Picha ikimuonyesha Lulu akipanda kwenye gari la mahabusu.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Lulu akiwa katika pozi.
Dhamana hiyo itapitiwa mbele ya Jaji, Zainabu Muruke, ambapo
itatoa picha kamili juu ya kesi ya mwanadada huyo na dhamana yake, baada ya
kudaiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba, mapema mwaka jana.
Kwa miezi kadhaa, msanii huyo amekuwa akisota Segerea,
kufuatia kesi hiyo inayomkabili mwanadada huyo.
Wakati msanii huyo anatoa ushahidi wa kesi yake hiyo,
mwanadada huyo alidai kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake,
marehemu Kanumba, hivyo kujenga hali ya wivu.
Muhtasari wa ushahidi huo ulisomwa Desemba 22 mwaka jana na
Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka, mbele ya Hakimu Mkazi, Augustino
Mmbando.
Lulu katika kesi hiyo anatetewa na Mawakili Fuljensi Masawe,
Kenedy Fungamtama na Peter Kibatala.
Picha kamili ya maisha ya Lulu itajulikana Jumatatu baada ya
dhamana iliyoombwa kwa msanii huyo kupitiwa, huku mashabiki wa mwanadada huyo
wakiendelea kuguswa na sakata la kesi ya msanii huyo mwenye makeke mengi katika
tasnia ya filamu nchini.
No comments:
Post a Comment