Na Mwandishi Wetu, Mbeya
WAENDESHAJI wa bahati nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’,
leo wamemkabidhi Sh Milioni 20 mshindi wao wa droo ya 18, Linda Mhewa, ambaye
ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji University (TEKU), kilichopo
jijini Mbeya.
Mshindi wa droo ya 18 ya Biko, Linda Mhewa, akiwa anazishangaa fedha zake kiasi cha Sh Milioni 20 alizokabidhiwa na waendeshaji wa bahati nasibu hiyo ya Biko Tanzania, leo jijini Mbeya.
Mwanafunzi huyo ambaye ni msichana wa pili kufanikiwa kuzoa
mamilioni ya Biko kupitia bahati nasibu ya Biko, aling’ara katika droo ya Jumatano
iliyopita, ikiwa ni mwendelezo wa bahati nasibu hiyo kumwaga mamilioni kwa
kupitia mchezo wao unaotoa zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000,
20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, bila kusahau droo kubwa ya
Jumatano na Jumapili ya Sh Milioni 20.
Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Paul William Ntinika mwenye suti, akimpongeza
mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko, Linda Mhewa, aliyeibuka kidedea katika droo
ya 18 iliyochezeshwa Jumatano iliyopita. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Mbeya. Kushoto aliyeshika kipaza sauti ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope
Heaven. Kulia ni Afisa wa Benki ya NMB, jijini Mbeya. Picha na Mpigapicha wetu Mbeya.