https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, March 31, 2016

Mbunge Mkuranga asaka uwezeshwaji wa wananchi wake



Mkurugenzi wa Baraza la Uwezeshaji la Taifa, Bengi Issa mwenye kilemba, akizungumza kwenye kikao cha pamoja na Mbunge wa Mkuranga, Mheshimiwa Abdallah Ulega kushoto kwake kwa ajili ya kuangalia namna ya kushirikiana naye kuwasaidia na kuwawezesha wananchi wa Mkuranga.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga, wilayani Mkuranga, mkoani Pwani, Abdallah Ulega, jana amefanya kikao na Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Taifa (NEEC), Bengi Issa, kwa ajili ya kutafuta fursa ya kuwawezesha wananchi wilayani humo.
Mbunge wa Mkuranga, Mheshimiwa Abdallah Ulega, akizungumza jambo katika kikao cha pamoja na Mkurugenzi wa Baraza la Uwezeshaji la Taifa (NEEC), Bengi Issa, hayupo pichani.
Kikao hicho pia kilihusisha Mkurugenzi wa Uwezeshaji, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuranga, ambapo pamoja na mambo mengine, kilijadili namna ya kusaidia vikundi vilivyosajiliwa 285, vikundi vya vicoba 109, ufugaji wa nyuki, vikundi vya wanawake, vijana na waendesha bodaboda.
Akizungumza baada ya kikao hicho kumalizika, Ulega aliyewahi pia kuwa Mkuu wa wilaya Kilwa, alisema kwamba lengo ni kuona wanananchi wa Mkuranga wanapiga hatua kutoka kwenye hali ya ukata na kufikia kiwango kizuri, sanjari na kufanikisha maendeleo kwa wananchi wote.

Wednesday, March 30, 2016

Izzo Bizness akamua balaa jijini Mbeya

Msanii Emmanuel Simwinga maarufu “ Izzo Bizness “ akitumbuiza kwenye tamasha la pasaka la home sweet home lililodhaminiwa Tigo jijini Mbeya jumapili iliyopita.

Hati za viwanja vya Bayport zatolewa kwa mtindo wa aina yake

Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto akimpatia hati ya kiwanja cha Vikuruti, mteja wao Ibrahim Yusuph Ismail, nyumbani kwao Kariakoo jijini Dar es Salaam, leo mchana. Kwa wiki hii tu Bayport imeamua kuwapelekea hati za viwanja wateja wao katika maeneo yao ya makazi na maofisini kwao. 


Na Mwandishi Wetu, Dar esSalaam
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, wateja wa Bayport waliojipatia viwanja vya Bayport vilivyopo Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha mkoani Pwani wameendelea kupewa hati zao, huku safari hii wakipewa hati kwenye maeneo wanayopatikana ikiwamo majumbani na maofisini. Hatua za kuwapelekea hati hizo wateja wao ni kitendo cha kuthamini uwapo wa wateja wao wanaoendelea kuiamini Bayport Financial Services katika bidhaa zake za mikopo ya fedha, bila kusahau huduma ya mikopo ya viwanja vyenye hati inayotolewa na taasisi hiyo, kwa kushirikiana na wadau wa ardhi walioingia mikataba na Halmashauri unapopatikana mradi wa viwanja kwa ajili ya watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi, wajasiriamali na Watanzania kwa ujumla.
Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabiti Mndeme, kushoto akizungumza jambo wakati anamkabidhi hati yake ya kiwanja mteja wao Neema Jameson Nawita, jijini Dar es Salaam leo mchana.

Akizungumza wakati wa kutoa hati kwa wateja watatu leo jijini Dares Salaam, Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema jambo kubwa la miradi ya viwanja kwenye taasisi yao ni kuona weteja wao wanapata hati ili kuweka ubora wa huduma zao, ikiwa ni sehemu muafaka ya kufuta migogoro ya ardhi kwa kununua viwanja vyenye hati. Alisema kwa wiki mbili mfululizo wamekuwa wakiendelea kutoa hati kwa wateja wao, huku kwa wiki hii tu, taasisi hiyo ikifika mbali kwa kujenga imani na kwenda sambamba na wateja hao, wakaona umuhimu wa kuwathamini na kuwataka wachague maeneo wanayoona wanaweza kupokea hati zao, iwe ni maofisini kwao au kwenye maeneo ya makazi.
Mteja wa Bayport na mkazi wa jiji la Dar es Salaam, Neema Jameson Nawita, kulia akipokea hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, aliyokabidhiwa leo na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services.

