Na Mwandishi Wetu, Handeni
MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Handeni, Athumani Malunda, pichani, amewataka
wananchi kuwakataa wawekezaji wanaoingia wilayani humo kwa kisingizio cha
kuchukua mashamba kwa ajili ya kilimo lakini badala yake, wanachoma mkaa na
kukata mbao na kuleta hatari ya jangwa wilayani humo.
Akizungumza
na wananchi wa Kijiji cha Kilimamzinga kilichopo kata ya Kang'ata wilayani
hapa, Mwenyekiti huyo alisema wawekezaji wa aina hiyo hawafai hata kidogo.
“Ndugu
zangu wa Kilimamzinga, hawa mliotueleza kwamba wameweka mnara wa simu na leo
hii wamewapa fedha za kujengea nyumba ya mwalimu wanafaa sana sababu
wanatusaidia katika maendeleo yetu.
“Ila tusikubali
kupokea wawekezaji wanokuja kwa lengo la kutaka mashamba ili walime lakini
baadaye wanachoma mkaa na kupasua mbao, tutakosa mvua wilaya yetu tukizidi
kukata miti," alisema Malunda.
Mbunge wa
jimbo hilo, Abdallah Kigoda, akizungumza katika mkutano huo amewataka viongozi
wa kata kuligawa haraka shamba la mwekezaji huyo katika kijiji hicho cha Gole
kwa kuwa taratibu za kupewa mwekezaji huyo zimekiukwa.
Pia
ametaka viongozi wa kata kufanya utafiti katika maeneo mengine katika wilaya
hiyo mashamba ambao yamekiukwa utaratibu wapewe wananchi wa Handeni ambao wengi
wao hawama mashamba ya kutosha.
No comments:
Post a Comment