Mshambuliaji wa Simba, Haruna Moshi Boban
Na Kambi Mbwana, Dar es
Salaam
HUKU mzunguko wa pili
wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza Jumamosi
(Januari 22 mwaka huu), mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
umesogezwa mbele kwa wiki moja ambapo sasa utaanza Februari 2 mwaka huu.
Kikosi cha Yanga mazoezini
Uamuzi wa VPL kuendelea
Januari 26 mwaka huu ulifikiwa katika kikao cha Kamati ya Ligi ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu za ligi hiyo kilichofanyika jana
(Januari 21 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Shirikisho la
Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema uamuzi huo umefikiwa huku yakiwapo
masharti kadhaa kutokana na uamuzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukamata
Sh. milioni 157 kwenye akaunti za TFF, fedha zilizotoka kwa mdhamini wa VPL
(Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom) kwa ajili ya timu zinazoshiriki ligi
hiyo.
Masharti hayo
yatawasilishwa na Kamati ya Ligi kwa maandishi kwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), nakala kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo. Awali klabu kupitia Kamati ya Ligi zilisisitiza zisingecheza ligi
hadi fedha hizo zitakaporejeshwa.
Kwa upande wa FDL
itaanza bila timu ya Small Kids ya Rukwa ambayo imeshushwa daraja kwa mujibu wa
kanuni baada ya kushindwa kucheza mechi mbili katika mzunguko wa kwanza.
Kwa mujibu wa kanuni za
ligi hiyo, matokeo yote ya mechi ambazo Small Kids ilicheza katika mzunguko huo
wa kwanza yamefutwa.
Kamati ya Sheria,
Maadili na Hadhi za Wachezaji iliyokutana Januari 19 mwaka huu chini ya
Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa imeliondoa shauri lililokuwa mbele yake dhidi ya
klabu ya Simba lililowasilishwa na wachezaji Pascal Ochieng na Daniel Akuffo
baada ya pande hizo kufikia makubaliano.
Wachezaji hao kutoka
Kenya na Uganda waliwasilisha malalamiko mbele ya kamati wakipinga kukatizwa
mikataba yao bila kulipwa stahili zao. Hata hivyo, pande zimefikia makubaliano
ya kuvunja mikataba nje ya kamati, na wachezaji hao kulipwa stahili zao.
Pia Simba imekiri
kudaiwa na wachezaji Shija Mkina, Swalehe Kabali, Victor Costa na Rajab Isiaka
na kuahidi kuwalipa wachezaji hao wakati Coastal Union na mchezaji wake Mohamed
Issa wamefikia makubaliano ya malipo, hivyo kuvunja mkataba kati ya pande hizo
mbili.
Katikahatua nyingine, Kamati
ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ilikutana Januari 19 mwaka huu kupitia
maombi ya usajili wa dirisha dogo kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo kipa Shabani Kado ameidhinishwa kuidakia
timu ya Coastal Union ya Tanga.
Wachezaji wengine
waliodhinishwa kwenye dirisha dogo na klabu zao kwenye mabano ni Humphrey
Mieno, Brian Umony, Jockins Atudo, David Mwantika, Abdallah Seif, Malika Ndeule
na Uhuru Selemani- kwa mkopo (Azam), Juma Mdindi, Njaidi Mohamed na Mahmoud
Mbulu (Ruvu Shooting), Mohamed kayi na Emmanuel Gabriel (Tanzania Prisons).
Nurdin Selemani, Shaibu
Nayopa, Hamidu Hassan, Paul Malipesa, Josephat Moses, Muharami Mnyangamala,
Majaliwa Mbaga na Alphonce Peter (Oljoro JKT), Shukuru Kassim, Chacha Marwa,
Salum Machaku, Mzamiru Said, Victor Bundala, Delta Thomas, Edward Mzeru na
Tizzo Chomba (Polisi Morogoro), Edmund Kashamila na Julius Mrope (Kagera Sugar).
Rajab Mohamed, Zakayo
Joseph, Baraka Anthony na Mussa Chambo (Mtibwa Sugar), Zahoro Pazi- kwa mkopo,
Emmanuel Linjechele, Kisimba Luambano na Nashon Naftali (JKT Ruvu), Moaka
Shabani, Ismail Mkaima na Damas Milanzi (Mgambo Shooting), Donald Obimma,
Exavery Muhollery, Mohamed Hussein na Ulugbe Odia (Toto Africans).
Obadi Mungusa, Juma
Seif, Yusuf Mgwao, Ibrahim Job- kwa mkopo, Shamte Ally- kwa mkopo, Buya
Jamwaka, Takang Valentine, Nurdin Mussa, Salvatory Jackson, Mohamed Athuman,
Athuman Kajembe na Jarufu Kizombi (African Lyon), Mussa Mudde na Abel Dhaila
(Simba).
Rashid Simba, Zuberi
Hamisi, Shaongwe Ramadhan, Castory Mumbara, Tinashe Machemedze na Shabani Kado
(Coastal Union). Mchezaji Martin Mlolere aliyeombewa usajili Mgambo
Shooting kutoka Majimaji amekataliwa kwa vile taratibu za uhamisho
hazijakamilika, hivyo anabaki kwenye timu yake ya Majimaji.
No comments:
Post a Comment