Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
HALI inazidi kuwa mbaya kwa vurugu na maandamano, baada ya
wasanii kutangaza kufanya maandamano mfululizo, endapo Serikali itaendelea
kuchekea dhuluma na manyanyaso wanayoendelea kufanyiwa wasanii hapa nchini.
Michael Sangu, Mwenyekiti TDFAA
Hatari hiyo ilitangazwa jana na wasanii zaidi ya 200
waliokutana katika Ukumbi wa Vijana, Kinondoni, wakiongozwa na viongozi wao
kutoka Mashirikisho mbalimbali, ikiwamo lile la Filamu TAFF.
Simon Mwapagata, msanii wa filamu Tanzania
Handeni Kwetu ilikuwapo katika viwanja hivyo na kukuta
wasanii wengi waliokuwa wakijadili mambo yao huku wakiwa na hasira kali kutoka
kwa viongozi, hasa wale wa COSOTA na Bodi ya Filamu Tanzania, chini ya Mkurugenzi
wake, Joyce Fisoo.
Akizungumza na Handeni Kwetu, Mwenyekiti wa Chama cha
Waigizaji Tanzania (TDFAA), Michael Sangu, alisema sheria zilizotungwa kwa
ajili ya wasanii hazina mashiko.
Alisema sheria hizo zitazidi kuongeza maisha duni kwa
wasanii Tanzania, kama walivyokufa baadhi yao wakiwa hawana chochote cha maana
zaidi ya kufanikiwa kuwa maarufu.
“Mchakato mzima wa kanuni za utekelezaji wa sheria ya filamu
na michezo ya kuigiza Tanzania Bara haukuhusisha wasanii wadau, wakiwamo
wasanii.
“Hii ni hatari maana itaongeza ugumu wa utendaji kazi, huku
wachache wao kuendelea kufanikiwa, huku serikali ikiwa kimya, jambo ambalo kwa
pamoja hatiwezi kulichekea,” alisema.
Awali wasanii wengi walipata kutoa maoni yao katika kutafuta
maisha bora ya wasanii, huku lawama zao zote wakizielekeza kwa watendaji wa juu
wa COSOTA, chini ya Yustus Mkinga na Joyce Fisoo wakitaka waondoshwe katika
nafasi zao.
“Kama hakutakuwa na mabadiliko katika nafasi za watu hawa,
hakika hatuwezi kufanya nao kazi, maana kauli zao, matendo yao katika suala
zima la sanaa hatuna imani nayo,” alisema Simon Mwapagata akiungwa mkono na
mamia ya wasanii wenzake.
Endapo wasanii hao watafanya maandamano bila kuchoka
kushinikiza watendaji hao wang’oke katika nafasi zao, ni wazi nao watakuwa
wameingia katika kutingisha utawala wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, mmoja wa
viongozi wa juu wan chi wanaokubaliwa na waliokuwa karibu mno na wasanii hapa
nchini.
Serikali kwa kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inapaswa kuliangalia hilo kwa haraka kabla ya kuzidi kuingiza chokochoko katika vuguvu vugu hizo za wasanii kwa kusikiliza kilio cha wasanii wao.
No comments:
Post a Comment