Tuesday, March 29, 2016

Kamati ya Bunge yaomba uingizaji sukari uruhusiwe

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji, Dk. Mary Nagu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu Serikali kutoa mapema vibali vya uingizwaji wa sukari kutoka nje ya nchi ili kuweza kuziba upungufu ya bidhaa hiyo nchini. Kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa.

Na Dotto Mwaibale
KAMATI ya Bunge ya Kudumu ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji, imeitaka Serikali kutoa mapema vibali vya uingizwaji wa sukari kutoka nje ya nchi ili kuweza kuziba upungufu ya bidhaa hiyo nchini.

Pia imeitaka Serikali kudhibiti bandari bubu na njia za panya ambazo huingiza sukari kinyume cha sheria na kuua viwanda vilivyopo na kuifanya Tanzania kununua sukari kutoka nje ya nchi na kuua uchumi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk.Mary Nagu alisema kwa sasa upatikanaji wa sukari ni mdogo ukilinganisha na mahitaji ambapo kunamapungufu wa tani 80,000 hadi 100,000.
 Mjumbe wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa akizungumza katika mkutano huo.

Milioni 37 zatengwa kukarabati barabara ya Kata ya Panzuo/Mkuranga

Na  Mwandishi Wetu, Mkuranga
JUMLA ya Sh Milioni 37 zimetangwa kwa ajili ya kukarabati barabara ya Mbogo na Mbezi Muungwana, inayopita katika vijiji kadhaa vya Kata ya Panzuo, wilaya Mkuranga, mkoani Pwani kwa ajili ya kupunguza adha za ubovu wa barabara wanazokutana nazo wananchi wa maeneo hayo hali inayopelekea wakati mwingine akina mama kujifungulia njiani.
Mwendesha bodaboda Ramadhan Rajab akijaribu kupita katika barabara mbovu inayotokea Kimanzichana kuelekea vijiji vya Mnyonzole na Kibesa, Kata ya Panzuo, wilayani Mkuranga, mkoani Pwani.

Mapema mwezi uliopita baadhi ya wananchi wakiwamo akina mama walizungumza kwa uchungu juu ya ukosefu wa barabara katika maeneo hayo, jambo linalowanyima raha na ukosefu wa mbinu za kujikwamua kiuchumi kwa kukosekana barabara inayopitika kwa wakati.

Akizungumza juu ya ukosefu wa barabara na mipango yao, diwani wa Kata ya Panzuo, wilaya Mkuranga, mkoani Pwani, Juma Magaila, alisema kwamba kiasi hicho cha pesa kitaanzia kwanza kuweka kifusi katika maeneo mbalimbali ili wananchi wae ndelee na majukumu yao kwa kuhakikisha kwamba suala hilo la barabara mbovu linashughulikiwa.

Alisema ni kweli wananchi katika maeneo hayo wamekuwa wakiishi kwa mashaka hususan mvua zinapoanza kunyesha, ila tayari fedha zimetangwa kwa ajili ya kuanza ukarabati wa barabara hiyo inayotumiwa na wananchi wengi wilayani Mkuranga.

Friday, March 25, 2016

Benki ya Maendeleo PLC na kuorodheshwa kwenye soko la hisa

Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji, Mwenyekiti wa Maendeleo Benki, Amulike Ngeliama (kushoto) na Mkurugenzi wa Tafiti, Sera na Mipango wa(CMSA) Nicodemus Mukama wakifuatilia jambo katika hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji akipiga kengele kuashiria uorodheshwaji rasmi wa Maendeleo Benki katika soko la hisa DSE jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Maendeleo Benki, Amulike Ngeliama na Mkurugenzi wa Capital Markets na Securities Authoriy (CMSA) Nicodemus Mukama 
Emmanuel Nyalali, Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji DSE akizungumza katika hafla hiyo. 
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji akiongea wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa Maendeleo Benki katika soko la hisa DSE 
Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Benki, Ibrahim Mwangalaba akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisah Mwenyekiti wa Benki hiyo kuzungumza na washiriki wa hafla hiyo. 

