https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, August 31, 2013

MAMBO FULANI MUHIMU:Umegundua nini kwa umpendae, chukua hatua

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KUNA watu ambao wanaendelea kuingia kwenye wasiwasi mkubwa kwasababu ya kutofurahia uhusiano wao au ndoa yao kwa wale waliofanikiwa.
Mambo Fulani Muhimu kwa watu muhimu.
Hawa ni wale wanaoshi bila hata kugundua namna gani ya kuwafurahisha watu wao.

Ni wale ambao licha ya kutarajia makubwa kutoka kwa wapenzi wao, ila wametumbukia katika wasiwasi wa aina yake.

Ndugu msomaji wangu, katika uhusiano wa kimapenzi, kuna wale ambao wapo pamoja lakini wanapokuwa kwenye tendo la ndoa, mmoja wapo haridhiki.

Francis Cheka amtandika Mmarekani Phil Williams Ukumbi wa Diamond Jubilee na kuwapa raha Watanzania


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa Tanzania, Francis Cheka, ameendeleza ubabe wake baada ya kumtandika mpinzani wake Phil Williams katika pambano lao lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Bondia wa Tanzania, Francis Cheka, pichani
Ushindi huo wa Cheka ni furaha kubwa kwa Watanzania wote, hususan wale wanaotokea mkoani Morogoro ambapo mkali huyo ndipo anapotokea kwenye mji huo.
Cheka na Phil Williams wakimenyana ulingoni.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara akimvisha mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBF, Francis Cheka, baada ya kumpiga mpinzani wake Phil Williams katika Ukumbi wa Diamond Jubuilee.

Cheka alipata ushindi huo na kunyakua ubingwa wa Dunia wa WBF, baada ya kumpiga Williams kwa pointi kuonyesha kuwa yeye ni mkali na hana mpinzani hapa Tanzania.

Mbali na kufanikiwa kumchapa Mmarekani huyo, mara kwa mara Cheka amekuwa akiibuka na ushindi kila anapoingia ulingoni kupambana na mabondia wa Tanzania.

Dayna ashusha pumzi

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Mwanaisha Said maarufu kama ‘Dayna’, amesema yupo katika nafasi nzuri kisanaa kutokana na kudhamiria kufanya makubwa katika sanaa hiyo na kuwapa raha mashabiki wanaomuunga mkono.
Dayna akiwa amepozi kama unavyomuona hapo.
Mwimbaji huyo wa ‘Mafungu ya Nyanya’ aliliambia gazeti hili juzi jijini Dar es Salaam kuwa mpaka sasa ameweza kuachia nyimbo tatu ambazo zote zilipokelewa kwa shangwe.

Alisema hali hiyo inamfanya aamini kuwa kiwango chake kimuziki kimefikia sehemu nzuri kiasi cha kumpa imani ya kuendelea kuwa juu katika tasnia hiyo.

“Nilianza na wimbo wangu wa Mafungu ya Nyanya na kufuatiwa na nyimbo mbili makini na zilizokonga nyoyo za mashabiki wangu kila nilipotia mguu.

DIAMOND PLATNUM: Kutoka Tandale hadi Serena Hotel kuweka historia mpya kimuziki


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMA kuna watu hawataki kuamini kuwa msanii Nassib Abdulmalick maarufu kama 'Diamond Platinum' ni mkali na mwenye ukwasi wa kutosha tu, huu ndio muda wao wa kuamini kinachosemwa.
Hapa Diamond akiwa nchini Uingereza kwenye safari zake za kimuziki.
Ni pale alipoweza kuwakusanya wasanii, wadau wake na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena, iliyopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzindua video ya wimbo wake ujulikanao kama My Number 1.
Diamond alipokuwa anamkabidhi gari lake mzee Gurumo.
Watu wengi wanataka kusikia kinachotakwa kusemwa na msanii Nassib Abdulmalick ama Diamond Platinum kama anavyopenda kutambulika hivyo katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.
Msanii Diamond alipokuwa akizungumza wageni wake aliowaita katika Hoteli ya Serena, juzi jijini Dar es Salaam.
Wapo waliokuwa wakibashiri labda anataka kumtambulisha mpenzi mwingine kama ilivyokuwa kawaida yake. Hizi zilitokana na kauli ya msanii Diamond alipowakalibisha wadau walioalikwa katika tukio la kuonyesha video yake mpya ya ‘My Number 1’.

