https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, May 16, 2016

Issa Michuzi atoa shukrani kwa kufarijiwa msiba wa mtoto wake

Familia ya Ankal Muhidin Issa Michuzi  inapenda kutoa  shukrani nyingi sana sana kwa ndugu, jamaa, majirani, marafiki na wafanyakazi wenzie kwa kujitoa kwa hali na mali katika wakati huu mgumu wa msiba wa mawanae Maggid (pichani) aliyefariki huko Durban, Afrika Kusini Jumapili ya wiki iliyopita  na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam juzi Jumamosi.
Ni vigumu mno kumshukuru mtu mmoja mmoja kutokana na wingi wenu na kwa jinsi kila mmoja wenu alivyojitoa na kuonesha upendo wa dhati kabla na baada ya mazishi. Tunaweza kujaza kurasa 200 kama hizi na tusiwe tumehitimisha robo tu ya shukrani zetu kwa kila mmoja wenu. Hivyo tunaomba radhi kwa yoyote ambaye hatutomtaja, kwani wafadhili wetu nyie mko wengi mno.
Pamoja  na hayo shukrani za kipekee ziwaendee Mheshimiwa Rais  Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mama Janeth Magufuli na familia yao yote, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt.  Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete na familia yao yote,  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake yote, Rais Mstafu wa awamu ya Tatu Mzee Benjamin William Mkapa na Mama Anna Mkapa na  familia yao yote, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Familia yake yote, Katibu Mkuu Kiongozi  Mhandisi Allan Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe.

Maisha Shamba wakusudia kupanda miti milioni 50,000,000

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WADAU wa ardhi, mazingira na mambo ya misitu wanaojulikana kama Maisha Shamba Group wameweka adhma ya kupanda miti milioni 50,000,000 ifikapo mwaka 2020, ikiwa ni mipango yao ya kutunza mazingira na kujikwamua kiuchumi kwa kupitia sekta ya misitu nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, akizungumza jambo katika mkutano wa wanachama wa Maisha Shamba Group wanaojihusisha na mambo ya misitu na mazingira mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.


Hayo yamesemwa na kiongozi mkuu wa group hilo, Asifiwe Malila, alipokuwa akizungumza na wanachama wake katika mkutano wao wa mwaka, huku mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, mwishoni mwa wiki, katika Ukumbi wa Shule ya Sheria Tanzania, jijini Dar es Salaam.

Mdau wa mambo ya ardhi na misitu, Ally Abdallah, akisikiliza kwa makini hutuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, hayupo pichani katika mkutano wa wadau wa misitu wanaojulikana kama Maisha Shamba Group.


Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, aliwapongeza wadau hao wa mambo ya misitu, akiwataka waendelee kubuni mambo yanayoweza kuwakwamua na kuisaidia nchi katika kutunza mazingira kwa kupitia sekta ya misitu.

Sunday, May 15, 2016

Zahir Zoro alitikisa jiji la Mwanza

Mwanamuziki wa siku nyingi nchini kwenye muziki wa dansi na rumba, Zahir Ally Zoro (pichani) usiku wa kuamkia leo (jumamosi mei 14,2014) amewaburudisha wakazi wa Jiji la Mwanza baada ya kufanya show kali katika Ukumbi wa Kilimanjaro Hotel, Nyegezi.

Ilikuwa ni show yake ya kwanza kwa mwaka huu 2016 ambapo wapenzi wa muziki wa dansi na rumba walivutiwa na burudani iliyotolewa na Zoro hasa baada ya kuimba live wimbo uitwao "Beatrice" ambao ni wimbo uliofanya vizuri sana wakati anauachia akiwa na band yake ya Mass Media.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...