Wachezaji wa timu ya Black Leopards wakitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, tayari kuwavaa Yanga kesho.
Na Mwandishi Wetu, Dar es
Salaam
MABINGWA wa zamani wa
Tanzania Bara, Yanga SC, kesho inaingia uwanjani kumenyana na Black Leopards ya
Afrika Kusini, ambao tayari wameshatua nchini leo.
Mchezo huo umepangwa kuanza saa 10.00 jioni na maandalizi yake yamekwisha kamilika huku waandaaji wakipunguza viingilio ili kuwawezesha
mashabiki wengi kufika.
Mratibu wa mechi hiyo, Shafii Dauda wa Prime Time promotion
alisema jana kuwa maandalizi yote yamekamilika na wamepunguza kiingilio cha Sh
5,000 na Sh 7,000 na kuwa cha Sh 3,500 ili mashabiki wengi waingie kuangalia
mchezo huo wa Kimataifa wa kirafiki.
Viingilio vingine ni shs 7,000 kwa viti vya rangi ya machungwa,
wakati VIP C ni Shs 15,000, VIP B Sh 20,000 na VIP A Sh 30,000.
Kocha wa timu hiyo, Abel Makhubela alisema kuwa wanauzoefu wa siku
nyingi na walifanya ziara nchi mbali mbali katika afrika na kuja Tanzania ni
moja ya faraja kwao.
Ziara hii ziara yetu ya kwanza Tanzania, tumefanya ziara nchini
Zimbabwe na nchi nyingie, tulipata matokeo mazuri na vile vile tunatarajia
kupata matokeo mazuri hapa, nimekuja na wachezaji wangu wote wa kikosa cha
kwanza, jumla ya wachezaji ni 23, mashabiki watarajie mchezo mzuri,” alisema
Makhubela.
Alisema kuwa wanaijua Yanga na Simba ni moja ya timu nzuri na
maarufu bara la Afrika na hivyo wamejiandaa kwani ni kipimo kizuri cha ligi ya
kwao ambayo ipo katikati.
No comments:
Post a Comment