Wane Star, akiwa jukwaani.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWIMBAJI ngoma za asili Wane Star na bendi ya
muziki ya Kalunde, wanatarajiwa kutoa burudani kwenye onesho la mavazi la Lady
In Red, litakalofanyika Februari 9 mwaka huu, katika Ukumbi wa Hoteli ya
Serena.
Akizungumza na Handeni Kwetu, muandaaji wa onesho
hilo na kupitia Kampuni yake ya Fabak Fashion, Asia Idorous, amemtaja Wane Star
na Kalunde kuwa ndio watakotoa burudani kwenye onesho hilo.
“Nimewapanga Wane Star na Kalunde kusindikiza onesho
langu la Lady In Red, naamini watatoa mchango mkubwa kwenye suala zima la
kunogesha onesho hilo la tisa la Lady In Red,” alisema Asia.
Katika onesho hilo wabunifu mbalimbali kama Khadija
Mwanamboka, Ally Remtullah, Mustafa Hassanal, Dayana Magese, Rukia Walele na
Annete Ngogi, wanatarajiwa kuonesha mavazi yao.
Asia aliwataja baadhi ya wadhamini wa onesho hilo
kuwa ni Darling Hair, Redds, Vayle Spring, Kebbys Hotel, One Touch Solution na Nyumbani
Lounge.
No comments:
Post a Comment