Kikosi cha maangamizi cha Twanga Pepeta
Na Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam
BENDI ya muziki wa
Dansi Tanzania, African Stars Band Twanga Pepeta Ijumaa hii wtafanya bonge la
shoo kwa ajili ya kuukaribisha mwaka huu wa 2013, litakalofanyika katika Ukumbi wa Harbours uliopo Kurasini.
Meneja wa Twanga Pepeta, Hassan Rehani, alisema onyesho hilo litaanza saa
tatu usiku na maandalizi yake yamekwisha kukamilika kinachosubiriwa ni muda tu
ufike ili burudani ipate kutolewa.
Katika onyesho hilo
Twanga Pepeta itatambulisha mitindo yake mbalimbali pamoja na nyimbo zake mpya
tano zinazotarajiwa kuwemo katika albamu yake ya 12 ya Bendi hiyo
itakayozinduliwa baadaye mwaka huu.
Nyimbo hizo ni
“Shamba la Twanga” iliyotungwa na Grayson Semsekwa, “Nyumbani ni Nyumbani”
iliyotungwa na Kalala Jr, “Ngumu Kumeza” umetungwa na Mirinda Nyeusi, “Kila
Nifanyalo” umetungwa na Juma Said au J4 na “Mwenda Pole” uliotungwa na Badi
Bakule.
No comments:
Post a Comment