Mkuu wa Mkoa Tanga, Chiku Gallawa
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKUU wa
Mkoa wa Tanga, kesho anatarajiwa kuzindua jengo la wazazi katika Zahanati ya
kijiji cha Lumutio, Kata ya Pwagi, wilayani Kilindi mkoani Tanga, ikiwa ni
muendelezo wa ziara yake itakayodumu kwa siku nne.
Mkuu wa Wilaya Kilindi, Selemani Liwowa
Akizungumza
na Handeni Kwetu leo mjini hapa, Mkuu wa Wilaya Kilindi, mkoani Tanga, Selemani
Liwowa, alisema uzinduzi wa jengo hilo utakuwa wa kwanza kwa mkuu wao wa Mkoa.
Alisema
taratibu zote kwa ziara ya Mkuu wa Mkoa zipo sawa, kwa ajili ya kutembelea na
kujionea mambo mbalimbali yanavyoendelea katika wilaya hiyo ya Kilindi.
“Tutakuwa
naye Mkuu wa Mkoa kwa siku zisizopungua nne, hivyo naamini mengi yaliyopangwa katika
utaratibu wetu yatakwenda sawa, ikiwa ni pamoja na jengo la wazazi.
“Ni ziara
nzuri kwa Mkuu wetu wa Mkoa, huku nikiamini kuwa atajionea mambo mengi katika
wilaya yetu na kufikia uamuzi kama sehemu ya utawala kwa mkoa mzima wa Tanga,”
alisema Liwowa.
Wilaya ya
Kilindi imetokana na kugawanywa kwa wilaya ya Handeni mkoani Tanga, kama sehemu
ya kufanikisha maendeleo ya watu wao, ambapo pia kumekuwa na changamoto nyingi,
ikiwamo njaa na shida ya maji kwa miaka kadhaa sasa.
No comments:
Post a Comment