Pages

Pages

Wednesday, January 16, 2013

Mkuu wa Mkoa Tanga kufungua jengo la wazazi Kilindi



Mkuu wa Mkoa Tanga, Chiku Gallawa

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKUU wa Mkoa wa Tanga, kesho anatarajiwa kuzindua jengo la wazazi katika Zahanati ya kijiji cha Lumutio, Kata ya Pwagi, wilayani Kilindi mkoani Tanga, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake itakayodumu kwa siku nne.
Mkuu wa Wilaya Kilindi, Selemani Liwowa

Akizungumza na Handeni Kwetu leo mjini hapa, Mkuu wa Wilaya Kilindi, mkoani Tanga, Selemani Liwowa, alisema uzinduzi wa jengo hilo utakuwa wa kwanza kwa mkuu wao wa Mkoa.

Alisema taratibu zote kwa ziara ya Mkuu wa Mkoa zipo sawa, kwa ajili ya kutembelea na kujionea mambo mbalimbali yanavyoendelea katika wilaya hiyo ya Kilindi.

“Tutakuwa naye Mkuu wa Mkoa kwa siku zisizopungua nne, hivyo naamini mengi yaliyopangwa katika utaratibu wetu yatakwenda sawa, ikiwa ni pamoja na jengo la wazazi.

“Ni ziara nzuri kwa Mkuu wetu wa Mkoa, huku nikiamini kuwa atajionea mambo mengi katika wilaya yetu na kufikia uamuzi kama sehemu ya utawala kwa mkoa mzima wa Tanga,” alisema Liwowa.

Wilaya ya Kilindi imetokana na kugawanywa kwa wilaya ya Handeni mkoani Tanga, kama sehemu ya kufanikisha maendeleo ya watu wao, ambapo pia kumekuwa na changamoto nyingi, ikiwamo njaa na shida ya maji kwa miaka kadhaa sasa.

No comments:

Post a Comment