Bank PLC ni benki iliyoanzishwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani na inamilikiwa na Wananchi mbalimbali kwa njia ya HISA bila kujali, kabila, itikadi, dini wala rangi, kwani benki hii imesajiliwa na soko la hisa la Dar es Salaam (DSE), kupitia dirisha dogo yaani Enterprise Growth Market (EGM) na inaendeshwa kwa kufuata taratibu zote za BOT na Soko la Hisa la Dar es S alaam. 

Maendeleo Bank ilianza kutoa huduma za kibenki tarehe 9/9/2013 baada ya kupewa leseni na Benki Kuu ya Tanzania na tarehe 05/11/2013 ilisajiliwa rasmi katika soko la hisa la Dar es Salaam baada ya kukidhi vigezo vyote vilivyowekwa na mamlaka husika. Benki hii ilianza na mtaji wa shilingi bilioni 4.5 kutoka kwa wanahisa zaidi ya 3,000 wa rika na itikadi mbalimbali walionunua wakati wa mauzo ya awali (IPO) yaliyofanyika mwaka 2013.

Novemba 9/11/2015 benki ilipata kibali cha kuuza hisa stahili ambapo matarajio yake yalikuwa kupata shilingi bilioni 3.06 ambazo zitatumika kuimarisha shughuli za uendeshaji wa benki pamoja na kuongeza matawi. Katika zoezi la uuzaji wa hisa stahili benki imeweza kupata jumla ya shilingi bilioni 2.8 na kufikisha jumla ya mtaji wa benki kuwa shilingi bilioni 7.3.

Kusudi kubwa la kuanzishwa kwa Maendeleo Bank PLC ni kufikisha huduma za kibenki kwa wananchi wa kipato cha chini na cha kati kwani hao ndio walio wengi na upatikanaji wa huduma za kibenki kwao ni changamoto kubwa. Benki hii imepata mafanikio mengi tangia kuanzishwa kwake takribani miaka miwili iliyopita ambapo mpaka tarehe 31/12/2015, benki imefikisha wateja zaidi ya 12,000, amana zaidi ya shilingi bilioni 46.0, mali za benki zimefikia zaidi ya shilingi bilioni 55, imetoa mikopo zaidi ya shilini bilioni 21.0 na mwaka 2015 imepata faida ya takribani shilingi milioni 200.0 baada ya kodi. 

Benki hii inatoa huduma mbalimbali za ubunifu ambazo zinawalenga wananchi wa kada mbalimbali, zikiwemo: huduma za kibenki kwa njia ya simu, huduma za BIMA, ATM kupitia mtandao wa UMOJA Switch, akaunti mbalimbali zenye gharama rafiki, kutuma na kupokea pesa kutoka nje na ndani ya nchi, na kutoa mikopo ya aina mbalimbali, ikiwemo kwa wajasiliamali wadogo ambayo haina dhamana, yaani mikopo ya vikundi. 

Patashika ya mbio za uspika Visiwani Zanzibar zaanza rasmi

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
HEKAHEKA zimeanza Visiwani Zanzibar ambapo wagombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Wawakilishi wameanza kupigana vikumbo kuwania nafasi hiyo huku sura mpya za vijana wenye damu mbichi zikijitokeza kuchuana na mkongwe aliyechukua tena fomu ya kutetea nafasi yake Mhe Pandu Ameri Kificho, pichani.

Kificho ni Spika wa Bunge la Wawakilishi kwa muda wamiaka 25 sasa ambapo wanachama wa CCM Zanzibar tayari wameanza kutilia mashaka uamuazi wa spika huyo aliyechukua fomu za kugombea tena akitaka kuendelea na kuongoza kiti cha uspika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, jambo, inalozua maswali mengi yasiyo na majibu.

Wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti baadhi ya wanachama wa CCM Zanzibar, walitoa maoni yao juu ya sakata hilo na kusema kuwa Kificho hakustaili kuwania nafasi hiyo kwa kipindi kijacho bali alitakiwa kuiga mfano wa baadhi ya viogozi kama Spika Pius Msekwa na wengine walioamua kuachia ngazi kwa kujiuzuru madaraka na kuwaachia vijana wenye hali ya kuongoza ili kupata radha mpya katika Bunge hilo la Wawakilishi.

Naye mgombea, Mahamud Muhamed Mussa, alisema kuwa amejitokeza kuchukua fomu ili kuwania nafasi hiyo kutokana na uwezo alionao na Zaidi akijiandaa kuongoza kisasa Zaidi na kuleta mabadiliko ili Bunge la Wawakilishi liwe lakisasa na kuendana na kaulimbiu ya Mhe Rais wa Jamhuri ya 'Hapa kazi tu', alisemaMussa. 

''Kiukweli Kificho sasa anaelekea kuwaudhi Vijana ambao nao sasa ni muda wao wa kuongoza ili waweze kuchangia mengi waliyonayo ili kuendana na Kasi ya Rais wa awamu ya tano Mhe Dkt. Magufuli, Kificho amekalia kiti cha Spika Bunge la Wawakilishi kwa muda wa miaka 25 sasa ni kwa nini asipumzike na kuwaachia vijana wafanye kazi, sidhani kama bado ana jipya'', alisema Mwanachama mmoja wa CCM aliyejitambulisha kwa jina la Kijeshi.

Aidha Wanachama hao walikwenda mbali Zaidi kwa kukumbushia wakati wa zoezi la Kura ya maoni kuhusu Serikali mbili,ambapo Mhe. Kificho alionekana kwenda kinyume na msimamo wa Chama chake wa Serikali mbili huku yeye akionyesha msimamo wake Zaidi wa kudai Serikali tatu akidai 'eti' ni msimamo wa Baraza la Wawakilishi.

Waliojitokeza kuchukua Fomu za kuwania nafasi hiyo ni pamoja na Pandu Ameri Kificho, Mahamud Muhamed Mussa, Zuberi Ali Maulid, Muhamde Ali Amhed, Jajh Janeth, Sadifa Juma, David Mwakanjuki, Perera Silmg na Abdallah Wazisi, ambapo mchuano mkali unaonekana kuwa kwa ni kati ya Spika aliyemaliza muda wake akijaribu kutetea kiti chake, Pandu Ameri Kificho, Mahamud Muhamed Mussa na Jaji Janeth Sekihola.

Wagombea wote walifika kuchukua fomu jana Machi 23,2016  na kurejesha jana hiyo hiyo, zoezi la kupitiamajina na kufanya mchujo na kupata majina matatu lilifanyika jana na kuwapata hao wanaochuana.

