Pages

Pages

Monday, January 28, 2013

Wane Star, Kalunde Band kunogesha Lady In Red



Wane Star, akiwa jukwaani.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWIMBAJI ngoma za asili Wane Star na bendi ya muziki ya Kalunde, wanatarajiwa kutoa burudani kwenye onesho la mavazi la Lady In Red, litakalofanyika Februari 9 mwaka huu, katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena.

Akizungumza na Handeni Kwetu, muandaaji wa onesho hilo na kupitia Kampuni yake ya Fabak Fashion, Asia Idorous, amemtaja Wane Star na Kalunde kuwa ndio watakotoa burudani kwenye onesho hilo.

“Nimewapanga Wane Star na Kalunde kusindikiza onesho langu la Lady In Red, naamini watatoa mchango mkubwa kwenye suala zima la kunogesha onesho hilo la tisa la Lady In Red,” alisema Asia.

Katika onesho hilo wabunifu mbalimbali kama Khadija Mwanamboka, Ally Remtullah, Mustafa Hassanal, Dayana Magese, Rukia Walele na Annete Ngogi, wanatarajiwa kuonesha mavazi yao.

Asia aliwataja baadhi ya wadhamini wa onesho hilo kuwa ni Darling Hair, Redds, Vayle Spring, Kebbys Hotel, One Touch Solution na Nyumbani Lounge.

No comments:

Post a Comment