Rais wa TFF, Leodgar Tenga
Na Kambi Mbwana, Dar es
Salaam
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodgar Tenga amesema hatagombea
tena wadhifa huo katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 24 mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi
wa Habari kwenye ofisi za TFF leo, Rais Tenga amesema wakati anaingia kwenye
uongozi mwaka 2004 ajenda ilikuwa na kuijenga TFF kama taasisi kwa kuweka
mifumo ya uendeshaji ikiwemo kutengeneza katiba na kanuni, jambo ambalo
limefanyika.
“Wajumbe wamekuwa
wakiniuliza Rais vipi? Mimi hapana. Nilishafika pale pa kufika. Tulipoanza
wakati ule ilikuwa ni kujenga taasisi. Na kazi hiyo tumeifanya. Tulipoingia
mwaka 2004 hiyo ndiyo ilikuwa ajenda,” amesema Rais Tenga.
Alisema walitengeneza
Katiba, vyombo huru vya kufanya uamuzi, kuongeza wigo wa wapiga kura ambapo
hivi sasa kwenye mpira wa miguu hakuwezi kutokea migogoro, hata ikitokea kuna
mfumo wa kuidhibiti.
Ametoa mwito kwa wadau
kujitokeza kugombea uongozi TFF, kwani baada ya kujenga taasisi ajenda
iliyobaki ni mpira wa miguu wenyewe ikiwemo nini kifanyika ili mpira uchezwe
katika maeneo mbalimbali.
“Tumeshatengeza mfumo,
sasa ni kuangalia jinsi ya kuendeleza mpira. Changamoto ni tufanye nini ili
mpira uendelee. Tunataka watu wengine wabebe hiyo ajenda ili tuangalie
tunakwendaje mbele,” amesema.
Pia amesema ushirikiano
ambao amepata kwa wapenzi na wadau wa mpira wa miguu ni wa ajabu. Vilevile
ameishukuru vyombo vya habari, Serikali, klabu, wadhamini na wafadhili kwa
mchango wao katika uendeshaji wa mpira wa miguu nchini.
No comments:
Post a Comment