Elizabeth Michael, Lulu
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII nyota wa filamu hapa
nchini, Elizabeth Michael, maarufu kama (Lulu), alishindwa kurudi uraiani, licha ya kuachiwa kwa dhamana, kutokana na kukosekana kwa watu wawili wa kutia sahihi ya kutoka kwa msanii, ingawa Jaji Zainabu Muruke wa Mahakama Kuu, alitangaza kutoa dhamana ya mwanadada huyo.
Lulu alifikishwa mahakamani akituhumiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba, ambaye hata hivyo baadaye alibadilishiwa kesi na kushitakiwa kwa kuua bila kukusudia.
Lulu alifikishwa mahakamani akituhumiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba, ambaye hata hivyo baadaye alibadilishiwa kesi na kushitakiwa kwa kuua bila kukusudia.
Masharti ya dhamana yalikuwa ni kuacha Hati ya Kusafiria Mahakamani, kuripoti Mahakamani kila
tarehe mosi, pamoja na wadhamini wawili waliotoa milioni 20 mmoja.
Kwa wiki kadhaa sasa, baadhi ya
watu wamekuwa wakisikika wakiomba dua njema kwa msanii huyo ili aweze kuachiwa
kwa dhamana na kufuatilia kesi yake akiwa nje na familia yake.
Lulu aliwasilisha mahakamani
hapo maombi ya dhamana, kupitia kwa jopo la mawakili wake, linaloongozwa na
Wakili Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala, Fulgence Masawe wa Kituo cha Msaada
wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Awali, maombi hayo ya dhamana
yaliwasilishwa mahakamani hapo kwa hati ya dharura na kusikilizwa na jaji
Zainabu Muruke.
Mara baada ya tukio la mauaji
ya Kanumba kutokea, kesi ya msanii huyo ilifunguliwa katika Mahakama ya Kisutu
ili kukamilisha hatua za awali, hasa masuala yote ya kisheria, upelelezi na
kushtakiwa kwa mauaji ya kuua bila kukusudia kwa kupitia Kifungi cha 196.
Kesi ya Lulu yenye namba 125,
jalada lake lilifungwa na kuhamishiwa Mahakama Kuu kwa kuwa ndiyo yenye uwezo wa kusikiliza kesi za
mauaji.
Mara baada ya kufika mahakamani
hapa leo asubuhi, dalili njema za kuachiwa kwa msanii zilianza kujitokeza hasa
baada ya dhamana yake kuwa wazi, ikiwa ni kutokana na hoja zilizokuwa
zinajadiliwa mahakamani hapo.
Katika mitandao ya kijamii,
ikiwamo facebook, baadhi ya watu walionekana wakipost habari na picha
mbalimbali za msanii huyo zikionyesha dhahiri kumuombea mema ili atoke na
kuendelea na maisha yake wakati kesi hiyo inaendelea.
Lulu ni miongoni mwa wasanii wa
kike wenye mvuto mkubwa katika jamii, huku uwezo wake na umahiri wake wa
uigizaji ukiacha watu midomo wazi.
Umaarufu wa Lulu ulitokea tangu
mdogo akiigiza katika kundi la Kaole Sanaa Group, akicheza kama mt0to hadi
kufikia kuwa msichana na mwenye mvuto miongoni mwa mabinti wa filamu Tanzania.
Bila shaka habari za kuachiwa
kwa dhamana kwa msanii huyo zitakuwa njema kwa kwa mashabiki na
wadau wote wa filamu Tanzania, hasa wale waliopiga simu Handeni Kwetu kutaka ukweli wa kuachiwa kwa msanii.
No comments:
Post a Comment