Kipa wa Stars, Juma Kaseja
Na Kambi Mbwana, Dar es
Salaam
TIMU ya Taifa, (Taifa
Stars), itacheza na Cameroon katika moja ya mechi za kirafiki za Kalenda ya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date zitakazofanyika
duniani kote Februari 6 mwaka huu.
Mechi hiyo itafanyika
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni. Kikosi cha
Cameroon kinachoundwa na wachezaji wengi wa kulipwa wanaocheza katika nchi
mbalimbali duniani kitaanza kuwasili nchini Februari 3 mwaka huu.
Akizungumza jana jijini
Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Shrikisho la Soka nchini (TFF), Boniface
Wambura, alisema nchi kadhaa ziliomba kucheza na Taifa Stars katika tarehe hiyo
ya FIFA, lakini Kocha wa Stars, Kim Poulsen ameamua kucheza mechi hiyo dhidi ya
Cameroon ambayo nahodha wake ni mchezaji nyota wa kimataifa, Samuel Etoo Fils.
Congo Brazzaville,
Equatorial Guinea, Rwanda na Swaziland nazo zilikuwa zimeomba kucheza dhidi ya
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager. Ukiondoa Swaziland iliyotaka
mechi hiyo ichezwe Dar es Salaam, nyingine zilitaka kucheza nyumbani kwao.
Wakati huo huo, Kocha
Kim Poulsen atakutana na Waandishi wa Habari kuzungumzia maandalizi ya mechi
hiyo ikiwemo kutaja kikosi ambacho atakitumia. Mkutano huo utafanyika saa 5
kamili asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF).
No comments:
Post a Comment