Pages

Pages

Thursday, January 31, 2013

Chid Benz, Amini, Tunda Man kukamuana na Extra Bongo kesho

Chid Benz


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WASANII wane wa muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva, Chid Benz, Amini, Synag na Tunda Man, wamepangwa kufanya shoo ya wiki nne za zawadi inayoandaliwa na Extra Bongo, itakayofanyika Ijumaa, katika Ukumbi wa Ikweta Grill, Temeke.

Kufanyika kwa onyesho hilo ni maalum kwa ajili ya kutoa burudani kwa wapenzi wa muziki nchini, huku ikitoa zawadi mbalimbali, ikiwamo 150,000 na elfu 50,000, katika shoo iliyofanyika Meeda wiki iliyopita.

Akizungumza na Handeni Kwetu, Mkurugenzi wa bendi hiyo, Ally Choki, alisema kuwaita wasanii hao wa kizazi kipya ni kuongeza hamu ya utoaji wa burudani kwa wapenzi wao.

Alisema kila kitu kinaendelea vizuri kwa ajili ya wanamuziki wa bendi yake na wasanii hao wa Bongo Fleva kufanya mambo katika shoo hiyo.

“Tunafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa burudani ya wiki nne za zawadi inakuwa ya aina yake na watu wapate raha wanapokuwa ukumbini.

“Naamini kila kitu kitakuwa sawa, maana waimbaji hao tumeshafikia muafaka na wamekubali kuja kutoa burudani katika tukio hilo la Ijumaa,” alisema.

Onyesho hilo la Ijumaa atakosena msanii Linah, ambaye nafasi yake imejazwa na msanii Chid Benz, ambaye naye amejigamba kufanya makubwa katika shoo hiyo.

No comments:

Post a Comment