Pages

Pages

Thursday, January 24, 2013

Jaji Zainabu Muruke kupitia dhamana ya Lulu Jumatatu



Picha ikimuonyesha Lulu akipanda kwenye gari la mahabusu.



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
NI kusuka au Kunyoa? Dhamana ya msanii wa maigizo na filamu hapa nchini, Elizabeth Michael, maarufu kama (Lulu), inapitiwa Jumatatu, katika Mahakama Kuu.

Lulu akiwa katika pozi.


Dhamana hiyo itapitiwa mbele ya Jaji, Zainabu Muruke, ambapo itatoa picha kamili juu ya kesi ya mwanadada huyo na dhamana yake, baada ya kudaiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba, mapema mwaka jana.

Kwa miezi kadhaa, msanii huyo amekuwa akisota Segerea, kufuatia kesi hiyo inayomkabili mwanadada huyo.

Wakati msanii huyo anatoa ushahidi wa kesi yake hiyo, mwanadada huyo alidai kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake, marehemu Kanumba, hivyo kujenga hali ya wivu.

Muhtasari wa ushahidi huo ulisomwa Desemba 22 mwaka jana na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka, mbele ya Hakimu Mkazi, Augustino Mmbando.

Lulu katika kesi hiyo anatetewa na Mawakili Fuljensi Masawe, Kenedy Fungamtama na Peter Kibatala.

Picha kamili ya maisha ya Lulu itajulikana Jumatatu baada ya dhamana iliyoombwa kwa msanii huyo kupitiwa, huku mashabiki wa mwanadada huyo wakiendelea kuguswa na sakata la kesi ya msanii huyo mwenye makeke mengi katika tasnia ya filamu nchini.

No comments:

Post a Comment