Wednesday, March 23, 2016

Bayport yakabidhi hati za viwanja vya Vikuruti



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo imekabidhi hati za viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani kwa baadhi ya wateja waliomaliza kulipa mikopo yao tangu walipochukua mikopo hiyo yaa viwanja mapema mwaka jana. Baadhi ya wateja waliokabidhiwa hati hizo ni pamoja na Desidery Didas Kalimwenjuma wa Temeke na James Moses Lubinza wa Kimara jijini Dar es Salaam, huku hati za wateja wengine zikiwa zimekaamilika kwa ajili ya kukabidhiwa wateja hao ambao walikuwa miongoni mwa Watanzania waliochangamkia fursa ya mikopo ya viwanja vya Vikuruti, vilivyokuwa vinauzwa na Bayport kwa kushirikiana na Kampuni ya Property International Ltd.
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed (kushoto), akishuhudia bwana James Moses Lubinza akitia sahihi katika tukio la upewaji wa hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani  leo mchana, jijini Dar es Salaam. Lubinza alikuwa miongoni mwa Watanzania waliochangamkia fursa ya mikopo ya viwanja vya Bayport. Huduma hizo za viwanja mwaka huu zinaendelea kwa kuanzishwa miradi ya Bagamoyo, Kigaamboni, Chalinze, Kibaha na Kilwa vikuhusisha watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali. Picha kwa hisani ya Bayport Financial Services.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services Ngula Cheyo katikati akikabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti kwa mteja wao James Moses Lubinza leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Sheria wa Bayport, Mrisho Mohamed.
Akizungumza leo mchana katika makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, Ngula Cheyo, alisema ni furaha yao kubwa kuanza kutoa hati ya viwanja vilivyouzwa kwa baadhi ya Watanzania walioamua kuchangamkia fursa za viwanja vyao. Alisema hatua hiyo ni sehemu muafaka ya kuhakikisha kwamba viwanja hivyo vilivyopimwa na vyenye hati vinakuwa sehemu ya kuendeleza na kusaidia wananchi ambao kwa kupitia viwanja hivyo wanaweza kuvitumia katika fursa mbalimbali kama vile mikopo, kujenga nyumba za biashara na makazi ya kuishi wao na familia zao.

Wednesday, March 16, 2016

RC Makonda alivyopokewa ofisini kwake

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akishukua kutoka kwenye gari lake la Ukuu wa Mkoa wakati alipokuwa akifika kwa mara ya kwanza ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana.
 Katibu Tawala Msaidizi- Utawala, Ellha Mcha (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kumpokea rasmi jana alipofika kwa mara ya kwanza katika ofisi yake.
Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shabani Mhando akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Balozi Juma Mwapachu arejea CCM, asema alichanganywa na mahaba ya Lowassa

Ndugu zangu,
Mtakumbuka kwamba mnamo tarehe 13 Oktoba 2015, nilitangaza kuihama CCM na kurejesha kadi yangu ya uanachama kwenye ofisi ya CCM Kata ya Mikocheni. Nilitoa maelezo kwanini niliamua kujiondoa CCM (maelezo hayo pia niliyabandika katika ukurasa wangu wa facebook). Nilieleza kwamba CCM imepoteza mwelekeo kwa kuamua kumnyima haki ya kugombea mcha mungu Edwad Lowasa. Nikasema Edwad Lowasa ndiye chaguo la wana-CCM na ndiye chaguo la Watanzania. Nikasema nitakuwa mnafiki nikiendelea kubaki CCM huku naamini Edwad Lowasa anafaa kuwa Rais kuliko John Pombe Magufuli.

Balozi Juma Mwapachu katikati akikabidhiwa kadi ya CCM leo jijini Dar es Salaam.

Baada ya miezi miwili ya uongozi wa Magufuli nataka niseme nilikosea sana. Nililewa mahaba ya Lowasa, nililewa ahadi ya Lowasa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje. Niliamini mafuriko ya Lowasa ambayo yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi. Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo.

Leo natangaza kurudi CCM kwasababu nimeona kazi nzuri ya Magufuli. Nimefanya kosa kubwa katika siasa ambalo nawasihi vijana kwenye siasa wasifanye. Nilihama kwa kwasababu ya mtu (Lowassa). Nimerudi kwasababu ya mtu (Magufuli). Nataka niwaahidi kwamba CCM ikiweka mtu hovyo baada ya Magufuli, sitahama. Usemi wa CCM kwamba Chama Kwanza, Mtu Baadaye sasa ndio nauona maana yake. Niliwalaumu CCM kwa kumuacha Lowassa lakini sikujua kwamba CCM ina uwezo wa miujiza wa kuibua jembe bora linaloitwa Magufuli.

Makala: Bayport yapanua wigo wa mikopo ya viwanja katika maeneo sita mapya


*Kibaha, Bagamoyo, Kigamboni, Kilwa, Morogoro na Chalinze waula
*Kila mtu sasa anaweza kumiliki nyumba

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
LICHA ya kuwa na changamoto mbalimbali za kimaisha, lakini suala zima la umiliki wa nyumba na rasilimali muhimu ya viwanja imezidi kuwa rahisi. Ndio, maana uwapo wa taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, inawapatia mwanga wananchi wa Tanzania juu ya adhma ya kumiliki ardhi na viwanja kwa ujumla.
Bayport taasisi inayojihusisha na mikopo ya fedha na bidhaa, mwaka jana mwezi wa tano ilizindua huduma yamikopo ya viwanja katika mradi wake wa Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani.

Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, (kulia) akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya wa mikopo ya viwanja vinavyotolewa na Taasisi hiyo nchini.


Katika mazungumzo na Mtandao huu, Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, anasema taasisi yao imepanua wigo wa kibiashara kwa kuanzisha miradi sita mipya ya viwanja katika maeneo ya Kibaha, Chalinze, Temeke, Kilwa, Morogoro na Bagamoyo baada ya kuuzindua Februari 22, katika Hoteli ya Ramada Encore, huku wageni waalikwa wakiwa ni Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile, Msaidizi wa Mkuu wa wilaya Temeke, Bertha Minga na wadau wengine wa ardhi nchini Tanzania.

Mradi umezingatia suala la mipango miji, maji na umeme ambavyo ni vitu muhimu katika maisha ya mwanadamu. Aidha Mbaga anasema ni kusudio lao kuu kutoa huduma bora kwa wateja na Watanzania ili maisha yawe mazuri kwa kufanikisha suala la makazi. Awali tulianza na huduma ya mikopo ya viwanja katikamradi wa Vikuruti, ambao ulihusisha watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali pamoja na walionunua viwanja vyetu kwa pesa taslimu na kuufanya mradi wetu uende vizuri na ndio maana tumepanua huduma hizi za viwanja.

"Tumezindua huduma ya viwanja katika mji wa Bagamoyo eneo la Kimara Ng'ombe vitakavyouzwa Sh 10,000 kwa mita moja za mraba, ikiwa ni Kilomita 6.5 kutoka Bagamoyo Mjini, huku umeme ukipatikana kwa umbali wa kilomita 1.5 tu bila kusahau maji, alisema Mbaga na kuwataka Watanzania wote waiunge mkono taasisi yao katika mahitaji ya mikopo ya fedha taslimu, viwanja na huduma nyingine muhimu.

Waziri Ummy Mwalimu: Mwanamke wa Afrika bado anakabiliwa na changamoto


Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu ( Mb) ametoa hutuba kwa niaba ya Kundi la Nchi za Afrika wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). 

Mkutano huu wa wiki mbili unawakusanya wawakilishi kutoka serikali mbalimbali duniani na Asasi za Kiraia ambapo hujadiliana na kubalishana uzoefu na kuelimishana kuhusu hatua mbalimbali ambazo serikali zao zinachukua katika kuboresha maisha ya mwanamke na mtoto wa kike.

Wakati mamia ya wanawake kutoka serikalini na Asasi za Kiraia wakiwa wanakutana hapa Umoja wa Mataifa kwa mkutano wao unaojadili hali yao katika maeneo mbalimbali. Mamia mengine ya wanawake hususani wale wa Afrika wanaendelea kukumbana na changamoto lukuki zinazowarudisha nyuma kimaendeleo. Ni wanawake hao wanaoishi katika nchi zenye migogoro, vita visivyokwisha, wenye kukabiliwa na uhaba na ukosefu mkubwa wa chakula, maji safi na salama, matatizo yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, ndio ambao Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu(Mb) ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza kasi ya ushirikiano ili malengo mapya ya maendeleo endelevu (Agenda 2030) yaweze kuwafikia.

Mtandao wa tigo wazindua 4g kwa mbwembwe jijini Mwanza


Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe  Joseph Mkirikiti (katikati), Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula (kulia), Mbunge wa Ilemela Angelina Mabula (wa pili kuhoto), Mkuu wa Kitengo cha Biashara Olivier Prentout (kushoto) na  Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Ali Maswanya (wa pili kulia) wakipiga ngoma ikiwa ni ishara ya  uzinduzi wa mtandao wa tigo wa 4G jijini Mwanza.

