alijitetea, “sio kweli kwamba siijui mashine ya (Printer) kama ulivyoniagiza,
ila sijaiona haraka karatasi uliyoniambia nikupe, sasa nashangaa mnacheka.
“Labda
mcheke kwa mengine lakini sio hili la printer maana itakuwa ajabu kama sitaijua
kitu kama hicho ambacho kila mtu anakijua,” alisema Dogo Rama.
Hata
hivyo, kushindwa kujua kitu sio jambo baya kwa mtu yoyote katika Dunia ya leo
inayotoa vifaa mbalimbali. Dogo Rama ni miongoni mwa vijana imara wanaoipaisha
bendi ya Twanga Pepeta, akijulikana pia kwa jina la Kilomita 10,000.
No comments:
Post a Comment