Friday, January 25, 2013
Mkwassa ataka ada ya fomu ipunguzwe uchaguzi TAFCA
Boniface Mkwassa
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWEKA hazina wa Chama cha Makocha Tanzania (TAFCA), Charles Boniface Mkwassa, amewataka viongozi wa chama chao wapunguze ada ya upatikanaji wa fomu ili wadau wengi washiriki katika uchaguzi huo.
Uchaguzi wa TAFCA ulisimamishwa baada ya kugunduliwa na Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho (TFF), kuwa haujakidhi viwango, hasa kutokana na uchache wa wagombea.
Akizungumza na Handeni Kwetu, Mkwassa alisema ugumu wa maisha, unawafanya wadau washindwe kununua fomu zinazouzwa kwa bei ghari.
Alisema jambo hilo linasababisha kuleta hoja ya kupunguza gharama za uchukuaji fomu, hasa kwa nafasi ya mwenyekiti na Katibu.
"Hili ni jambo gumu ambalo kwa hakika ibabidi tukae na kulizungumzia suala hilo, hasa kwa kupunguza gharama za upatikanaji wa fomu.
"Bila hivyo idadi ya wanaotaka nafasi za uchaguzi wa TAFCA, itazidi kuwa ndogo, jambo litakaloweka ugumu wa uchaguzi wetu," alisema.
Kwa mujibu wa Mkwassa, uchaguzi wa TAFCA umepangwa kufanyika tena Machi tano mwaka huu, mjini Dodoma, baada ya kusimamishwa na TFF.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment