Limekuwa Taifa la
wabunge wasaka ‘tonge’
Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete
Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WATANZANIA
waliokuwa wengi wanaishi maisha magumu kwa kiasi kikubwa. Wapo ambao mlo wao wa
siku moja ni tatizo huku unga wa sembe ukiuzwa toka Sh 1300 hadi 1500.
Mbali
na unga wa sembe, bidhaa nyingine kama vile sukari imekuwa ikiuzwa zaidi Sh 2000,
tofauti na bei elekezi iliyotolewa na Serikali
ambayo ilikuwa na lengo la kumpunguzia makali mlalahoi.
Kutokana
hali hiyo hivi sasa yapo baadhi ya maeneo ambapo watu wameanza kuhangaika kwa
ajili ya kutafuta mlo alau kuweza kukidhi mahitaji ya familia zao hali
inayolifanya Taifa letu kuwa katika picha tofauti na ile inayohubiriwa ya
kufika kuwa nchi yenye neema ya kupata mlo uliokamilika.
Ili
kuweza kuondokana na tatizo hili la umaskini hata katika kutafuta chakula kwa Watanzania
walio wengi, zinahitajika juhudi za makusudi kwa kuongozwa na wawakilishi wa
wananchi katika majimbo yao ili kuweza kuweka mipango ya kuwasaidia wapiga kura
wao.
Katika
jambo lolote ambalo linahitaji mafanikio chanya ni lazima ushiriki wa wabunge
uwepo kwa kina kwani wao hupaza sauti zao na hata kuweza kutunga sheria na sera
ambazo zitamkomboa mpiga kura wake.
Kutokana
na hali hii ambayo imekuwa ikiwaumiza wananchi wengi hasa wanaoishi katika
ameneo ya vijiji wengi wamekuwa hawafikiwi na wawakilishi wao na hata
kusikiliza kero zao kwa kina hali inayowafanya wajione ni sawa na yatima
kutokana na kupoteza matumaini na wabunge wao.
Silisemi
hili kwa kuwaonea wabunge wetu ila ninachoweza kusema wengi wao wakati wanaomba
nafasi hizo kuanzia ndani ya vyama vyao na hata nje ya ambao walibeba matumaini
ya kuwakomboa wapiga kura wao.
Baada
ya kuchaguliwa kwao wengi wao waliishia kuishi mijini huku wananchi wakiendelea
kupiga mayowe ya kutowaona tena wawakilishi wao zaidi ya kuwaona kupitia
luninga hasa wanapokuwa ndani ya Bunge.
Ninajua
wapo wengi ambao watasema kuwa nimetumwa kuyasema haya leo hii kwa ajili ya
mkakati maalumu, lakini la hasha! ninapenda kuweka wazi hili baada ya kuona
kila kukicha taarifa kupitia vyombo vya habari namna wananchi wanavyolalama
mithili ya kuku yatima aliyekosa mama wa kumuongoza katika kutafuta chakula
chake huku kila mwewe anayepita anataka kumnyakua.
Wakati
wa utawala wa Rais wa kwanza wa Taifa letu, hayati Mwalimu Julius Nyerere,
kabla na baada ya Uhuru kila wakati alikuwa akisema tunataka na tumepata uhuru
na sasa tuna kazi moja ya kupamba na maadui watatu ambao ni maradhi, ujinga na
umaskini.
Na
bado akaendelea kusema ili tuweze kuendelea na kupiga hatua tunahitaji ardhi,
siasa safi na utawala bora, ambao hadi leo hii imekuwa ni ngonjera kwa baadhi
ya wabunge kushindwa kutimiza majukumu yao ya utawala wa majimbo.
Mbali
na hilo hali ilipofikia hivi sasa kuna baadhi ya wilaya na majimbo yamekumbwa
na uhaba wa njaa hali inayowafanya wananchi kula mizizi na hata kuuziwa bidhaa
za chakula kwa bei ya juu lakini bado wabunge kama wawakilishi hawaonekani
katika maeneo yao na hata wanapopigiwa simu na wapiga kura wao hutoa majibu
mepesi, kuwa nipo kikaoni hali ya kuwa yumo katika gari lake anapigwa kiyoyozi.
Ninasema
ukweli ili siku moja nami nitoke kwenye lawama ya kwa nini sikuisaidia jamii
yangu kwa kusema ukweli juu ya viongozi ambao wamekuwa wakikiuka misingi ya Taifa
letu.
Hivi
karibuni Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA)
ilitangaza kuanza kwa mvua za vuli ambazo zinatakiwa kutumiwa vema na wananchi,
lakini katika hili hakuna hata mbunge mmoja aliyejitokeza na kwenda
kuwahamasisha wapiga kura wake ili waweze kulima ili kuweza kuondokana na baa la
njaa.
Wakati
nayasema haya; wapo baadhi ya wabunge wamekuwa na mawazo yale yale ya zamani na
hawana mipango zaidi ya kulia huku wakisema tusubiri bajeti toka serikalini.
Kuwa
na wawakilishi wa aina hii ni hatari kwa ustawi wa Taifa na watu wake kwani
wanaishia kulipwa mshahara na posho za walipa kodi wanyonge huku wao
wakishindwa kutimiza majukumu yao kikamilifu.
Katu
huwezi kuitwa mbunge wa jimbo hali ya kuwa wewe siku zote mawazo yako yapo katika
kujadili siasa za kitaifa badala ya kujiuliza ni namna gani umeweza kutatua
kero ya maji katika jimbo lako je, hali ya kilimo ikoje na kama ukitumia vema
nafasi yako wapiga kura watanufaika vipi na uwakilishi wako kwao.
Kila
kona kumekuwa na kero na shida ya maji huku baadhi ya vijiji vyao, bado wapo
viongozi ambao kila kukicha wanaibuka na hoja binafsi ndani ya Bunge.
Lakini
kiongozi huyo anajua, hadi wazo lake litakapofanyiwa kazi, ni dhahiri muda
mrefu utapita. Kama wananchi wanaishi kwa taabu leo, unawezaje kusubiri kikao
cha Bunge?
Kama
ndivyo hivyo katu atuhitaji mbunge ambaye yupo kimya mijini akijitanua na
familia yake, wakati wapiga kura wake wanakufa na njaa sambamba na kuhangaika
na kero ya maji.
Kuwa
na wabunge wa aina hii ni mizigo na ninaweza hata kuwaita wasaka tonge ambao
wakishapata wanaishi na familia zao vizuri wakati Watanzania walio wengi
wanaishi maisha ya taabu na kulala na njaa vijijini.
Bila
hata kuangaliana usoni, vijiji vingi vya Tanzania vinasumbuliwa na njaa, vyakula
vimekuwa vikipatikana kwa bei ya juu, huku vibarua navyo vikikosekana, ipo haja ya Serikali kutangaza baa
la njaa katika wilaya zilizokumbwa na janga hilo.
Tusikae
kimya na kusubiri hatari zaidi. Watu wengi watanyanyasika au hata kupoteza utu
wao na uhai wao.
Kwa mfano; mwishoni mwa mwaka jana, Kampuni ya Mwiba Holding Ltd ya hifadhi ya wanyama pori katika pori la Makao lilitoa mahindi tani kumi yenye thamani ya Sh milioni 15 kwa ajili ya wakazi kwenye kata hiyo wanaosumbuliwa na njaa.
Kwa mfano; mwishoni mwa mwaka jana, Kampuni ya Mwiba Holding Ltd ya hifadhi ya wanyama pori katika pori la Makao lilitoa mahindi tani kumi yenye thamani ya Sh milioni 15 kwa ajili ya wakazi kwenye kata hiyo wanaosumbuliwa na njaa.
Kwa
mujibu wa diwani wa kata hiyo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Makao, wilayani
Meatu, mkoani Simiyu, Anthon Phillip, alisema zaidi ya kaya 400 zinakabiriwa na
njaa kutokana na mtawanyiko wa mvua uliochanganyika na ukame.
Mbali na Sengerema, lakini pia Ngorongoro hali hiyo pia imesharipotiwa, hivyo kuonyesha kuwa tatizo hilo lipo na linahitaji ufumbuzi wa haraka.
Wakulima wetu wamekuwa wakitaabika na kufikia kuchoka kuendelea na kazi hiyo, jambo linalosababisha njaa kuendelea kukaa kwa wananchi wengi.
Ili kuweza kujenga nchi ambayo ina wawakilishi ambao wamejawa na uzalendo na huruma kwa wapiga kura wao ni lazima tuondakane na wabunge wasaka ‘tonge’.
0712
053949
0753
806087
No comments:
Post a Comment