Pages

Pages

Tuesday, January 15, 2013

Yanga kukipiga na Black Leopard Jumamosi




Kocha wa Yanga, Ernest Brandts

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MABINGWA wa zamani wa Tanzania Bara, Yanga SC, Jumamosi inatarajia kujitupa uwanjani kumenyana na Black Leopard inayoshikilia nafasi ya 12 katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini, mchezo uliopangwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, viingilio vimepangwa kuwa shilingi 5,000, viti rangi ya Chungwa Sh 10,000, VIP C Sh 15,000, VIP B Sh 20,000 wakatia VIP A Sh 30,000.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Kocha mkuu wa Yanga Ernest Brandts, alisema mechi za majaribio kwa Yanga itazisaidia timu kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

“Katika msimu wa mzunguko wa kwanza, sikuwa na timu ila baada ya kukabidhiwa timu, niliomba uongozi tufanye maandalizi ya kutosha sambamba na kupata mechi nyingi za majaribio ili kuweza kuweka timu fiti kwa ajili ya mzunguko ujao, hivyo mechi tulizozipata zitatusaidia katika kuongeza ubora wa timu,” alisema Brandts.

No comments:

Post a Comment