Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi akiwaelekeza wakulima wa pamba kijiji cha Msai
wilayani Iramba, vipimo vya kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia
kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
Wakulima wa pamba
kijiji cha Msai wilayani Iramba, wakishiriki kwa vitendo mafunzo yya kupima
urefu kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili
waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emmanuel
Luhahula, asimamie kuvunjwa kwa bodi ya Ushirika wa Kijiji cha Msai Wilayani
Iramba ndani ya wiki mbili, kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi
milioni 50.
Dkt Nchimbi ametoa
agizo hilo mwishoni mwa wiki alipokuwa katika mkutano na wakulima wa Pamba wa
Kijiji cha Msai, ambao wamemueleza kutokuwa na imani na viongozi wa bodi hiyo
kutokana na upotevu wa fedha hizo na wakiwa hawajachukuliwa hatua yoyote.
Wakulima hao
wamemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa fedha zaidi ya milioni 50 zilitolewa na seikali
kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la ghala la ushirika wa kijijini hapo lakini
hakukuwa na ujenzi wowote uliofanyika huku wakifuatilia hawapewi majibu sahihi.