Michael Wambura, akisisitiza jambo.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIBU
Mkuu wa zamani wa kilichokuwa Chama cha Mpira wa miguu (FAT), sasa Shirikisho
la Soka nchini (TFF), Michael Wambura, leo amechukua fomu za kuwania nafasi ya
Makamu wa Rais, katika Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu.
Wambura
alichukua fomu jana za kuwania nafasi hiyo katika Ofisi za TFF, ambapo pia
aliwaambia waandishi wa habari kuwa lengo lake ni kuchangia maendeleo ya mpira
wa miguu, baada ya kipindi cha Leodgar Tenga kumalizika.
Wambura
ameingia kwenye uchaguzi huo, huku akiwa na kumbukumbu ya kufanyiwa mizengwe,
ambapo hata hivyo mwenyewe alikiri kukubali yaliyofanywa na Rais anayemaliza
muda wake, Leodgar Tenga.
Akizungumza na Handeni Kwetu, Wambura alisema,“Nimeamua
kuchukua fomu kwa ajili ya kusaidiana na wadau wengine wa michezo kukuza na
kuendeleza mazuri yaliyofanywa katika kipindi cha Tenga, ambaye hapana shaka
ametangazaa kuwa hataendelea kugombea,” alisema.
Ofisa
Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema kuwa mbali na Wambura, wengine sita
wamechukua fomu za kuwania ujumbe hivyo, hivyo kufikisha watu 27 waliochukua
fomu hizo.
No comments:
Post a Comment