Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAPO
wengi wanaoingia katika maisha magumu kutokana kujiingiza mahali ambako sio
pazuri.
Kwa bahati mbaya, kuingia huko kumetokana na tabia zao za kukubali
kudanganyika na vijineno vitamu vinavyotolewa na wenzi wao.
Nasema
hivyo maana inajulikana kama maneno ni kitu cha kawaida kabisa.
Waswahili
wamesema hata kwenye khanga yapo. Ni kutokana na hilo , nakuomba ndugu msomaji
wangu kuwa makini katika suala hilo lenye tija na umuhimu wako.
Mambo
haya hutokea sana kwenye mapenzi. Utakuta mwanadada au mvulana kutumbukia kwa
watu ambao ni waongo. Ni matapeli wa kutupwa. Ni mafisadi wa mapenzi, jambo
linalowachanganya wenzao siku za usoni.
Ni
hapo binti anapomwambia mvulana wake kuwa Nakupenda sana . Ni wewe tu hapa
chini ya jua na maneno mengine lukuki. Kwa bahati mbaya, wenzi wao hao,
wamejaza wapenzi. Mtu huyo huyo ana wapenzi zaidi ya watano.
Huu
ni wizi na ujambazi wa kutupwa katika kona ya wapendanao. Sasa kwanini ujute
siku za usoni? Kwanini? Ni wakati wako wa kuchagua kuwa na watu ambao ni salama
na hawawezi kukuweka kwenye mtego.
Dunia
imeharibika. Magonjwa mengi yamejaa. Kuwa na mvulana au msichana ambaye
hajatulia ni kujiwekea ramani ya kifo. Nasema hivyo huku nikikutana mpenzi
msomaji wangu kutodanganyika na maneno ya watu hao.
Kuwa
makini unapokutana na watu hao. Fungua moyo wako kama unavyotaka kwa kuchukua
muda wako kuchunguza kabla ya kudanganyika. Hayo ni maneno tu. Siku zote
hayawezi kuvunja mfupa, hivyo wakati ni wako.
Chagua
pumba na mchele kwa faida yako. Nimelazimika kuandika makala haya kwakuona watu
wengi wanatumbukia katika shimo hilo . Wapo waongo kiasi kwamba wanaongea hadi
kutaka kulia kwa kuwabuluza watoto wa watu.
Sio
wanaume au wasichana. Wote ni waongo na wanaolaghai wenzao. Kwanini sasa
upoteze muda wako kwa kukubali kudanganywa? Inakuwaje? Kumbuka kosa moja tu
linaweza kukugharimu miaka nenda rudi.
Huu
ni wakati wako wa kuangalia kitu gani cha kufanya kwa faida yako mwenyewe.
Unaweza kujiuliza haya yanakujaje, ila ukweli ni kwamba kudanganywa kunauma
sana . Kunachanganya kichwa vibaya.
Penzi
la uongo halina thamani. Linakera kupita kiasi. Ndio, maana mtu anaonyesha
upendo wake wa dhati, lakini anazomewa kimoyo moyo. Kuwa naye kwa dakika kadhaa
lakini muda huo huo ataondoka na kwenda kwa mwengine.
Fanya
ufanyavyo lakini kamwe huwezi kuwa sehemu ya maisha yake, maana yupo mtu ambaye
kikweli ni chaguo lake la moyo. Unapoteza muda wako bure. Chukua uamuzi sahihi
kwa ajili ya maisha yako.
Wanasiasa
wanaita kujivua gamba kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, maana hapo ulipo sio
mahali sahihi. Kwa bahati mbaya, sehemu hiyo ungeweza kuibaini mapema kama
ungetumia muda mwingi kuchunguza na sio kukubali kirahisi kwa maneno yake ya
matamu.
Sasa
je, maana kama ni maneno tu yaliyokufanya uvutiwe naye basi yanakuweka sehemu
ngumu na kupoteza mwanga wako wote wa maisha. Mapenzi ni matamu lakini sio kwa
kuingia kwa mtu ambaye hajui thamani ya kupendwa.
Huu
ndio wakati wako wa kuangalia hapo ulipokuwa sasa ni sehemu sahihi? Hapo
ulipokuwa ni kwa milele au upo kwa muda? Amekupataje wewe? Je, alikuahidi kitu
gani, iwe ni ndege, meli au nyumba ya kifahari?
Kumbuka
unaweza kufaidi penzi sehemu yoyote isipokuwa iwe ni yenye utulivu na thamani
ya kweli ya mapenzi na sio maneno ya uongo ambayo kwa kawaida hayawezi kuwa ya
kweli na kukuweka sehemu nzuri.
Mapenzi
matamu bwana lakini yanaweza kuwa machungu kwako hivyo wakati ni huu wa
kuangalia thamani ya moyo wako kwa faida yako.
0712
053949
0753
806087
No comments:
Post a Comment