Fastjet yapanua mabaya safari za Dar es Salaam na Nairobi


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
               
Dar es Salaam, Machi 15, 2016 – Shirika la ndege la gharama nafuu Afrika, Fastjet Tanzania limeongeza idadi ya safari zake  kwenye njia yake ya Dar es Salaam  na Nairobi ikiwa ni mwitikIo  mkubwa kwa mahitaji ya abiria.

Kuanzia Machi 21 fastjet itakuwa inafanya safari zake mara mbili kwa siku kwenda na kurudi  kati ya miji hiyo miwili  kila siku  ndani ya wiki na hivyo kufanya safari zake  kuwa ni 28 kwa wiki kati ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta  jijini Nairobi.

Shirika hilo ambalo hadi sasa  linafanya safari moja kila siku  kati ya miji hiyo miwili, limeongeza masafa yake ya kuruka  ili kuwapatia abiria huduma nzuri nyakati za asubuhi na jioni. Kwenye safari ya asubuhi, ndege itakuwa inaondoka Dar es Salaam saa 12.00 na kutua Nairobi saa 1.20. Aidha, safari ya kurudi itaanza saa 1.50 na itatua Dar es Salaam saa 3.15.

Aidha, safari mpya za jioni ndege itakuwa inaondoka  Dar es Salaam saa 2.15 na kutua Nairobi saa 3.35. Safari ya kuridi ndege itaondoka Nairobi saa 4.05 na itatua Dar es Salaam saa 5.30. Kupanuka kwa  ratiba hiyo kutawezesha kusafirisha takribani  abiria 19,000 kila mwezi  kupitia safari za fastjet  kati ya hiyo miji miwili, na hivyo kuwapa wasafiri njia nzuri zaidi  na mbadala wa safari kwa nauli wanayoimudu.

Sunday, March 13, 2016

Paul Makonda Mkuu wa Mkoa mpya Dar es Salaam

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara, ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.
Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe leo tarehe 13 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.
Wakuu wa Mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
1. Mh. Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
2. Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga - Mkuu wa Mkoa wa Geita.
3. Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu - Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
4. Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga - Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
5. Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga - Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
6. Mh. Godfrey Zambi - Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
7. Dkt. Steven Kebwe - Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
8. Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven - Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
9. Mh. Anna Malecela Kilango - Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
10. Mhandisi Methew Mtigumwe - Mkuu wa Mkoa wa Singida.
11. Mh. Antony Mataka - Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
12. Mh. Aggrey Mwanri - Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
13. Mh. Martine Shigela - Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
14. Mh. Jordan Mungire Rugimbana - Mkuu wa Mkoa Dodoma.
15. Mh. Said Meck Sadick - Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
16. Mh. Magesa Mulongo - Mkuu wa Mkoa Mara.
17. Mh. Amos Gabriel Makalla - Mkuu wa Mkoa Mbeya.
18. Mh. John Vianey Mongella - Mkuu wa Mkoa Mwanza.
19. Mh. Daudi Felix Ntibenda - Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
20. Mh. Amina Juma Masenza - Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
21. Mh. Joel Nkaya Bendera - Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
22. Mh. Halima Omary Dendegu - Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
23. Dkt. Rehema Nchimbi - Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
24. Mhandisi Evarist Ndikilo - Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
25. Mh. Said Thabit Mwambungu - Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
26. Luteni Mstaafu Chiku Galawa - Mkuu wa Mkoa wa Songwe (Mkoa mpya).

Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa, wataapishwa Jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa 3:30 Asubuhi Ikulu, Jijini Dar es salaamv.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

13 Machi, 2016

Tuesday, March 08, 2016

Proin Promotions Ltd yajivunia kutoa washindi wawili wa tunzo za Africa Magic 2016

 Baadhi ya wadau na wapenzi wa filamu wakiwa uwanja wa ndege wakimsubiri kumpokea Mshindi wa Tunzo ya Filamu bora ya Kiswahili Single Mtambalike katika shindano la Africa Magic lililofanyika nchini Nigeria Mwishoni mwa wiki
wapenzi wakisubiri mshindi