Hakika kulikuwa na maswali kadhaa yaliyoshangaza wengi. Kwanini Diamond? Huyu ni nani? Mbali na kutaka kuonyesha video yake mpya, kipi kingine anataka kusema?

Kweinchili: Bila sisi wenyewe Handeni haitabadilika, chifunge bete mwe vigudi.


Na Adam Malinda Seif.
KWA mara ya kwanza naomba kutumia nafasi hii niliyoomba mwenyewe katika mtandao huu (Blog ya Handeni Kwetu) ili kuunganisha mawazo ya yangu kwa Watanzania wenzangu, hususan wale wilaya ya Handeni na kupeana mawazo muafaka kwa mustakabali wa Taifa.
Adam Malinda, mwandishi wa makala haya.
Hii itafanikiwa kwa kuleta usawa, kushauriana kwa njia ya amani kabisa kutoka kwa sisi wananchi na viongozi tunaowachagua. Lengo ni si kupata sifa za mtu mmoja mmoja, bali ni kutafuta jawabu la matatizo ya waliowengi na hatimae kuondokana na ufukara uliokithiri.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani.
Kwa nafasi hii lengo ni kuunganisha nguvu kila upande ili kuwa kitu kimoja ingawa nafahamu kutoka hali fulani kwenda nyingine kuna changamoto nyingi ikiwa ni baadhi ya watu kuona wanaingiliwa katika maslahi yao, bila wao kujali wangapi wanaathirika na mfumo huo ambao wao kwao ni neema.

Lakini mara zote linapokuwepo tatizo katika mifumo fulani ya maisha inakuwa imetengenezwa kwa madhumuni fulani, hivyo tunapaswa kuwa wawazi katika kubainisha haya tunayoyazungunza yana faida ipi kwa walio wengi, na kuwasadikisha kuwa yakifanyika haya yataweza kufika kule wanakotarajia wengi, hali itakayohamasisha maendeleo tunayokusudia.

Nilijisikia hivi juzi aibu kubwa na kunichoma moyo pale jamaa mmoja ambaye sasa ni mchungaji wa dhehebu moja tulipokutana katika ofisi ya chombo kimoja cha habari akisahau  kwa kuniuliza hivi wewe ni kutoka eneo gani la Tanzania?

Friday, August 30, 2013

TFF wasaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni ya Azam kwa ajili ya kuonyesha mechi za ligi Kuu



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Azam Media leo (Agosti 30 mwaka huu) wamesaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni (exclusive rights) utakaoiwezesha Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Rais wa TFF. Leodgar Tenga
Mkataba huo wa miaka mitatu wenye thamani y ash. 5,560,800,000 umesainiwa kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Athuman Nyamlani amesaini kwa niaba ya TFF wakati aliyesaini kwa upande wa Azam Media ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Thys Torrington.

Ligi Kuu ya Tanzania sasa itakuwa ikipatikana kupitia kisimbuzi (decorder) cha Azam TV kitakachokuwa na chaneli zaidi ya 50. Mechi hizo zinatarajiwa kuoneshwa moja kwa moja wakati wowote kuanzia mwezi ujao.

Makamu wa Rais wa TFF, Nyamlani amesema udhamini huo wa televisheni ni fursa pana kwa klabu kwani zitaweza kujitangaza zaidi huku wachezaji nao wakipata soko zaidi za mpira wa miguu.

Picha tofauti yaliyojiri wakati Diamond anamkabidhi gari lake mzee Muhidini Gurumo

1
Mwanamuziki Diamond Platinum akimkabidhi funguo ya gari mzee Muhidini Gurumo.
2
Mzee  Muhidin Gurumo akimshukuru Diamond.
3
Diamond akimuongoza mzee Gurumo kwenda kumuonyesha gari.

CCM yajitosa sakata la mafao ya wazee Tanzania


Baadhi ya wawakilishi wa Mtandao wa Wazee wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye nje ya ofisi za Makao Makuu ya Chama Dodoma leo Agosti 30, 2013.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na mmoja wa wawakilishi wa Mtandao wa Wazee Bibi Koku , Wazee hao walifika Makao Makuu ya CCM kuja kuzungumza madai ya mafao yao ambayo waliahidiwa na serikali.


LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...