HATIMAE Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania FAT
sasa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Michael Wambura, ametimuliwa kuwa
mwanachama wa klabu ya Simba, kwa tuhuma za kuipeleka klabu yake mahakamani.
Sunday, August 03, 2014
Chiku Gallawa mgeni rasmi Handeni Kwetu Foundation
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa, pichani chini, anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika uzinduzi wa taasisi ya Handeni Kwetu Foundation, utakaofanyika
kesho Jumanne, katika Ukumbi wa Vijana Social Hall, Kinondoni, jijini Dar es
Salaam.
Tukio hilo la uzinduzi wa taasisi hiyo limepangwa kuanza saa
10 za jioni ambapo wamealikwa wageni mbalimbali kwa ajili ya kuitambulisha
kabla ya kuanza kazi zake rasmi nchini Tanzania.
Akizungumzia hilo, jijini Dar es Salaam, Msemaji wa taasisi
hiyo, Kambi Mbwana, alisema kuwa wameona wamualike RC Gallawa kuwa mgeni rasmi
kwakuwa ni miongoni mwa viongozi makini na wenye kiu ya maendeleo hapa nchini.
Alisema kuwa kitendo cha kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa Tanga, kinaonyesha
namna gani viongozi wa serikali wanashirikiana na wadau wote kwa ajili ya
kufanikisha mipango ya kimaendeleo.
“Tanzania imejaliwa kuwa na viongozi makini mno, hivyo
taasisi imemualika Mheshimiwa Gallawa kuwa mgeni wake rasmi ili ashirikiane na wageni
waalikwa kuitambulisha taasisi.
“Tunaamini kwa pamoja tutafanikisha kuitambulisha taasisi kwa
wadau wote, hususan Watanzania kwa kupitia Handeni Kwetu Foundation,
ukizingatia kuwa imesajiliwa kufanya kazi zake nchini nzima,” alisema.
Kwa mujibu wa Mbwana, sera na mikakati ya taasisi hiyo
itaanikwa katika utambulisho huo utakaokuwa na malengo mahususi ya kujikwamua
kiuchumi na kuhamasisha masuala ya utawala bora.
Subscribe to:
Posts (Atom)