Bagamoyo wapokea vizuri mradi wa viwanja vya Bayport


Meneja wa Bayport wilayani Bagamoyo, Francis Ndunguru, akizungumza na waandishi wa Habari walipotembelea mradi wa viwanja vya mikopo vinavyotolewa na taasisi yao, katika eneo la Kimara Ng'ombe, Bagamoyo, mkoani Pwani jana. Picha zote na Mpiga Picha Wetu, Bagamoyo

Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
WAKAZI na wananchi wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani, wamepokea vizuri mradi wa viwanja vya mikopo vinavyotolewa na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, wakisema kuwa mradi huo utachangia kwa kiasi kikubwa kuupanua na kuuweka mji wao katika kiwango cha juu kimaendeleo.

Meneja wa Bayport Financial Services wilayani Bagamoyo Francis Ndunguru akionyesha alama za viwanja vilivyopimwa katika eneo la mradi wa Kimara Ng'ombe, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani. Viwanja hivyo vinauzwa kwa mkopo kwa watu wote wenye kuhitaji kumiliki ardhi.

Kwa mjini Bagamoyo, mradi huo wa viwanja vya Bayport unapatikana Kimara NG’ombe, huku maeneo mengine ya nchi viwanja hivyo vikipatikana KIbaha, Chalinze, Morogoro, Kilwa na KIgamboni, vikihusisha watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali.
Meneja akionyesha barabara zilivyochongwa kuonyesha ubora wa mradi huo wa Bagamoyo, mkoani Pwani.

Akizungumza na mtandao huu, mkazi wa Bagamoyo, Said Juma, alisema kwamba huduma za viwanja vya Bayport vinavyopatikana kwa fedha taslimu na mikopo si vya kukosa, kwa sababu zitachangia kuuweka mji wa Bagamoyo kwenye kiwango cha juu pamoja na kujibu malalamiko ya wananchi kushindwa kumiliki viwanja kwa njia rahisi na isiyokuwa na gharama kubwa.
Mwandishi wa habari Phillip Daud, akimhoji mwananchi wa Bagamoyo, Mwanaisha Khalfany juu ya ubora wa viwanja hivyo na uwezekano wa Watanzania hususan wakazi wa Bagamoyo kuvichangakia viwanja hivyo vilivyopimwa na vyenye hati.

“Uwezekano wa kumiliki viwanja Bagamoyo mjini ni mgumu kwa sababu vinauzwa bei ghari, hivyo kwa Bayport kuanzisha huduma hizi kwa watu wote bila kusahau sisi wajasiriamali, hakika ni jambo la kushukuru na kuwapongeza kwa mawazo yao mazuri yenye kutuendeleza sisi wananchi na wateja wao,” alisema Juma na kuwataka watu wa Bagamoyo na Watanzania wote kuchangamkia fursa hizo.

Saturday, March 05, 2016

Changamoto za wanawake kumiliki ardhi Tanzania

Hii  ni Ofisi ya afisa Mtendaji Kata ya Iwawa, Kituo cha wakulima

Na Blogs za Mikoa Tanzania
Mila potofu zinazokandamiza wanawake zimeripotiwa kuendelea kushamiri katika baadhi ya mambo baada ya kutembelea katika maeneo tofauti tofauti ya wilaya ya Makete mkoani Njombe na kuzungumza na wakazi wa wilaya hiyo

Katika kijiji cha Iwawa wilaya ya Makete mkoani Njombe mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Jane Sanga amesema wanawake wengi wilayani hapo hawamiliki ardhi kutokana na mila potofu kuwa wamiliki wa ardhi ni wanaume pekee
"Kwa hapa Makete wanawake unaowaona wanamiliki ardhi kwa kiasi kikubwa unakuta ni mjane anaimiliki baada ya kufiwa na mumewe au unakuta mwanamke huyo ana uwezo wa kifedha na ameamua kukunua kipande chake cha ardhi na anakimiliki mwenyewe, hapo hakuna anayemuingilia, na hata wale wajane bado utakuta wanasumbuliwa na ndugu wa marehemu mumewe, kwa hiyo bado hali ni ngumu" amesema Jane

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...